Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,830
Rais Samia Suluhu leo Juni 09, 2023 amesema sekta binafsi ndiyo itakayoitoa Tanzania kiuchumi, ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC).
Rais Samia amesema wajibu wa Serikali ni kutengeza mazingira bora ya kufanya biashara jambo ambalo pia litatanua wigo wa kukusanya kodi.
“Sekta binafsi ndio itakayotutoa kiuchumi, Serikali hatufanyi biashara lakini Sekta binafsi inafanya biashara, wajibu wetu kama Serikali ni kutengeneza mazingira bora ambayo yataleta chachu katika ufanyaji biashara na uwekezaji ili uchumi wetu ukue zaidi”
“Lakini tunavyofanya hivyo tunatanua msingi wa kukusanya kodi kwa upande wa Serikali kwahiyo tukazifanyie kazi kero zote ili tusukume utendaji mzuri wa biashara na uwekezaji nchini”
Alisema Rais Samia