Rais Samia, safari za nje ziambatane na hotuba zenye mvuto. Hongera Mama wa Barbados, umetikisa kikao

Yote ni saw a kabisa. Lakini kwa kuongezea tu ni;

1. Waelewe lengo la ziara ni nini. Kama Rais anahudhuria mkutano au kongamano, at the first place wahusika watambue linahusu nini ili wamwandalie hotuba inayobeba maudhui ya kusanyiko hili...

Mf. Ukisikiliza hotuba hii ya Rais wetu, kuna eneo kataja Mlima Kilimanjaro lakini binafsi nimeshindwa kuelewa alitaka hadhira ipate picha gani kuhusu Mount Kilimanjaro in relationship to the global climate changes...

2. Ma Rais wetu waachane na hotuba za mfumo "full text" za kusoma mwanzo mwisho NENO KWA NENO, SENTENSI KWA SENTENSI na AYA KWA AYA. Zimepitwa na wakati na zinadumaza akili..

Badala yake awe na hotuba iliyo katika mtindo wa "mifupa" au "skeleton" na nyama unajaza mwenyewe in the process...

Huu ndiyo mtindo Wa hotuba za Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwl J. K. Nyerere...

å Aidha mtindo huu wa hotuba ndio unaovutia na kuvuta attention ya hadhira/watazamaji na ni kipimo cha uelewa na ufahamu wa mhutubiaji....

Ni mtindo unaotumiwa/uliotumiwa na watu wa aina ya Tundu Lissu, Mwl. J. K. Nyerere, Nelson Mandela, Martin Luther Jr, Rais wa sasa wa Zambia Hakainde Hichilema nk. Ni mtindo wa hotuba zenye kuvuta hisia na kuhamasisha watu kutenda na kushiriki....

å Aidha, ni kwa sbb ni mtindo unaohitaji watu wenye exposure na uelewa mpana wa past and prevailing current global issues na wanaojisumbua kutafuta maarifa na kujisomea kwa wingi kila wakati...

Nasikitika kusema hili kwa ndugu zangu wa CCM ya leo, kuwa mimi sioni mtu wa kariba hii huko...

Na sababu ni moja tu, wamechoka, wamebweteka, wanadhani wameshafika Kanaani, hawana cha kuwasumbua, akili zao zimelala usingizi wa pono na walishalewa madaraka...

Kilicho mbele yao kwa sasa ni kula na kunywa kujaza Marumbo yao hadi kusaza, baaaasi..

Hiki ndicho kinachomsumbua Rais wetu huyu Samia S. Hassan...

Kuna kila dalili kuwa, amekwenda Scotland kupiga "misele" tu na kutalii. Anadhani kila wakati ni Wa kufanya ROYOL TOUR tu...!!​
Mkuu umemaliza kila kitu, aina ya uhutubiaji wa watu uliotaja kama Nyerere nk. unahitaji uwe na wide knowledge na uwe ni mtu ambaye ni conversational ambayo itaonekana kwenye demeanor yako namna unavyo interact na audience, jinsi unavyotumia gestures na jinsi unavyobadili tone ya sauti kuashiria emotion mbalimbali. Kwa sababu hangaya hayuko conversant na kiingereza ni vigumu kuhutubia kwa ule mtindo wa PM wa barbados hata kama atakuwa ana uelewa mkubwa kwenye hilo eneo, hivyo ataishia ku concentrate kwenye kusoma kilichoandikwa ili angalau awe na confidence ya kuwasilisha hicho ambacho anataka hadhira isikie.....so public speaking ni kipaji na pia ni taaluma inayofundishwa, tusiichukulie poa wakati tunafundisha vijana mashuleni............​
 
Kwa mtu kama Rais ana mtu wa kumsaidia kila eneo mpaka wa kwenda chooni a.k.a msalani...

Sijui kwanini wataalamu wa mambo haya wasimfundishe...

Labda ni jeuri au hafundishiki. Hatujui..
 
Suala la hotuba zisizo na mvuto limekuwa ni tatizo sugu kwa awamu zote nne zilizopita na sasa hii ya tano zimeendelea kusikika, nimeondoa awamu ya Nyerere.

