Rais Samia: Serikali Yangu Sio ya Maneno ni ya Vitendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amewasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo ataongoza maadhimisho siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya itakayofanyika kitaifa mkoani humo tarahe Juni 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda.

Rais Samia amezungumza baada ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kumpokea katika eneo la Tengeru kuanza kuimba nyimbo zenye maneno "Samia Sema, Sema usiogope sema..."

Rais Samia aliwajibu akisema
"Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi (huku akiweka mkono wake masikioni) naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya”

Wanajamvi, Rais wa Nchi kasema sisi tuseme tu yeye anapiga kazi tu
---

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati aliposimama kuwasalimia wakazi wa Tengeru mkoani Arusha amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda. Rais Samia amesema:

"...Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya...”
---

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona vijana wa Kitanzania wakijenga uchumi imara pamoja na kujenga ustawi wa maisha yao na familia zao.

Ameyasema hayo leo Juni 24, 2023 jijini Arusha wakati alipowasili na kusalimiana na wananchi wa mkoa huo ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Juni 25, mwaka huu.

“Tunataka kuona vijana wa Kitanzania wakiwa wako ‘busy’ kuzalisha mali na kujenga ustawi wa maisha yao na kujijengea uchumi wenye hadhi, uchumi imara kwa wenyewe na familia zao,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufungua nchi na kukaribisha sekta binafsi ili zije zifanye kazi na Tanzania katika maeneo mbalimbali ili kuzalisha ajira kwa vijana na kujenga kesho yao iliyo njema.

Mbali na hayo, Rais Samia amesema Serikali yake haina maneno mengi bali inafanya kazi kwa vitendo na kuangalia wapi inakusudia kwenda ili kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Credit: Clouds Media
 
Attachments

  • IMG_0899.MP4
    17.4 MB
Akauze na bandari ya Zanzibar kama kweli ana nia njema. Asitufanye watoto tushajua malengo yake
Siyo lazima tuwe werevu wote hata wajinga mna nafasi yenu hivyo hautushtuwi sisi ni vitendo tu maneno endeleeni kuongea.
 
Sijawahi kwenye maisha yangu kuwa na mashaka na rais yeyote, ila huyu mama hapana!

Tangu aliposema ukiscratch my back i will scratch yours,mmmhh wanawake tunajuana tu udhaifu wetu japo sio wote, ila kwa mama huyu alopata urais kwa kudra, hapana kabisa imani naye!
Hujaandika hoja zako kinachokufanya usimuelewe hapo tunahitimisha ni chuki tu na husda kwa mwanamke mwenzio pole sana.
 
Wiki iliyopita mama katangaza kilometa 2000 za barabara ya lami kujengwa kwa wakati mmoja hii hajawahi kutokea tukumbuke ni ndani ya miaka hii miwili. Mtakufa kwa kihoro
 
Kwa sehemu kubwa kashapoteza Imani kwa wale waliokuwa wakimuunga mkono. Waliobaki hivi sasa ni wale ignorant people na wale chawa wake.
Ndani ya miaka miwili kwa uchache sana nakuorodheshea mambo yaliyofanyika
1. Maslahi ya watumishi mishahara na madeni amelipa
2. Amesaini kandarasi za uendelezaji wa reli sgr mikoa ya tabora mwanza mpaka isaka
3.amejenga madarasa ya shule za msingi zaidi ya 5000
4.amejenga health centers zaidi ya 500
5.amelipa kandarasi navumaliziaji bwawa la nyerere sada ni zaidi ya 90%
5. Juzi TANROADS wamesaini kuanza ujenzi wa barabara za lami KM 2035 zinaanza kwa mara 1 hii haijawahi kutokea ( kumbuka kuna ujenzi wa barabara zingine unaendelea)
6. Bandari ya Dar inakwenda kuongeza mapato kutoka trillion 7 hadi trillion 26
7.watu hawapotei wala kutekwa
8.Ujenzi wa hospital za wilaya na mikoa unaendelea
9. BRT miradi ya ujenzi inaendelea

Kwa uchache sana nimetaja hayo ila mambo ni mengi sanaa muda hautoshi ukimchukia huyu mama una laana unatakiwa kutubu usamehewe.
 
Kwa akili zako chawa hapo unaona kuna jipya gani lakujitapa?
 
Kwa sababu huna akili huwezi kuona linalofanyika. Nakuongezea tena kuna miradi ya maji , umeme kupitia REA inaendelea kufikia mwisho wa mwaka huu vijiji vyote vitakuwa na umeme na tunaanza kuwasha kwenye vitongoji hii yote ni miaka miwili ya Samia Suluhu utamkubali tuu na chuki zako.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amewasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo ataongoza maadhimisho siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya itakayofanyika kitaifa mkoani humo tarahe Juni 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda.

Rais Samia amezungumza baada ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kumpokea katika eneo la Tengeru kuanza kuimba nyimbo zenye maneno "Samia Sema, Sema usiogope sema..."

Rais Samia aliwajibu akisema
"Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi (huku akiweka mkono wake masikioni) naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya”

Wanajamvi, Rais wa Nchi kasema sisi tuseme tu yeye anapiga kazi tu
---

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati aliposimama kuwasalimia wakazi wa Tengeru mkoani Arusha amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda. Rais Samia amesema:

"...Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya...”
---

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona vijana wa Kitanzania wakijenga uchumi imara pamoja na kujenga ustawi wa maisha yao na familia zao.

Ameyasema hayo leo Juni 24, 2023 jijini Arusha wakati alipowasili na kusalimiana na wananchi wa mkoa huo ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Juni 25, mwaka huu.

“Tunataka kuona vijana wa Kitanzania wakiwa wako ‘busy’ kuzalisha mali na kujenga ustawi wa maisha yao na kujijengea uchumi wenye hadhi, uchumi imara kwa wenyewe na familia zao,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufungua nchi na kukaribisha sekta binafsi ili zije zifanye kazi na Tanzania katika maeneo mbalimbali ili kuzalisha ajira kwa vijana na kujenga kesho yao iliyo njema.

Mbali na hayo, Rais Samia amesema Serikali yake haina maneno mengi bali inafanya kazi kwa vitendo na kuangalia wapi inakusudia kwenda ili kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Credit: Clouds Media
Ni maneno ya kujifariji, ni dhamana tu ya mda ndo kapewa , ili jambo awe makini nalo sio dogo kama afikiliavyo
 
Unaongeza elfu 20 alafu gharama za maisha zinapanda kwa 200% alafu unapiga makofi?

Huo ni upumbavu na kichaa
Wameongezewa kama 70,000 hao wafanyakazi wa Chini, mungu wako alikaa miaka 6 sukari na vitu kibao vilipanda bei maradufu hakuongeza hata sh 10.

Pia Hakuajiri mama wa Watu juzi tu kaajiri 20,000 kada ya Elimu na Afya. Toka aingie madarakani kaajiri watu wengi tu.

Mnyonge mnyongeni haki yake Mpeni.
 
Huyo msaliti hayupo kwa ajili ya kuwaongoza watanganyika, yupo hapo kwa ajili ya kuwanufaisha ndugu zake waarabu, hata azibe masikio na jiwe, bado kelele zitapigwa tu, hawezi kusema serikali yake ni ya vitendo, huku vitendo vyenyewe vya kumkandamiza mtanganyika na kumnufaisha mwarabu.
Nyie endeleeni kupiga kelele mkija kuamka wenzenu matajiri halafu mnaanza kulilia umasikini.

Wakati mama anapiga Trip za Congo na Zambia mkawa mnamuita Majina kibao, wenzenu wanapiga fursa Nyie mnashinda Jf keyboard warriors, mnasubiria mtu aje na Briefcase ya Hela aje akutumbukizie chumbani.

Sasa Hivi Dp world wenye Akili Tayari wanaanza kuangalia watanufaika vipi, miaka 10 ijayo washaangalia we endelea tu kupiga mayowe hapa.
 
Wameongezewa kama 70,000 hao wafanyakazi wa Chini, mungu wako alikaa miaka 6 sukari na vitu kibao vilipanda bei maradufu hakuongeza hata sh 10.

Pia Hakuajiri mama wa Watu juzi tu kaajiri 20,000 kada ya Elimu na Afya. Toka aingie madarakani kaajiri watu wengi tu.

Mnyonge mnyongeni haki yake Mpeni.
Hiyo 70 umeongezwa pekeako?

Bora ujiite mama mwajuma tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom