Wabunge wapya walioteuliwa kuwa wabunge ni pamoja na Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Kakurwa Ali, Mbarouk Nassor Mbarouk na Liberata Mulamula.
Rais Samia Suluhu akiteua Baraza la Mawaziri amesema...
''Kuondoka kwa Mpango kumefanya nifanye mabadiliko kidogo kwenye Baraza la Mawaziri na nitatangaza hapahapa zege halilali''
Baadhi ya Wizara zimefanyiwa Mabadiliko na nyingine zimebaki kama zilivyokuwa.
Ummy Mwalimu - Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Mohammed Mchengelwa - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Selemani Jafo - Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Geoffrey Mwambe - Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji
Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha na Mipango
Profesa Palamagamba Kabudi, - Waziri Wizara ya Katiba na Sheria