Wakati wa Magufuli hazikujitokeza kabisa kwa kuwa hakusafiri nje ya nchi. Rais Samia ameingia na tabia ya kusafiri nje kwa kujitangaza, kuifungua nchi. Tatizo ni ubora duni wa hotuba zake.

Hatukuhitaji hotuba ya kueleza madhara ya Climate change. Hii ni mikutano ya kuwaambia waharibifu kubeba mzigo. FINITO! COP ni tofauti na jukwaa la Dodoma unaposhangiliwa kwa kila sentensi unayozungumza.

Huyu ndo Samia wa TZ

Huyu ni Mia wa Barbados
Mkuu Zygot, hayo masuala alikuwa akiyaweza Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hawa ndio walikuwa na uwezo wa ku_deliver speech zenye mvuto na kwa lugha ya kiingereza chenye vocabularies za kutosha.

Hawa wengine waliobaki inabidi twende nao hivyo hivyo, hakuna namna.
 
Kwa mtu kama Rais ana mtu wa kumsaidia kila eneo mpaka wa kwenda chooni a.k.a msalani...

Sijui kwanini wataalamu wa mambo haya wasimfundishe...

Labda ni jeuri au hafundishiki. Hatujui..
Kama huna kipaji hicho, kufundishwa ni kuanzia shule ya msingi..........ndo yale mambo ya debate kule sekondari, sijui kama bado zipo.....kwenye nchi ambayo matumizi ya lugha ya kiswahili yako prominent, kuwa conversant na lugha ambayo unatumia tu shuleni kusomea na ukaongea kwa kujiamini ni mtihani......hii labda wanaweza watu kama kina Idd Amin, anaongea kiingereza kibovu kweli kweli na bado anajiamini.......​
 
Rais siyo mtaalamu wa kila kitu, ukiona hotuba haijakaa sawa wataalamu waliobobea kwenye hilo eneo hawajawa consulted kutoa mitazamo yao au chambuzi zao kuhusu hilo eneo kabla ya kuandaa hotuba......
Tatizo ni kuwa kwa katiba yetu kiongozi wetu kila kitu ni yeye. Washauri wooote anateua yeye kwa mapenzi yake. Sasa akiteua maimuna, nani alaumiwe?
 
Viongozi hawafanani na kuna njia nyingi za kutoa ujumbe. Mara nyingi mtu anayeongea kwa lugha ya upambanaji " combative style" na akawa na data za kufikirisha anafurahisha kumsikiliza. Tunampongeza Rais wetu kwa kuthubutu bila kujali kama maono yake yatapokewa vipi. Nchi zetu zipo njia panda - mataifa yaliyoendelea yanataka kuacha matumizi ya petroli mwaka 2050 sisi tuko kwenye harakati za kujenga bomba la mafuta, kuchimba mkaa wa mawe, wananchi bado wanakata miti kwa ajili ya nishati ya mkaa - sasa ukienda kwenye jukwa la kupunguza uharibifu wa mazingira , utasema nini?
Mama aliongea vizuri sana...
"We know what is required... The time to act is now..."
Watu wanatofautiana...
Big up #SSH
Tusimpambe bila sababu. Hotuba alibowa!!
Mtoa hotuba mzuri ni yule anayefahamu aina ya wasikilizaji wake. Anayefahamu lengo na dhumuni la mkusanyiko. Hotuba ya rais wetu haijulikani ililenga nini. Hata kama utaandikiwa, mtoa hotuba mzuri lazima ana namna ya kuwavuta wasikilizaji. Kumbuka hotuba za Mugabe na Chavez kule UN.

Kikwete alianza tabia ya hotuba za kitaifa kila mwezi. Hotuba zikabowa kwa kutokuwa na mvuto. Tukaelezwa mwandishi ni Januari. Januari aliishia kuandikia mapitio ya matukio kila mwezi na kuyaita ni hotuba kwa wananchi kila mwezi.
 
