Rais Samia tupatie Azimio la maadili ya mtanzania kuliepusha Taifa na mmomonyoko wa maadili

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Kwako Rais wetu, kiongozi shupavu na mwanamapinduzi wa kweli Mhe.Samia, ninakusalimu Kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nchi yetu katika vipindi tofauti katika awamu ya kwanza ya utawala, utawala wa Mwalimu ilishuhudia uwepo wa maazimio mbalimbali lakini linaloishi mpaka sasa ni lile Azimio la Arusha la 1967 liliweka msingi wa siasa za ujamaa na kujitegemea, msingi ambao upo mpaka Leo. Maazimio mengine ni Azimio la Iringa lililoitwa siasa ni kilimo la 1972 na Azimio la musoma la 1974 liliweka mkazo wa elimu ya msingi Kwa wote.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, maazimio hayo yalisaidia kuleta Mapinduzi na mageuzi makubwa kwenye uchumi wa nchi yetu na yanabaki kuwa ni kumbukumbu inayoishi.

Kwa kutambua mchango wa uwepo wa Azimio ni muda muafaka Taifa likaandaa Azimio jipya ili kuliepusha na mmomonyoko wa maadili Kwa vijana na kuweka misingi ya uwajibikaji Serikalini na kuweka misingi ya kimaadili Serikalini ili kuliondolea aibu ya rushwa na ufisadi.

Rais Samia napendekeza pawepo na AZIMIO LA MAADILI YA MTANZANIA kama nyenzo Mojawapo itakayokusaidia kushughulikia masuala yote ya kimaadili katika jamii zetu na Serikalini ndani ya Taifa letu.

Ahsante
 
Wa kizazi hiki hatuwezi kuwa na azimio, hatuna fikra yakinifu kama wazee wa zamani
 
Back
Top Bottom