Rais Samia: Sisi tunalumbana kuhusu Bandari, wenzetu wanatumia fursa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi wateule Ikulu jijini Dar es Es Salaam leo tarehe 14 Julai, 2023



RAIS SAMIA: SISI TUNALUMBANA KUHUSU BANDARI, WENZETU WANATUMIA FURSA
Rais wa Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo wakati wa kuwaapisha viongozi wateule Ikulu Jijini Dar es es Salaam, leo Julai 14, 2023 ambapo amesisitiza kuhusu kutumia fursa za kupata maendeleo pindi zinapopatikana.


RAIS SAMIA: KILA MABADILIKO YANA UGUMU WAKE
Rais wa Samia Suluhu Hassan anasema “Mkiwa na nia safi na ya kujenga Nchi msiogope kuja na mawazo ya kubadilisha mwekeleo wa Nchi, kila mabadiliko yana ugumu wake, hakuna mabadiliko marahisi.”

Ameongeza “Watu wakizoea kushoto ukiwaambia geuka kulia watalalamika, msiogope kuna na madiliko ya uelekeo wa Nchi yetu.”

 
Hii michezo inafanywa kwa mkupuo ili kupunguza nguvu ya kupinga mkataba wa hovyo wa bandari, Samia amepwaya sana kwenye hili.

Kama Samia anajielewa hata kidogo azungumzie la bandari hapo kwenye huo uapisho, japo najua utetezi wa kijinga kama ule wa Mbarawa ndio utakuwa kichwani mwake pia.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi wateule Ikulu jijini Dar es Es Salaam leo tarehe 14 Julai, 2023

Uapisho huu unafuatia mabadiliko yaliyofanywa katika Baraza la Mawaziri na kuunda wizara mpya.

Ikumbukwe Rais Samia alivunja Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuunda Wizara tatu; Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Katika Mabadiliko hayo, alimteua aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.

Pia alimteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha.

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji ofisi ya Rais.

 
Hii michezo inafanywa kwa mkupuo ili kupunguza nguvu ya kupinga mkataba wa hovyo wa bandari, Samia amepwaya sana kwenye hili.

Kama Samia anajielewa hata kidogo azungumzie la bandari hapo kwenye huo uapisho, japo najua utetezi wa kijinga kama ule wa Mbarawa ndio utakuwa kichwani mwake pia.
Azungumzie la bandari ili kiwe nini.
Hilo la bandari ongeleeni nyie, wenye bandari yao wanaendelea tu na michakato yao
 
Anabomoa utaifa wetu, wewe utakuwa na matatizo ya upeo kifikra huoni vizuri.

Unapokuwa na kiongozi bubu kwenye masuala ya msingi yanayowavuruga anaowaongoza huyo anajenga nini?
Nyie ndio mnabomoa.
Mkilala mkiamka bandariiii bandariiii bandari.
Watu wako busy na mishe zao
 
Judge Mkuu naona karusha Dongo ,fupi lakini Kali sana...sasa sijui kama walengwa wamemwelewa!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom