Rais Samia: Sekta binafsi ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi yetu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,827
12,009
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua na kushiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) katika Ukumbi wa Kikwete - Ikulu Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni, 2023.



Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kama mnavyofahamu mkutano huu ni mwendelezo wa jitihada za pamoja kati ya Serikali na Sekta binafsi, Serikali imeendelea kufanya majadiliano na sekta binafsi katika kuleta maendeleo kwenye sekta binafsi.

Ni miaka 22 tangu kuanzishwa kwa baraza hili na maanikio makubwa yamepatikana tangu kuanzishwa kwa baraza hili ni matumaini yangu kuwa baraza hili litakuwa moja ya vyombo rasmi ya kuishauri Serikali kwenye mambo ya kukuza biashara ili kujenga uchumi.

Mashauri haya yawe pia njia ya kuimarisha sekta binafsi nchini ili kuzalisha na kuongeza thamani na tupunguze kuagiza bidhaa nje na tukute kupeleka bidhaa zetu nje Hatua hii itaiwezesha nchi yetu kupunguza matumizi ya fedha za kigeni, kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa. Pato la taifa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka jana liliongeza, matokeo hayo ni maboresho ya mazingira ya biashara, ongezeko la uboreshaji wa sheria na kukuza biashara hapa nchini.

Juhudi hizi hazitaishia kwenye ngazi ya Taifa peke yake bali zitaendelea katika ngazi za mikoa wilaya nk, na ndio maana hapa kuna wakuu wa mikoa nimewaleta hapa muone yanavyofanyika kwenye ngazi ya taifa ili nanyi mkafanye huko kwenye ngazi zenu, Nawaagiza viongozi ngazi zoote muendelee kuweka mabaraza haya huko kwenye na kuweka ripoti ya majadiliano haya kila robo mwaka na katika taifa hizo tutakuja kuibua wanaofanya vizuri na tutawazawadia muende mkashindane huko, na mtultee taarifa tutafatilia na kuona nani kakuza uchumi na tutamzawadia.

Niwapongeze Zanzibar katika uchumi wao buluu, na sisi Tanzania bara hatujachelewa katika kukuza uchumi kupitia uchumi wa buluu, Zanzibar wana soko kubwa na hawezi kulimaliza ivyo sisi nasi tushirikiane na Zanzibar kuchakata mazeo ya uchumi wa buluu na tuweze kuuza na kukuza uchumi wetu kwani tuna coastlinendefu twende tukawashawishi vijana waingie kwenye uzalishaji wa mazao ya maji.

Serikali kuanzia mwaka jana imeweka bajeti kubwa kwenye kilimo ili kuwashawishi vijana waweze kuingia kwenye kilimo, niombe sana ushirikiano na private sekta katika kuwafanya vijana waingie kwenye sekta hii, hatua kadhaa tumechukua hatua kadhaa kama kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo, kuzalisha mbegu bora, matumizi sahihi ya teknolojia, kuimarisha usalama wa chakula nchini, na hili tumelidhamiria kwa sababu uchache wa fedha za kigeni unaondelea sasa hivi duniani sis Tanzania tunaweza kupata haraka kwa kulima na kuuza mazao ya chakula.

Serikali hatufanyi biashara ila sekta binafsi wanafanya biashara, na wajibu yetu serikali ni kuweka mazingira bora ya biashara ili uchumi wetu uweze kukua zaidi na kufanya ivyo tunatanua wigo wa kodi kwa serikali, kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini

lakini kwenye kukuza sekta binafsi ili twende sawa inabidi mifumo yote ya serikali isomane, taarifa zioane tatizo mifumo yetu nchini haisomani, na sasa tutahakikisha mifumo yetu nchini inasomana na inakuwa na vigezo vya kimataifa na kubeba taarifa zetu hizo zote ili kila kitu kinachotokea bandarini nakisoma mimi rais ikulu na hii ni ndani ya miezi 6.

Nawataka Wawekezaji wa Sekta binafsi kujenga Hoteli nyingi kwakuwa kuna Wageni wengi wanakuja kutalii Tanzania na hawatakiwi wakose pa kulala. Mafanikio makubwa tumeyapata kupitia Royal Tour lakini Kuna changamoto kwamba Wageni wanaokuja mwakani na mwaka unaofuata watakosa mahali pa kulala kama tusipochangamka kujenga Mahotel sasa hivi kwahiyo Sekta binafsi hiyo ni fursa muhimu

Niombe upande wa Serikali tupunguze michakato kwenye kutoa vibali vya ujenzi wa Mahoteli sijui mara NEMC hajatoa ruhusa sijui nani kazuia nini!?, tuharakisheni kwasababu Watu watakaokuja mwakani na mwaka utakaofuata hawana pa kulala

Kubwa zaidi kwenye Sekta yenyewe kufanya marekebisho, takwimu zinaonesha Wageni waliokuja mwaka jana ni 30% tu wamerudi mwaka huu hii, means Watu wanakuja wanasema Tanzanja hatuji tena pamoja na vivutio tulivyonavyo, tukaliangalie hilo ili wakija warudi na washawishi wengine kuja

Kwa upande wa booking za Wageni takwimu zinaonesha Wageni wengi sana, hofu yetu mahali pa kulala
 
Back
Top Bottom