Lugha lugha hii ya kigeni tujifunze, ukiwa na vocabulary chache sana inakuwa ngumu kucheza na lugha ya kigeni ukaleta mvuto wa kusikilizwa.
Huyu mama wa Barbados alijua anakuja kufanya nini. Anazo takwimu kichwani, ana gesture za kuvutia badala ya kuinamia karatasi kwenye podium. Unaona wazi akina Boris wakiitikia kwa kichwa anayosema. Hakika, wimbo siyo maneno, ni melody. Sijui ni elimu yake maana naona sanayo shule ya uchumi na sheria. Sisi wetu je?
 
Oooh yes exactly!

Kwanza huwezi kumlinganisha mama yetu SSH na Waziri Mkuu wa Barbados anaeongoza kainchi kenye jumla ya watu 287,000.😆😆😆
Yaani ni kama watu waliopo pale Mawasiliano wakisubiri daladala...
 
Oooh yes exactly!

Kwanza huwezi kumlinganisha mama yetu SSH na Waziri Mkuu wa Barbados anaeongoza kainchi kenye jumla ya watu 287,000.😆😆😆
UNanikumbusha tunavyofungwa magori na timu za Rwanda na Burundi. Bora uwe na nchi ya watu laki moja wenye IQ kubwa kuliko kujivunia kuongoza milioni 50 na kupata miongoni mwao rais mwenye IQ ndogo.
 
Acheni ujinga mnampangia cha kuongea kama nani, enzi zile hazirudi tena kwenu jifunzeni historia. Rais SSH wa viwango vya juu piga kazi. Kazi iendelee
Nasubili siku moja aweze kuhutubia baraza la idd!
 
Suala la hotuba zisizo na mvuto limekuwa ni tatizo sugu kwa awamu zote nne zilizopita na sasa hii ya tano zimeendelea kusikika, nimeondoa awamu ya Nyerere.

Wakati wa Magufuli hazikujitokeza kabisa kwa kuwa hakusafiri nje ya nchi. Rais Samia ameingia na tabia ya kusafiri nje kwa kujitangaza, kuifungua nchi. Tatizo ni ubora duni wa hotuba zake.

Hatukuhitaji hotuba ya kueleza madhara ya Climate change. Hii ni mikutano ya kuwaambia waharibifu kubeba mzigo. FINITO! COP ni tofauti na jukwaa la Dodoma unaposhangiliwa kwa kila sentensi unayozungumza.

Huyu ndo Samia wa TZ

Huyu ni Mia wa Barbados

Huyu waziri mkuu wa Barbados alikuwa ni mmoja wa "Keynote Speakers" ( kuelezea ubobezi wake, matatizo na matarajio ya mkutano) - alikuwa amepewa jukumu hilo, kwahiyo siyo sawa kulinganisha hotuba yake na Marais wengine.
 
you are just biased for no reasonable reason. Hata awe keynote speaker au mtoa hotuba, Barbados lady is just an elephant to our president. President wetu hana huo uwezo, hana huo mpangilio wa hoja na hata speech gestures. Kwa mengine, just read my signature below.
 
Hapo ndio uwezo wa mama yetu unaishia. Ni vema umeweka hotuba ya huyo kiongozi wa barbado kulinganisha. Mama yetu jukumu lake atuvushe hadi 2025 tuweze pata magufuli mpya. Mambo mengi ya kimataifa including ubeberu mama hana uelewa. Tumsadie kuhakikisha watu wema na weledi wanamzunguka maana fisadi wasije mshika.
Mwambieni abaki huko Egypt, she is useless anajua kusafiri sana. Hizo safari tunalipa sisi wewe Samia . Kula nchi. Problem ya kuwa na un educated President aliye ndani ya polygamy.
 
UNanikumbusha tunavyofungwa magori na timu za Rwanda na Burundi. Bora uwe na nchi ya watu laki moja wenye IQ kubwa kuliko kujivunia kuongoza milioni 50 na kupata miongoni mwao rais mwenye IQ ndogo.
Sio kwamba IQ yake yake itaendana na idadi ya watu unaowaongoza??, the more the population #, the more the IQ and vise versa😆😆😆😆😆😆 up to infinite!!
 
Back
Top Bottom