Rais Samia, tupitie upya tena mradi mkakati wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Omukajunguti ambacho kitaunganisha EAC

Kwasenga

Member
Feb 24, 2021
50
52
Rais wetu kipenzi,

Kabla ya mambo kubadilika, kulikuwa na mpango mkakati wa ujenzi wa kiwanja cha ndege eneo la Omukajunguti mkoani Kagera. Huu mradi ulilenga kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki, lakini si hivyo tu mama, kama umeenda Bukoba umeona ni jinsi gani ndege zinastrugle kutua katika kiwanja cha mjini Bukoba, imetokea mara nyingi ndege zimekuwa zikishindwa kutua hadi zinarudi Mwanza.

Inawezekana Rais wetu aliyeondoka hakuona umuhimu wa huo uwanja japo watangulizi wake akiwemo Rais wa awamu ya nne aliona umuhimu wake ndio wakaweka plan. Hata malipo ya fidia yalikuwa yashaandaliwa ila tukaona mradi unayeyuka.

Tunakuomba mama yetu uliangalie na hili kama unavyoangalia marejeo ya mradi wa Bagamoyo. Kwa kuwa hii miradi ni muhimu sana kwa taifa letu.
 
Infact sio kwamba tunahitaji msaada kwa sababu tukiamua kuitisha harambee kuanzia kwa dr. Rwechungura, prof. Rugemalila, hon. kokutona, mugendi snr, na nshomile wachache tu ni pocket money zetu tukichangia huo uwanja unakuwa kama wa amsterdam uholanzi. Point ni kwamba hatutaki kutumia wakandarasi wa kichina bado tupo kwenye mazungumzo na mkandarasi kutoka ujerumani.
 
Back
Top Bottom