Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa: Baada ya ujenzi Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga utakuwa wa kisasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Salaam,

Hatimaye ile ndoto ya siku nyingi ya Uwanja wa ndege sumbawanga uliokuwa hautumiki imetimia.

Leo Serikali inayoongozwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan imetia saini kuanza kwa ujenzi wa Uwanja.


photo_2023-04-29_19-40-17.jpg

ILIKUWAJE?
Awamu ya kwanza ya Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga ulifanywa na Kampuni ya Sir Fredrick Snow & Partners Ltd ya Uingereza ikishirikiana na Kampuni ya Belva Consult ya Tanzania kati ya mwaka 2007 mpaka mwaka 2009 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania.

Usanifu huu ulihusisha Viwanja vya Ndege saba nchini vikiwepo viwanja vya Ndege vya Arusha, Bukoba, Mafia, Kigoma, Sumbawanga, Shinyanga na Tabora.
photo_2023-04-29_19-40-40.jpg

Usanifu uliofanywa kwa Viwanja vyote Saba ulihusisha usanifu wa barabara za kutua na kurukia ndege; (Runways), barabara za viungio (Taxiways), Maegesho ya ndege (Apron), Majengo ya Abiria na vifaa vya waongoza ndege (Furnished Control Tower), barabara za kuingia viwanjani na maegesho ya magari.
photo_2023-04-29_19-41-05.jpg

photo_2023-04-29_19-42-08.jpg

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa asema Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga utakuwa wa kisasa
IMG-20230430-WA0000.jpg

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa

Akizungumza wakati wa tukio la utiaji saini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa Mnyaa amesisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unatarajiwa kuwa wa kiwango cha juu.

Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa baada ya maboresho hayo Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga unatarajiwa kuwa wa kisasa ukiwa na kila kitu muhimu kwa ajili ya huduma hiyo, pia utawezesha ndege kutua usiku na mchana.

Aidha, Waziri Mbarawa amempongeza Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilal kwa kuwa mstari wa mbee katika kufanikisha mchakato wa ujenzi unafanikiwa kutokana na kukumbushia mara kwa mara.
IMG-20230430-WA0002.jpg

Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Justin Malisawa

Mbarawa amesema ujenzi huo ambao Mkandarasi wake ni Kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd ya China, gharama ya mradi ni TSh. Bilioni 55.9 na muda wa utekelezaji wa mradi ni miezi 18 wakati muda wa uangalizi wa mradi ni miezi 12.
photo_2023-04-29_19-43-35.jpg

Amesema “Kiwanja cha Sumbawanga ni moja ya viwanja muhimu nchini kitakachoonganisha mikoa na Ukanda wa Magharibi, mikoa Jirani nan chi jirani pia, hata ndugu zetu wa DR Congo wanaweza kuja hapa na kupata huduma ya kwenda Dar kisha kwenda sehemu nyingine, tumefanya hivyo ili kuondoa changamoto ya usafiri.

“Uboreshaji wa uwanja huu utachochea shughuli za kiuchumi kama vile utalii, uwekezaji, uvuvi, usafirishaji wa mizigo na abiria.

“Tunatarajia Oktoba 2024 ndege ya kwanza itaruka kutoka Dar es Salaam kuja Sumbawanga.

“Uwanja wa sasa una barabara ya kuruka na kutua yenye kiwango cha changarawe, urefu wa Kilometa 1.516 na upana wa Mita 30.

“Kupitia mradi mpya kiwanja cha ndege kitaboreshwa na kufikia urefu wa Kilometa 1.75 na upana Mita 30, na ndege ya Bombadier Q400 na ndege ya ATR 72 zitaweza kuruka muda wote wa wiki.”

Aidha, ametoa wito kwa TANROAD kumsimamia vizuri Mkandarasi, pia wananchi watakaopata nafasi ya kufanya kazi katika mradi huo wawe wastaarabu na kutojihusisha na masuala ya udokozi.


Mkurugenzi TANROADS azungumza
IMG-20230430-WA0005.jpg

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila

Akizungumza katika tukio la utiaji saini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa Mnyaa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila amesema:

“Mradi wa Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii Mkoani Rukwa.

"Kiwanja hiki cha Ndege cha Sumbawanga ni moja kati ya viwanja vya ndege muhimu kinachounganisha mkoa huu na mikoa mingine nchini.

"Uboreshaji wa miundombinu ya kiwanja hiki cha ndege cha Sumbawanga utachochea shughuli za kiuchumi kama vile utalii kwenye mbuga yetu ya Katavi, usafirishaji wa mizigo na abiria na shughuli za kijamii kwa ujumla.

“Mwaka 2010, Serikali ilipata mkopo kutoka Benki ya Dunia ambao ulitumika kukarabati Viwanja vya Ndege vitatu kati ya viwanja 7 vilivyofanyiwa Usanifu.
IMG-20230430-WA0006.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga

“Viwanja hivyo na kazi zilizofanyika ni Kiwanja cha Ndege cha Bukoba ambapo kulifanyika ukarabati wa barabara ya kutua na kurukia ndege kwa kiwango cha lami, ujenzi wa barabara ya kiungio, maegesho ya ndege, ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani na eneo la maegesho ya magari kwa kiwango cha lami.

Vingine ni ujenzi wa miundombinu ya kuondoa maji taka na maji ya mvua kiwanjani, ujenzi wa jengo jipya la abiria pamoja na ununuzi wa vifaa vya uendeshaji na samani (furniture). Mradi huu ulikamilika Mwaka 2016.
IMG-20230430-WA0003.jpg

Ndugu Gerald Musabila Kusaya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa

“Kiwanja cha Ndege cha Tabora, Ukarabati wa barabara kubwa ya kutua na kurukia ndege (main runway) iliokamilika mwaka 2013; na ukarabati wa barabara ya pili ya kutua na kurukia ndege (Secondary Runway), barabara ya kiungio, maegesho ya ndege, ujenzi wa sehemu ya uzio wa usalama, usimikaji wa taa (AGL) na mitambo ya usalama DVOR/DME uliokamilika mwaka 2017.

"Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, upanuzi wa barabara ya kutua na kurukia ndege yenye urefu wa meta 1800 na upana wa meta 45 na barabara mbili za viungio. Ukarabati wa awamu hii ulikamilika mwaka 2013."

"Kuhusu Mkandarasi atayetekeleza kazi ni Kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd ya China. Mradi huu utajengwa kwa gharama ya Tsh. 55,908,086,039.80 ikijumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Muda wa utekelezaji wa mradi ni miezi 18 na muda wa uangalizi (defects notification period) wa mradi ni miezi 12.

"Mhandisi Mshauri ni M/s SMEC International Pty Ltd ikishirikiana na kampuni ya SMEC Ltd ya. Kampuni hii pia itasimamia mradi wa ukarabati wa kiwanja cha Ndege cha Shinyanga. Gharama ya usimamizi ni Dola za Kimarekani 2,602,343.00 na TZs. 23,735,554.00.

“Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kwa kutoa fedha za utelekezaji wa mradi huu. Wakala ya Barabara itasimamia utekelezaji wa mradi huu na kuhakikisha kuwa unazingatia viwango vya kitaaluma na unakamilika kwa wakati.”
IMG-20230430-WA0001.jpg

Mbunge wa Sumbawanga Aesh Khalfan Hilal

Pia soma >> Wizara ya uchukuzi imeutelekeza uwanja wa ndege na kugeuzwa shamba la mboga
 
Back
Top Bottom