Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,626
- 41,264
Sikumfahamu kwa ndani marehemu Mfugale lakini kwa yale aliyoyafanya, hakika ameacha alama katika maisha yake ya hapa Duniani. Hakuna shaka juu ya uchapakazi wake, hakuna shaka juu ya uzalendo wake, na mapenzi yake kwa Taifa. Hakuna shaka juu ya uwezo wake mkubwa wa utaalam wake. Amevitumia vema vipaji alivyopewa na Mungu.
Mungu wetu tunakushukuru kwaajili ya maisha na utumishi wake ndugu yetu Mfugale. Kwa kuwa umemwita kwako kwa wakati ulioona unafaa, japo ni kwa majonzi, tunalazimika kuyapokea mapenzi yako.
Tunakuomba muumba wetu, iipe faraja familia ya huyu ndugu yetu. Kwaajili ya mema mengi aliyoyafanya mzazi na mwanafamilia wao kwao kama familia na Taifa, itoshe kukushukuru wewe uliyemfanya akawa kama alivyokuwa.
Kwa mapenzi na huruma yako, tunakuomba yale mema aliyoyafanya kwaajili ya watu wako, yakatoshe kuwa sadaka ya yale ambayo hakuyatenda vema.
Kwetu tuliobakia, matendo mema ya huyu ndugu yetu yakawe shule, injili na mafunzo kwa maisha yetu.
Kuambiwa sababu ya kifo chake hakuwezi kubadilisha chochote kwa marehemu, lakini ni jambo ambalo linaondoa gossiping. Kifo na ugonjwa, siyo kosa la yeyote, na hakuna mwenye uwezo wa moja kwa moja katika kuvizuia. Sijui kwa nini siku hizi baadhi ya watu, na hasa viongozi, sababu za vifo vyao hazielezwi.