Rais Samia: Tanzania kuchora ramani yake mpya

Rais Samia: Tanzania kuchora ramani yake mpya

Mikataba hiyo iliyowekwa na wakoloni lazima tuiheshimu. Vinginvyo unaonaje Kenya wakadai sehemu za Kilimanjaro, au Serengeti ni zao? Kumbuka hata ziwa Nyanza halimilikiwi kwa usawa kati ya Tanzania, Kenya na Uganda.
mkataba uliwekwa wakati wa wajerumani, tulipo kuwa chini ya uingereza ukavunjwa. tulipopata uhuru tukachora mpaka wetu katikati, tumeishi hivyo tukitumia maji hayo hadi leo. unataka heshima gani sasa wewe mmalawi?
 
Wanazunguka Tanzania nzima Kupima Square mita za mlaba but hiyo pesa ni Nyingi Milioni 400 ingetosha
Tufanye bilioni 3 pamoja na vifaa na kila kitu, huu ni utapeli kuna drones zinaweza fanya hizi kazi kupitia vyuo vya ardhi Tabora, Morogoro na Dar.
 
Ramani ni ya mwaka 1978 na Katiba ni ya mwaka 1977 Bi-mkubwa haoni kipi kinatakiwa kiwe Cha kwanza kufanywa upya? Watanzania kazi tunayo!
 
Hilo nalo jipya, tunachora ramani ya nini? Kuna eneo tumeongeza au kupunguza.
 
Je iyo ya zamani imeleta impact gani kijamii na kiuchumi, na hiyo wanaendea italeta impact gani?
Na hapo kati kati tukiwa na ya zamani tulipungukiwa nini?
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo mbioni kuanza mchakato wa kuchora ramani mpya ili kuendana na mabadiliko yaliyojitokeza.

Pia, Soma: Rais Samia aikabidhi Wizara ya Ardhi magari 70

Rais Samia amesema mara ya mwisho ramani ya Tanzania ilichorwa mwaka 1978 huku vitu vingi vikibadilika.

"Hii tukimaliza, itatuwezesha kuchora ramani mpya ya Tanzania, ramani ya mwisho ya Tanzania, ilichorwa mwaka 1978, kwa kiasi kikubwa kuna mabadiliko makubwa hata ukichua tu, Jiji la Dar es Salaam, la mwaka 1978 na leo tofauti, mfumo huu utatuwezesha kutengeneza mipango ya kidijitali," amesema Rais Samia.

Watanganyika! Haya subilini muone mipaka ya upande wa bahari inayogombewa na wajomba otakavyonyoshwa safari hii.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo mbioni kuanza mchakato wa kuchora ramani mpya ili kuendana na mabadiliko yaliyojitokeza.

Pia, Soma: Rais Samia aikabidhi Wizara ya Ardhi magari 70

Rais Samia amesema mara ya mwisho ramani ya Tanzania ilichorwa mwaka 1978 huku vitu vingi vikibadilika.

"Hii tukimaliza, itatuwezesha kuchora ramani mpya ya Tanzania, ramani ya mwisho ya Tanzania, ilichorwa mwaka 1978, kwa kiasi kikubwa kuna mabadiliko makubwa hata ukichua tu, Jiji la Dar es Salaam, la mwaka 1978 na leo tofauti, mfumo huu utatuwezesha kutengeneza mipango ya kidijitali," amesema Rais Samia.

Hv kuna ramani ukiitaka hauwezi kuipata Google map? Au wenzetu wanataka kuchora ramani gani?
 
Back
Top Bottom