Rais Samia: Tuwasaidie wananchi kupata haki zao

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
122
Reaction score
241
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka majaji kuwasaidia wananchi waweze kupata haki zao kwa kuwa wengi hawana uelewa wa nini wafanye. Lakini katika kuhakikisha wanapata haki zao kwa wakati ametoa wito wa mapitio ya sheria ili kupunguza michakato inayosababisha maamuzi ya kesi hizo kuchelewa.

"Natoa wito kwa Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Fedha, pamoja na mwanasheria mkuu na wote wanaohusika kushirikiana na kuzifanyia marekebisho sheria zote zenye mizunguko inayochelewesha kesi na upatikanaji wa haki mapema" - Rais Samia Suluhu

Aidha amesisitiza juu ya hatari ya taifa kupoteza amani ikiwa wananchi watakosa haki zao kwani haki ikipotezwa na amani inakua amna.

"Uwepo wa amani nchini ni chachu ya maendeleo ya kijamii, kisiasa. Mara nyinyi panatokea uvunjifu wa amani, ni kwamba haki imepotezwa, na haki ikopotezwa na amani inakuwa haipo" Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Fn3uWbOWQAEOVAT
 
Rushwa ni adui wa haki, ajabu amewakumbatia wala rushwa.
 
Watanzani tunaiona nuru mbele yetu hakika Rais Samia Suluhu anaendelea na ujenzi wa Tanzania mpya yenye haki upendo na amani
 
Siku hizi hatuitwi tena wanyonge aisee ashukuriwe kutupumzisha pale futi 6 chini
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka majaji kuwasaidia wananchi waweze kupata haki zao kwa kuwa wengi hawana uelewa wa nini wafanye. Lakini katika kuhakikisha wanapata haki zao kwa wakati ametoa wito wa mapitio ya sheria ili kupunguza michakato inayosababisha maamuzi ya kesi hizo kuchelewa.

"Natoa wito kwa Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Fedha, pamoja na mwanasheria mkuu na wote wanaohusika kushirikiana na kuzifanyia marekebisho sheria zote zenye mizunguko inayochelewesha kesi na upatikanaji wa haki mapema" - Rais Samia Suluhu

Aidha amesisitiza juu ya hatari ya taifa kupoteza amani ikiwa wananchi watakosa haki zao kwani haki ikipotezwa na amani inakua amna.

"Uwepo wa amani nchini ni chachu ya maendeleo ya kijamii, kisiasa. Mara nyinyi panatokea uvunjifu wa amani, ni kwamba haki imepotezwa, na haki ikopotezwa na amani inakuwa haipo" Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Fn3uWbOWQAEOVAT
Natoa wito kwa Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Fedha, pamoja na mwanasheria mkuu na wote wanaohusika kushirikiana na kuzifanyia marekebisho sheria zote zenye mizunguko inayochelewesha kesi na upatikanaji wa haki mapema" - Rais Samia
 
Watanzani tunaiona nuru mbele yetu hakika Rais Samia Suluhu anaendelea na ujenzi wa Tanzania mpya yenye haki upendo na amani
Kutamka neno Haki na Amani kwa mwanaccm ni ajabu sana.

Kongole kwa Rais
 
Naunga mkono hoja hii ya no 1,haki ndani ya mahakama zetu ni duni mno, CJ alikuwepo kwenye kikao hiki?,nasubiria comment ya Adv.Mayala kama atapitia uzi huu, maana ametoa uzi unaoonyesha sio yeye kuhusu suala la haki mahakamani hasa kwa mwanakijiji wa pale shinyanga
 
Back
Top Bottom