Rais Samia, unda tume huru kuchunguza mauaji ya Hamza

Wewe rejesha milion 400 na madini ya marehemu Hamza kwanza kubla haujaendelea kumbambikia marehemu tuhuma feki za ugaidi wakati yeye aliwaua Asikari wawili huku wengine wakiuana wenyewe kwa wenyewe kwa kutupa risasi hovyo
Serious? Kama ndio ukweli uwekeni wazi, Ukweli utatuweka huru
 
Tunataka kuujua ukweli, na ukweli hauwezi kutoka kwa mtuhumiwa. Polisi nao, kama wanataka kujisafisha na tuhuma hizi, nao wasisitize uchunguzi ufanywe na chombo kingine, kilicho huru.
 
Kuna mtu anakuwa gaidi kwa vile tu mtu fulani katamka kuwa ni gaidi?

Kauli yako ni ya kutafuta ridhisho la moyo wako, haina maana yoyote.
Unajaza server kutetea upuuzi wa gaidi na wewe Inaonesha una damu ya kigaidi
 
Leo DCI ametoa taarifa aliyoiita kuwa ni matokeo ya uchunguzi.

Kwangu mimi, na nadhani kwa Watanzania walio wengi, Polisi hawakuwa taasisi sahihi ya kufanya uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na Hamza dhidi ya polisi na pia kifo chake yeye mwenyewe Hamza.

Kwa nini?

Katika tukio la mauaji ya polisi na Hamza, kulikuwa na maelezo kuwa mauaji ya Hamza yalikuwa ya kulipiza kisasi dhidi ya polisi ambao kabla ya shambulio, walikuwa wamempora mali yake. Hii tayari ilikuwa ni tuhuma dhidi ya Jeshi la Polisi, ambayo ilikuwa na uzito wa wazi kutokana na shambulio la Hamza kuwalenga polisi na siyo mauaji holela dhidi ya raia.

Hoja ya pili, kwetu tulio wengi, au hatuna imani au tuna imani ndogo kwa jeshi la polisi kutokana na historia ya jeshi hili. Miaka ya nyuma polisi waliwahi kupora pesa kutoka kwa wafanyabiashara wa madini, kisha wakawaua hao wafanyabiashara, tena wakaenda kuwaulia msituni.

Wakatengeneza kile walichokiita kamati ya uchunguzi, nayo ikaleta taarifa kuwa eti wale wafanyabiashara walikuwa majambazi, na walikufa kwa kupigwa risasi wakati wanakimbia kutoroka mkono wa dola.

Uchunguzi wa baadaye ulithibitisha kuwa polisi walifanya kazi kama genge la majambazi ambapo wapo waliowapora wafanyabiashara wale, wengine wakawaua, na wengine wakawalinda wahalifu wenzao kwa kutoa taarifa ya uwongo dhidi ya marehemu.

Tunataka kuujua ukweli, na ukweli hauwezi kutoka kwa mtuhumiwa. Polisi nao, kama wanataka kujisafisha na tuhuma hizi, nao wasisitize uchunguzi ufanywe na chombo kingine, kilicho huru.

Uchunguzi wa kitaalam, wa kina na ulio wa kweli ndio utakaolisababishia Taifa kuepuka matukio ya kutisha kama haya yaliyotokea hivi karibuni.

Mungu naomba uwajalie hekima watawala katika kufanya maamuzi yenye kulihakikishia amani ya kweli Taifa letu.
Kwakweli ni aibu! Kuna haja ya IGP kuwajibishwa.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
DCI ametoa report yake kuwa Hamza alikuwa ni gaidi mfia dini.

Hoja zinazojenga haja ya uchunguzi:

1) Magaidi wafia dini hulenga imani za watu wengine tofauti na zao. Tunajua kuwa Hamza alikuwa muislam, kwa hiyo DCI Wambura anataka kutuambia kuwa Hamza ni gaidi mfia dini ya Kiislam aliyelenga dini ya Polisi. DCI atuambie polisi wa Tanzania dini yao ni ipi, maana shambulio lake lililenga polisi tu.

2) Siyo kila muuaji ni gaidi. Polisi wamewahi kuua raia wema wafanyabiashara wa madini. Na pia wameua watanzania wengi wanapokuwa kwenye mahabusu za Polisi. Na hili, Rais Samia amelikemea hivi karibuni. Je, kwa mauaji mbalimbali yaliyokuwa yamefanywa na polisi, inatosha kuthibitisha kuwa polisi wetu ni magaidi?

3) Jeshi la polisi halina historia ya weledi katika kuchunguza matukio tata ya uhalifu, lilishindwa kufanya hivyo kwa tukio la shambulizi dhidi ya Tundu Lisu, Azory Gwanda, Ben Saanane, na wengine wengi, ujuzi huu wa kufanya uchunguzi na kutoa majibu haraka kiasi hiki wameanza kuwa nao lini?

4) Jeshi la polisi limekuwa na sifa ya kuficha na kutetea uovu unaofanywa na jeshi la polisi. Kwenye mauaji ya wafanyabiashara wa madini, taarifa yao ilisema wafanyabiashara wale walikuwa majambazi, wakati ukweli ni kuwa polisi walifanya ujambazi dhidi ya raia kwa kutumia ofisi ya polisi. Kwenye mauaji ya mwanahabati Mwangosi, polisi walisema amepondwa na kitu kizito kutoka juu, picha za video ziliwaumbua, ndipo wakakubali kuwa ni polisi waliomwua. Kwenye tukio la Akwilina, kika mmoja anajua kuwa ni polisi ndio waliomwua lakini mpaka leo wamagoma kuhusika kwao. Kuanzia lini jeshi la polisi limekuwa na credibility ya kuweza kufanya uchunguzi unaosimama katika weledi?

5) Tabia mbaya ya uovu wa polisi katika kubambikia watu kesi imekuwa ndiyo sifa kuu ya jeshi la polisi. Na hili limethibitishwa hata na Rais wa JMT.

6) Ripoti zote kuhusiana na rushwa, polisi ndiyo taasisi ambayo kila mwaka inaongoza kwa ulaji rushwa. Mla rushwa, ana uwezo wa kujichunguza na kutoa ripoti inayoweza kuaminika?

Kamati/Tume ya uchunguzi iangalie mambo yafuatayo:

1) Uwezo wa jeshi la polisi katika kufanya uchunguzi

2) Maadili ya jeshi la polisi katika kusimama katika ukweli

3) Kwa kutegemea majibu ya hoja ya 1 na 2, itoe tamko kama taarifa ya uchunguzi aliyoitoa DCI inatakiwa kuaminika au kupuuzwa. Kama inastahili kupuuzwa, ipendekeze kuundwa kwa chombo kingine kuchunguza tukio la Hamza, na pia kuchunguza uwezo wa polisi kiweledi na kimaadili.
Wanataka kuhalalisha kesi ya Mbowe mbele ya jamii na dunia.
Badala yake wanaidhalilisha serikali.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Polisi asilimia kubwa ni wahuni Sana ,yaan wanaishi Kama Digi Digi ujanja ujanja mwingi.

Haki nakuambia yule Hamza aliporwa na hao polisi maana wamezoea pesa za bure bure ,hili la ugaidi ni kuficha tu aibu na kufunika hii picha mbaya kwa polisi.

Na hii issue imechezwa na vigogo wa polisi Ila walioucheza huu mziki ni vidagaa wa polisi
 
Hawawezi kuunda tume huru, wanataka kutulewesha na maneno yao ili tuwaamini, wanajua Tume huru inaweza kuja na maneno tofauti na tuliyoambiwa na DCI.
Kuna huyu jamaa anaitwa Seleman 0715132277 ni rafiki wa marehemu Hamza na pia ni rafiki mkubwa wa Polisiccm anasema kuwa rafiki yake Hamza hakuwa gaidi anao ushahidi kuwa Polisiccm waliuana wenyewe kwa wenyewe kwa kurusha risasi hovyo kasema marehemu Hamza aliwaua Polisi wawili tu hao wengine na wale waliojeruhiwa ni kazi ya Polisi kurusha risasi bila mpangilio
 
Polisi asilimia kubwa ni wahuni Sana ,yaan wanaishi Kama Digi Digi ujanja ujanja mwingi.

Haki nakuambia yule Hamza aliporwa na hao polisi maana wamezoea pesa za bure bure ,hili la ugaidi ni kuficha tu aibu na kufunika hii picha mbaya kwa polisi.

Na hii issue imechezwa na vigogo wa polisi Ila walioucheza huu mziki ni vidagaa wa polisi
Pesa milion 400 na madini ya Hamza viwekwenda na mungu atawalaani wote waliomdhulumu marehemu Hamza
 
Kwa nini isiundwe tume ya kuchunguza mauaji ya polisi?
Kwa mujibu wa Seleman ambaye ni msiri mkuu wa Polisi anadai marehemu Hamza aliwaua Polisiccm wawili tu, hao wengine waliuana wenyewe kwa wenyewe kwa kurusha risasi hovyo
 
Siku hizi imekua ni 'style' wanaojitambua kubambikiwa kesi za ugaidi.Huu mwendo wanaokwenda nao Jeshi la Polisi,wataichafua hii nchi.
 
Back
Top Bottom