Rais Samia, safari za nje ziambatane na hotuba zenye mvuto. Hongera Mama wa Barbados, umetikisa kikao

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,047
2,000
Suala la hotuba zisizo na mvuto limekuwa ni tatizo sugu kwa awamu zote nne zilizopita na sasa hii ya tano zimeendelea kusikika, nimeondoa awamu ya Nyerere.

Wakati wa Magufuli hazikujitokeza kabisa kwa kuwa hakusafiri nje ya nchi. Rais Samia ameingia na tabia ya kusafiri nje kwa kujitangaza, kuifungua nchi. Tatizo ni ubora duni wa hotuba zake.

Hatukuhitaji hotuba ya kueleza madhara ya Climate change. Hii ni mikutano ya kuwaambia waharibifu kubeba mzigo. FINITO! COP ni tofauti na jukwaa la Dodoma unaposhangiliwa kwa kila sentensi unayozungumza.

Huyu ndo Samia wa TZ
Huyu ni Mia wa Barbados

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
8,302
2,000
Hapo ndio uwezo wa mama yetu unaishia. Ni vema umeweka hotuba ya huyo kiongozi wa barbado kulinganisha. Mama yetu jukumu lake atuvushe hadi 2025 tuweze pata magufuli mpya. Mambo mengi ya kimataifa including ubeberu mama hana uelewa. Tumsadie kuhakikisha watu wema na weledi wanamzunguka maana fisadi wasije mshika.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,837
2,000
Wacha tubembeleze wahisani bajeti yetu isije kukwama tena utekelezaji wake, hakuna masikini jeuri hapa duniani ni uongo tu.
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,550
2,000
Kuna utofauti kati ya hotuba ya kuandikiwa na ya kujiandalia
Rais siyo mtaalamu wa kila kitu, ukiona hotuba haijakaa sawa wataalamu waliobobea kwenye hilo eneo hawajawa consulted kutoa mitazamo yao au chambuzi zao kuhusu hilo eneo kabla ya kuandaa hotuba......
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,603
2,000
Lugha lugha hii ya kigeni tujifunze, ukiwa na vocabulary chache sana inakuwa ngumu kucheza na lugha ya kigeni ukaleta mvuto wa kusikilizwa.

..mimi nadhani kwenye hotuba hutakiwi kutumia misamiati migumu-gumu.

..ukiwasikiliza maraisi kama Obama au Biden hotuba zau huwa zina misamiati ya kawaida ambayo inaeleweka hata na mtu mwenye elimu ya kawaida.

..Maza hakujiandaa kwa hii kazi na ndio maana anaonekana anapwaya.
 
kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,341
2,000
Dahhh...kweli hakujiaandaa na hata walioandaa hutuba hafahamu wajumbe wa mkutano wanataka nini unapotakiwa kutoa huduma. Pale nafikiri ilikuwa nikutoa mawazo yakitaalamu ya nini cha kufanya. Samia kaeleza madhara ya climate change, nani asiyeyafahumu? Hutuba nyepesi, haina mvuto wa kisayansi na kisiasa, kikubwa kajishusha ilikuomba misaada.
 
NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,979
2,000
Mama ana kazi sana, wakishashindwa yooote watamlinganisha hadi kimo na viongozi wengine ili muradi tu wapate cha kusema na kuponda!
 
Jorojik

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
3,909
2,000
Hapo ndio uwezo wa mama yetu unaishia. Ni vema umeweka hotuba ya huyo kiongozi wa barbado kulinganisha. Mama yetu jukumu lake atuvushe hadi 2025 tuweze pata magufuli mpya. Mambo mengi ya kimataifa including ubeberu mama hana uelewa. Tumsadie kuhakikisha watu wema na weledi wanamzunguka maana fisadi wasije mshika.
Watu wenye kaliba ya magufuli wangesubutu kwenda kwenye majukwaa makubwa kama haya? Hii ni annual meeting ya Mataifa duniani kukutana kila mwaka kujadili agenda ya global climate change. Ulishahi kusikia agenda hii ikigusiwa ktk utawala Wa awamu ya tano? Kwanini? Kwa sababu hawakuwa washiriki licha ya wachangaji!
 
Xaph87

Member
Sep 26, 2020
67
150
Bi mkubwa mmoja alikuwa anaflow na kumudu/engage audience (public speaking katika ubora wake).
Bi mkubwa mwingine alikuwa anasoma tu.
 
PETER THE ROCK

Senior Member
Feb 17, 2014
158
250
Suala la hotuba zisizo na mvuto limekuwa ni tatizo sugu kwa awamu zote nne zilizopita na sasa hii ya tano zimeendelea kusikika, nimeondoa awamu ya Nyerere.

