Rais Samia tunaomba uturejeshee mradi wa uwanja wa ndege wa Omukajunguti-Kagera uliokataliwa na Rais Magufuli

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Uwanja wa Ndege wa sasa wa Bukoba ulivyo ni uwanja hatarishi sana na hii ndege ya @precisionairtz kupata ajali ni ndege ya 4 . Zingine zimewahi pata ajali kwenye mawe kutokana na ufinyu wa uwanja. Huu uwanja rasmi ulijengwa 1940 na serikali ya Uingereza kipindi cha ukoloni wakati wa vita ya pili ya Dunia. Baada ya kupata Uhuru ulikuwa unafanyiwa fanyiwa marekebisho .

Wabunge wa Kagera huko Bukoba waliendelea kupaza sauti zao Mama Seveline Mwijage aliyekuwa Mbunge wa CUF Viti Maalumu Sasa ni mwanachama wa ACT wazalendo na mjumbe wa kamati kuu,Masilingi akiwa Mbunge wa CCM Muleba Kusini, Wilfred Lwakatare akiwa Mbunge wa Chadema Bukoba Mjini na Prof. Annna Tibaijuka wamekuwa wakishinikiza uwanja mwingine kujengwa huo wa Bukoba haufai kwani ni uwanja hatarishi.

Serikali ya awamu ya 4 chini ya kikwete ikaweka suala la uwanja wa ndege wa Omukajunguti katika ilani ya CCM uchaguzi wa 2010.Mwaka 2013 tar 26 Jakaya Kikwete akafanya ziara Bukoba ,akatamka "Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kajunguti kuanza rasmi" na kuweka jiwe la msingi. Wakati ule Waziri wa Ujenzi akiwa Harrison Mwakyembe, Mwakyembe akawaambia mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) wafanye haraka kulipa fidia watu wahame uwanja ujengwe.

Uwanja wa Kajunguti design yake ulikuwa ni kama uwanja wa Japani wa Kansai International airport (KIX), ulikuwa pia uhudumie nchi jirani Rwanda, Burundi na Uganda.

Hadi serikali ya Kikwete inatoka madarakani 2015 ilikuwa tayari imeandaa fedha za fidia takribani Bil.9 za awali zilikuwa tayari zipo ,Mkandarasi aliyejenga JKN Airport, Mwanza Airport ndiye alikuwa ajenge uwanja wa ndege wa Omukajunguti, upimaji ulikuwa unaendelea ili Ujenzi uwanze.

Serikali ya awamu ya 5 ilivyoingia madarakani tuu ikapiga STOP Ujenzi wa uwanja wa Omukajunguti,tar 6,Nov 2017,Rais wa awamu ya tano akaamuru fedha zote za fidia TSH Bil.9 ziende kufanya upanuzi wa Uwanja huu wa Bukoba,akisema Ujenzi wa uwanja wa Omukajunguti haukuwa kwenye mpango wake . Hivyo mradi wa Omukajunguti Airport huko Misenyi ukajifia kifo cha Mende

Huu ni wakati sasa Mh. Rais Samia Mwigulu Nchemba kusaidia mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege.

Omukajunguti kuendelea ili kuepusha maafa zaidi.
 
Hivi viwanja vilivyo kandokando ya ziwa ni hatarishi iwapo tu havitaboreshwa kuzingatia mazingira yake. Uwanja wa Mwanza ndege ya mizigo minofu ya samaki iliwahi kudumbukia ziwani mazima, leo uwanja wa Bukoba hao hivyo hivyo, baadaye uwanja wa Musoma, Kigoma nao utaleta maafa. Ebu serikali ya awamu ya 6 ifuatilie kuhusu viwanja hivi vinginevyo tumekalia kuti bovu.
 
Uwanja wa Ndege wa sasa wa Bukoba ulivyo ni uwanja hatarishi sana na hii ndege ya @precisionairtz kupata ajali ni ndege ya 4 . Zingine zimewahi pata ajali kwenye mawe kutokana na ufinyu wa uwanja. Huu uwanja rasmi ulijengwa 1940 na serikali
Asante sana Abdul Nondo , wewe ni hazina kubwa hapa jf. Mtafute Mkuu britanicca muunde a pressure group kulipush hili jambo. Yeye mwenzio alianza nalo kitambo, Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana na ndiye aliyemtambulisha kwetu jamaa mmoja fulani hivi aitwae Katto.

P
 
Huyo Bibi angepaswa mpaka Sasa awe amejiwajibisha mwenyewe. Ninyi walamba asali hasa ACT wanafiki na wazandiki wa kutupwa. Nini na hilo li CCM ni wale wale. Shame on you.
 
Back
Top Bottom