Rais Samia: Serikali Yangu Sio ya Maneno ni ya Vitendo

Rais Samia: Serikali Yangu Sio ya Maneno ni ya Vitendo

My Take
Kazi Iendelee

=======

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona vijana wa Kitanzania wakijenga uchumi imara pamoja na kujenga ustawi wa maisha yao na familia zao.

Ameyasema hayo leo Juni 24, 2023 jijini Arusha wakati alipowasili na kusalimiana na wananchi wa mkoa huo ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Juni 25, mwaka huu.

“Tunataka kuona vijana wa Kitanzania wakiwa wako ‘busy’ kuzalisha mali na kujenga ustawi wa maisha yao na kujijengea uchumi wenye hadhi, uchumi imara kwa wenyewe na familia zao,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufungua nchi na kukaribisha sekta binafsi ili zije zifanye kazi na Tanzania katika maeneo mbalimbali ili kuzalisha ajira kwa vijana na kujenga kesho yao iliyo njema.

Mbali na hayo, Rais Samia amesema Serikali yake haina maneno mengi bali inafanya kazi kwa vitendo na kuangalia wapi inakusudia kwenda ili kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Swahili times
 
Hii Nchi siyo Mali ya Samia na chawa wake, amepewa tu dhamana ya kuongoza basi!

Hatutakubali kuingizwa kwenye mikataba ya Kimangungo !

Rais Samia usisaini huo mkataba urudishe Bungeni na Wananchi wapewe muda wa kutosha watoe maoni yao!

Ikibidi uondolewe kabisa na kama kuna uhitaji wa uendeshaji na uboreshaji wa Bandari zetu basi sheria za manunuzi zifuatwe kama kawaida!

Hao "wajomba " zako wa DP World washindanishwe na wengine Duniani!

Vinginevyo 2025 hutoboi !,
Mimi ni mwana CCM na kwakweli Rais Samia ulikuwa unaenda vizuri ila hili la DP World limekuchafua sana na approval rating yako imeshuka sana!

Hao Chawa wako wasikudanganye, pembeni wanakuzomea ni wachumia tumbo tu hao!
 
Vitendo vya kuuza nchi

C3E4751D-A4E5-404E-95A9-E4DF387E5922.jpeg
 
My Take
Kazi Iendelee

Huyu mama,anatia aibu nchi,kwanza ilipangwa akutane na boss wa USAID arusha,akaingia mitini,
Tangu aingie hajahojiwa hata na chombo kimoja Cha kimataifa,bbc Swahili Wana ofc bongo, msasani kwa mwalimu,kwanini haendi,kanajificha TU nyumba ya upuuzi wa ccm,

Eti wabunge wanashindana kula ubwabwa!!really !!

SI Bora wangeandaa bonanza la mpira au riadha na watoto wa mitaani,nchi imejaa kenge watupu,ikulu,kwenye media,wale kenge wa wcb waliopo Dubai, wanasema wamefsnya mahojiano na DP, Sasa hayo mahojiano kwanini hawayaweki mtandaoni,?ili tusikie yes no yes no!
 
Hiyo staili kaitoa kwa yule msanii wa Msoga, JK...ni upepo tu utapita!.
Huyu msanii wa Zenj ye anaweka pamba masikioni walalahoi asitusikie kilio chetu.
 
Jambo zuri hapa Jf kila kiongozi huwa anakuwa wajinga na machawa wa kumsapoti kwa chochote.
Kila awamu hao members hubadilika,walikuwepo humu wanazi wa Kikwete,wakaja wa Magufuli na sasa SAMIA
 
Jambo zuri hapa Jf kila kiongozi huwa anakuwa wajinga na machawa wa kumsapoti kwa chochote.
Kila awamu hao members hubadilika,walikuwepo humu wanazi wa Kikwete,wakaja wa Magufuli na sasa SAMIA
Wanazi au sio!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom