Shirika la DDC Kuchukua Ardhi huko Mbopo, Kinondo na Mabwepande kutoka kwa Wananchi ni Uporaji

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,036
3,478
Maeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.

Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?

Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?
 
Kwa stahili hiiii, Unadhan Wananchi wa Tanzania, utawaeleza nn kuhusu JPM Hadi wamuone mbaya??.

Mimi nadhani ni wapumbavu tu ndo wanaweza kupambana na Hayati JPM
wananchi wapi? labda wa mwanza waliovamia airport magufuli akasema wasiondolewe kwa sababu walimpa kura. Lakini wananchi wa morogoro road waliokuwa na hati miliki zinazolipiwa serikalini wakabomolewa bila huruma kwa sababu wengi wao siyo wasukuma wenzake!
 
Hivi kirefu cha ddc ndo ddc mliman park au? Wana tofauti gan na cda dodoma?
 
Hakuna Mtu aliekua na hati Miliki barabara ya Morogoro.

Mimi nilikua moja ya wahanga.

Usiongee usichofahamu mkuu
 
Hivi kirefu cha ddc ndo ddc mliman park au? Wana tofauti gan na cda dodoma?
Shirika la Uchumi la Jiji la Dar es Salaam (DDC)

Shirika la DDC lilianzishwa kama kitega uchumi cha Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam kwa lengo la kufanya shughuli za uzalishaji, biashara na burudani kwa ajili ya wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
 
Kinondo kupo vizuri sana juzi kati nilikuwa napita pita nikaonyeshwa eneo la mtoto wa mstaafu mmoja mkubwa

Amehodhi eneo kubwa sana limezungushiwa ukuta waliojenga ndani ya eneo nyumba zimeanza kubomolewa

Sasa sijajua nani mvamizi na nani mmiliki halali wa eneo

Mabwapande inajulikana miaka nenda rudi ni eneo lenye utata. Unaweza ukajenga leo kesho tingatinga inakuja kuvunja nyumba yako unaitwa mvamizi
 
Hivi kirefu cha ddc ndo ddc mliman park au? Wana tofauti gan na cda dodoma?
Kirefu chake ni 'District Development Cooperation-DDC' likijumuisha wilaya zote za wakati huo za Dar Es Salaam ambalo lilianzishwa na serikali mnamo tarehe 18/5/1971 na miradi yake ilikuwa DDC Kariakoo, DDC Mlimani, DDC Magomeni, DDC Keko, Garage, Mashamba nk
 
Kwa stahili hiiii, Unadhan Wananchi wa Tanzania, utawaeleza nn kuhusu JPM Hadi wamuone mbaya??.

Mimi nadhani ni wapumbavu tu ndo wanaweza kupambana na Hayati JPM
Mpumbavu ni wewe unayedhania Magufuli ana nguvu wakati analiwa na mchwa huko Chato.

Acheni UJINGA wa kumfanya Magufuli eti alikuwa mtetezi wa wanyonge. Kwanza kukubali kuitwa mnyonge ni LAANA tu
 
Kuna wakili mmoja nimesoma mahali anadai iwapo mtu atavamia eneo lisilo lake na akaliendeleza kwa miaka 12 mfululizo bila mmiliki halali kujitokeza basi eneo hilo linatambulika lake kisheria.

Hii sheria ya ardhi ipo kweli au jamaa ni wale bush lawyers?
 
Ninajua vizuri sana hili sakata na kesho nitakuja na Uzi kuhusu eneo hili ambalo aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwan Kikwete aliwauzia wawekezaji kutoka Uturuki bila uhalali Sasa mwekezaji aliyeuziwa anadai eneo lake anataka kujenga malls. Ridhiwan aliwadanganya Waturuki eti eneo hilo ni pori na akaliondoa kwenye ramani ya google. Dogo jizi sana.
 
Maeneo kadhaa huko Mbopo, Kinondo na sehemu fulani huko Mabwepande shirika la DDC linadaiwa kuvamia raia na kuyapora maeneo wakidai ni ya kwao. Nyumba zinavunjwa viwanja walivyonunua wananchi kwa taratibu kabisa na uwepo wa wajumbe wa maeneo husika lakini wanakuja kuwapora huu ni uvunjifu wa HAKI za binadamu na haikubaliki kunyanyasa raia wa nchi hii.

Ombi kwa serikali kuu ingilieni mtafaruku huu utasababisha uvunjifu wa amani pasipo sababu zozote. Muda wote walikuwa wapi hao DDC wakavizia wananchi wameuziwa na kujenga nyumba kisha waende kupora ardhi na kuvunja nyumba zao bila fidia?

Mada iko mezani wadau na wanasheria jitokezeni kukomesha uonevu huu. Mbunge wa Kawe yuko wapi?
Hiyo ddc ipo hao wavamizi wakiwa watoto
 
Siku Zote nasali njia Bora ya kuliweka Jiji katika mpangilio Hawa DDC walichelewa sana hadi Hawa wavamizi wakajimilikisha maeneo mengi Kama utulivu, Mwendokasi, Islamic na Zimbabwe, kote Huku wamejenga vibanda vya hovyo na kaharibu Mazingira!! Chonde chonde Serekali isimame mahala pake na kupima haya maeneo ili watu waweze kuwekewa barabara na huduma nyingine za kijamii, Najua maji yamewekwa katika mtazamo Watu watakapopimiwa huduma iwepo!!Mbona NSSF waliweza kuondoa wavamizi why not DDC!?
 
Hiyo ddc ipo hao wavamizi wakiwa watoto
Ukipita maeneo husika, Manzese ni kama masaki Sio Kwa uchafuzi uliopo!! Na nasikia Hawa wavamizi walinunua viwanja Kwa tzs 150,000 (10*10m)kutoka Kwa wajumbe WA chama 2017, Makonda alitumia nafasi hiyo pia kupora baadhi ya maeneo kwenye huu mvurugano na wengine kuporwa kiitikadi, Mfano Sumayi wakati huo CDM
 
Ninajua vizuri sana hili sakata na kesho nitakuja na Uzi kuhusu eneo hili ambalo aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwan Kikwete aliwauzia wawekezaji kutoka Uturuki bila uhalali Sasa mwekezaji aliyeuziwa anadai eneo lake anataka kujenga malls. Ridhiwan aliwadanganya Waturuki eti eneo hilo ni pori na akaliondoa kwenye ramani ya google. Dogo jizi sana.
Usije kuwa na chuki binafsi!? Ila toa facts
 
Kuna wakili mmoja nimesoma mahali anadai iwapo mtu atavamia eneo lisilo lake na akaliendeleza kwa miaka 12 mfululizo bila mmiliki halali kujitokeza basi eneo hilo linatambulika lake kisheria.

Hii sheria ya aridhi ipo kweli au jamaa ni wale bush lawyers?
Ila Hawa wavamizi ni WA 2017 TU, waondoke TU Sio Kwa kuharibu Jiji kihivyo, kizazi chetu kitakuja kutushangaa
 
Back
Top Bottom