Rais Samia: Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya Afya na Elimu baadhi zinatozwa kodi kwa sababu zinafanya biashara

kidereko

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
882
1,254
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ameeleza kuwa Serikali inazitoza kodi taasisi za dini zinazotoa huduma za afya na elimu kwa sababu baadhi zinafanya biashara na si kutoa huduma.

Rais Samia ameeleza hayo leo Alhamisi Julai 8, 2021 wakatia akifungua mkutano mkuu wa 31 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) unaofanyika mkoani Morogoro.

Amesema wakati mwingine Serikali inakuwa na hospitali na taasisi ya dini inajenga kituo cha afya kwenye eneo hilohilo.

“Hapa ndipo panapokuja lile suala linalolalamikiwa la ushindani wa huduma, taasisi ya dini ina hospitali yake hapo Serikali inajenga kituo cha afya hapo kwa kuona wananchi wakienda huku wanatoa pesa nyingi zaidi kuliko wakipata huduma serikalini.”

“Pia inafanya Serikali kufanya vitu mara mbilimbili kwa kuweka huduma ileile inayopatikana kwa kuweka sehemu moja ambayo sio mtindo mzuri,” amesema

Amesema lengo la Serikali ni kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi ambapo suluhisho lake ni kufanya kazi kwa uwazi na kuaminiana ili wanaotoza kodi wajue taasisi za dini hazifanyi kazi kibiashara.

“Ni lazima mahesabu yawe wazi, watoza kodi waweze kukagua na wajue hali halisi inavyokwenda katika taasisi hizo, ni kweli kumetokea shida mbili tatu katika mifumo hii kuna shule zinazopata misaada kutoka nje, wanapokea wanatoa huduma ya elimu au afya lakini bado taasisi zetu za kodi zimeenda kutoza kodi,”

“Hapa utaona wale wamekusanya jasho la watu wengine sisi tunaenda kutoza kodi, haya yote ni kwa sababu hatukuwa na uwazi, niombe sasa tufanye kazi kwa uwazi na kuaminiana,” amesema.

Rais Samia pia ameeleza kuwa huduma za afya na elimu zimekuwa zikitolewa na sekta binafsi ambapo gharama zinazotolewa kwenye elimu na afya zinalingana ndio sababu na taasisi za dini zikaonekana zinafanya biashara.

“Wale wanaofanya kwenye sekta binafsi malipo yao na viwango ni vilevile vinavyotozwa na taasisi za dini,” ameeleza.
 
Hizi taasisi za dini wala zisijitee kwa chochote,ni wafanyabiashara kama wengine tu,tena gharama zao zipo juu acha walipe Kodi tu.

Kuna hospitali wilaya fulani inamilikiwa na taasisi ya kidini ila Mgonjwa akipelekwa kutoka kituo cha serikalini kabla hio Ambulance haijaondoka wanataka walipwe hela yao,kama mgonjwa hana pesa wanaambiwa ondoka nae hatuwezi kumpokea,halafu ndio useme taasisi za dini zinatoa huduma?

Halafu Unakuta lihospitali lina jina eti la Mtakatifu gani sijui,utakatifu upi wakati mnakataa wagonjwa wasio na kipato?

Hospitali hizi hizi tunazichangia kanisani tukiziita ni zetu lakini ugua uone kama huna hela utatibiwa kisa wewe muumini.

Ni bora hata hospitali za wapagani
 
Viongozi wa dini ndilo kundi linaloshika nafasi ya pili kwa kuishi maisha ya anasa baada ya wanasiasa! Majumba ya kifahari, magari makubwa, mipete ya gold na vidani.

Yanapenda kukaa kwenye viti vya mbele kama wasanii na Yesu alikataza!

Walipe kodi tu maana hakuna namna! Kwanza kulipa kodi ni heshima na wakiheshimika hata yale matamko yao yatapewa heshima!
 
Hizi taasisi za dini wala zisijitee kwa chichote,ni wafanyabiashara kama wengine tu,tena gharama zao zipo juu acha walipe Kodi tu.

Kuna hospitali wilaya fulani inamilikiwa na taasisi ya kidini ila Mgojwa alipelekwa kutoka kituo cha serikalini kabla hio Ambulance haijaondoka wanataka walipwe hela yao,kama mgonjwa hana pesa wanaambiwa ondoka nae hatuwezi kumpokea,halafu ndio useme taasisi za dini zinatoa huduma?

Halafu Unakuta lihospitali lina jina eti la Mtakatifu gani sijui,utakatifu upi wakati mnakataa wagonjwa wasio na kipato?

Hospitali hizi hizi tunazichangia kanisani tukiziita ni zetu lakini ugue uone kama huna hela utatibiwa kisa wewe muumini.

Ni bora hata hospitali za wapagani
Dah, taasisi ya kishetani iyo
 
Back
Top Bottom