Rais Samia: Serikali Yangu Sio ya Maneno ni ya Vitendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amewasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo ataongoza maadhimisho siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya itakayofanyika kitaifa mkoani humo tarahe Juni 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda.

Rais Samia amezungumza baada ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kumpokea katika eneo la Tengeru kuanza kuimba nyimbo zenye maneno "Samia Sema, Sema usiogope sema..."

Rais Samia aliwajibu akisema
"Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi (huku akiweka mkono wake masikioni) naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya”

Wanajamvi, Rais wa Nchi kasema sisi tuseme tu yeye anapiga kazi tu
---

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati aliposimama kuwasalimia wakazi wa Tengeru mkoani Arusha amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda. Rais Samia amesema:

"...Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya...”
---

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona vijana wa Kitanzania wakijenga uchumi imara pamoja na kujenga ustawi wa maisha yao na familia zao.

Ameyasema hayo leo Juni 24, 2023 jijini Arusha wakati alipowasili na kusalimiana na wananchi wa mkoa huo ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Juni 25, mwaka huu.

“Tunataka kuona vijana wa Kitanzania wakiwa wako ‘busy’ kuzalisha mali na kujenga ustawi wa maisha yao na kujijengea uchumi wenye hadhi, uchumi imara kwa wenyewe na familia zao,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufungua nchi na kukaribisha sekta binafsi ili zije zifanye kazi na Tanzania katika maeneo mbalimbali ili kuzalisha ajira kwa vijana na kujenga kesho yao iliyo njema.

Mbali na hayo, Rais Samia amesema Serikali yake haina maneno mengi bali inafanya kazi kwa vitendo na kuangalia wapi inakusudia kwenda ili kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Credit: Clouds Media
Arrogance of power
 
DP wakitaka kutukonga watuondolee Kodi komozi kwenye ushuru wa kuingiza magari nchini
 
Matokeo ya darasani ya huyu bibi tokea O-level kwenda mbele nani anajua atuwekee hapa?
🤣🤣Ya nini Sasa?kwani anaomba ajira zinazohitaj gpa na one za form four? mwenzio ndo mtoa ajira namba moja Sasa🤔haijalishi yeye alitaga🤣🤣🤣
 
View attachment 2667579

Kama ana hata chembe ya aibu , basi ajiuzulu haraka.., na hatuachi hadi ajiuzulu au wajitoe kwa lazima kwenye huo mkataba usio na kikomo, hata tukipelekwa mahakamani, potelea mbali.
Tulia wewe.
JamiiForums-633051173.jpg
 
Atuuze mara ngapi? Mkataba unasema DP world akitaka sehemuyeyote ya ‘Territory’ ya Tanganyika, seriakli inatakiwa iwaondoe watu katika eneo hilo kwa gharama zetu wenyewe, na akapewe DP world bila kulioa chochote, apewe bure! Sas auuzwe mara ngapi? Na hii haina kikomo, hata Yesu akirudi..

Sasa sijui anafanya nini madarakani hadi muda huu

View attachment 2667601
Hahahaa!.
JamiiForums-633051173.jpg
 
DP wakitaka kutukonga watuondolee Kodi komozi kwenye ushuru wa kuingiza magari nchini
Hii kitu unairudia rudia sana, Dp world anahusika vipi na Kodi za TRA?

Kldi ya magari ni TRA, dp world hahusiki kabisa huko. Ushuru wa bandari ni kiasi kidogo Wala sio sababu ya magari kuwa bei vile.

Kwa kukueleza tu mwaka huu Leo hapa inasomwa bajeti, serikali imeongeza tena Kodi ya magari. Hivyo tarajia bei kupanda zaidi
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amewasili mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo ataongoza maadhimisho siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya itakayofanyika kitaifa mkoani humo tarahe Juni 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda.

Rais Samia amezungumza baada ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kumpokea katika eneo la Tengeru kuanza kuimba nyimbo zenye maneno "Samia Sema, Sema usiogope sema..."

Rais Samia aliwajibu akisema
"Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi (huku akiweka mkono wake masikioni) naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya”

Wanajamvi, Rais wa Nchi kasema sisi tuseme tu yeye anapiga kazi tu
---

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati aliposimama kuwasalimia wakazi wa Tengeru mkoani Arusha amesema yeye hana maneno mengi bali ana vitendo zaidi huku akiangalia wapi anakwenda. Rais Samia amesema:

"...Nimeshasema wanangu, mimi sina maneno mengi, mimi vitendo tu ndio vingi. Wakisema mimi ninafanya masikio hivi naangalia wapi ninakwenda, kwa hiyo waseme sisi tunafanya...”
---

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona vijana wa Kitanzania wakijenga uchumi imara pamoja na kujenga ustawi wa maisha yao na familia zao.

Ameyasema hayo leo Juni 24, 2023 jijini Arusha wakati alipowasili na kusalimiana na wananchi wa mkoa huo ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Juni 25, mwaka huu.

“Tunataka kuona vijana wa Kitanzania wakiwa wako ‘busy’ kuzalisha mali na kujenga ustawi wa maisha yao na kujijengea uchumi wenye hadhi, uchumi imara kwa wenyewe na familia zao,” amesema Rais Samia Suluhu.

Aidha, amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufungua nchi na kukaribisha sekta binafsi ili zije zifanye kazi na Tanzania katika maeneo mbalimbali ili kuzalisha ajira kwa vijana na kujenga kesho yao iliyo njema.

Mbali na hayo, Rais Samia amesema Serikali yake haina maneno mengi bali inafanya kazi kwa vitendo na kuangalia wapi inakusudia kwenda ili kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Credit: Clouds Media
Ndiyo ni ya vitendo vya ujambazi wa raslimali zetu kimyakimya. Tumewashitukia
 
Hii kitu unairudia rudia sana, Dp world anahusika vipi na Kodi za TRA?

Kldi ya magari ni TRA, dp world hahusiki kabisa huko. Ushuru wa bandari ni kiasi kidogo Wala sio sababu ya magari kuwa bei vile.

Kwa kukueleza tu mwaka huu Leo hapa inasomwa bajeti, serikali imeongeza tena Kodi ya magari. Hivyo tarajia bei kupanda zaidi
IST gari ya masikini itauzwa milion 20 mtaishia kuuziana used hadi mkome
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom