Rais Samia, suala la ardhi la Shirika la Maendeleo Dar es Salaam na wananchi ni saizi yako. Futa hati, gawia wananchi, DDC waje Serikalini tumalizane

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,009
20,683
Hawa watu wa DDC hata kama Wana hati, hawakutimiza sharti la msingi la kulinda ardhi yao.

Hili ni shirika la umma, liko chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, sioni sababu kwa nini lisumbue wananchi.

Rais akilifutia umiliki kwani litamfanyaje? Si ni shirika la umma? Na kiongozi ni Rais? Namshauri SSH, tena aende kwa mguu wake akatangaze kufuta hati hiyo, ardhi igawiwe wananchi, kama Kuna iliyo wazi, basi DDC ndio wabaki nayo.

Shirika la maendeleo Dar es Salaam, hao ni wakazi wa Dar es salaam, shida nini? Hati ifutwe halafu tuone mtu wa DDC atakayekoroma.

Namshauri Rais asiwape umaarufu wa burebure hawa watu wachache. Ni wakati Sasa azidhibiti kura za Mbopo na mabwepande. Washauri wa Rais mko wapi?
 
Back
Top Bottom