Wakati wa Magufuli hazikujitokeza kabisa kwa kuwa hakusafiri nje ya nchi. Rais Samia ameingia na tabia ya kusafiri nje kwa kujitangaza, kuifungua
Kwa kawaida Rais anapozungumzia masuala yanayohusu jumuiya ya kimataifa anakuwa anazungumza kwa niaba ya sisi Watanzania kwa maana kuwa anaueleza Ulimwengu Tanzania inasema nini katika agenda inayojadiliwa. Ushauri wangu wa dhati kabisa ni kila mikutano hii mikubwa ambayo Rais wetu anategemewa kuzungumza kwa niaba yetu wote basi atumie hazina ya vipaji vyote vya Watanzania kuhusu somo hilo.

Draft ya kwanza (zero draft) itokane na jopo la wataalam wa somo husika. (Ni jukumu mojawapo la Idara ya Utumishi kuwa na data bank ya wataalam mbali mbali waliobobea na wenye uzoefu wa taaluma mbali mbali).Wasaidizi wapendwa wa Rais na Rais mwenyewe watumie hiyo draft ya kwanza kuifinyanga hutoba kwa kuqeka lugha rafiki kwa msomaji, Rais wetu kama anavyotaka lakini substance ya jambo analoongelea itokane na wataalam wa kiwango cha juu kabisa.

Uzoefu wa kawaida unaonesha hakuna mtaalam mwenye hekima ya wastani ambaye hawezi kuwa radhi kusaidia Rais wake afanye vizuri kwenye masuala ya heri kama haya. Tusitengeneze, kwa mfano, timu ya mpira ya taifa inayokwenda kwenye mashindano ya world cup inayotokana na ligi ya mpira kutoka daraja la tatu! Watanzania lazima tukubali kuwa kutumia uwezo na vipaji vyote tulivyonavyo ndiyo siri ya hao viongozi wenzetu ambao tunaona wanafanya vizuri!
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
11,815
2,000
Suala la hotuba zisizo na mvuto limekuwa ni tatizo sugu kwa awamu zote nne zilizopita na sasa hii ya tano zimeendelea kusikika, nimeondoa awamu ya Nyerere.

Wakati wa Magufuli hazikujitokeza kabisa kwa kuwa hakusafiri nje ya nchi. Rais Samia ameingia na tabia ya kusafiri nje kwa kujitangaza, kuifungua nchi.
Huyu ndiyo rais sasa. Lkn huyu wa kwetu ni chifu
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
11,815
2,000
Suala la hotuba zisizo na mvuto limekuwa ni tatizo sugu kwa awamu zote nne zilizopita na sasa hii ya tano zimeendelea kusikika, nimeondoa awamu ya Nyerere.
Huyu ndiyo rais sasa. Lkn huyu wa kwetu ni chifu.

Hakika tumepigwa.
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
5,141
2,000
Suala la hotuba zisizo na mvuto limekuwa ni tatizo sugu kwa awamu zote nne zilizopita na sasa hii ya tano zimeendelea kusikika, nimeondoa awamu ya Nyerere.
Mama aliongea vizuri sana...
"We know what is required... The time to act is now..."
Watu wanatofautiana...
Big up #SSH
 
Claude Henry

Member
May 25, 2017
80
125
Kuna utofauti kati ya hotuba ya kuandikiwa na ya kujiandalia
Viongozi hawafanani na kuna njia nyingi za kutoa ujumbe. Mara nyingi mtu anayeongea kwa lugha ya upambanaji " combative style" na akawa na data za kufikirisha anafurahisha kumsikiliza. Tunampongeza Rais wetu kwa kuthubutu bila kujali kama maono yake yatapokewa vipi. Nchi zetu zipo njia panda - mataifa yaliyoendelea yanataka kuacha matumizi ya petroli mwaka 2050 sisi tuko kwenye harakati za kujenga bomba la mafuta, kuchimba mkaa wa mawe, wananchi bado wanakata miti kwa ajili ya nishati ya mkaa - sasa ukienda kwenye jukwa la kupunguza uharibifu wa mazingira , utasema nini?
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
5,141
2,000
Watu wenye kaliba ya magufuli wangesubutu kwenda kwenye majukwaa makubwa kama haya? Hii ni annual meeting ya Mataifa duniani kukutana kila mwaka kujadili agenda ya global climate change. Ulishahi kusikia agenda hii ikigusiwa ktk utawala Wa awamu ya tano? Kwanini? Kwa sababu hawakuwa washiriki licha ya wachangaji!
Bora Mama katufikisha hapo... Tuliko toka ni kubaya zaidi!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom