Rais Samia Ondoa hiki kikokotoo kinawaumiza wastaafu

Ni kweli kabisa kanuni hii mpya ya kikokotoo itailetea serikali hasara badala ya faida kwani itachochea vitengo vya wizi wa fedha za umma kwani watumishi wataona hakuna mustakabali mzuri baada ya kuhitimisha utumishi wao hasa kama mtu hajajenga nyumba
 
Inategeme

Inategemea anafanya kazi na ana majukumu gani ya kifamilia. Hivi unajua kima Cha chini Cha mfanyajazi wa umma ni sh. Ngapi. We acha tu. Wafanyakazi kazi wanayo.
Anafikiri kujenga ni rahisi kwa mfanyakazi wa kawaida, wale wanaoitwa waandamizi wenyewe kujenga ni kwa kudunduliza sana, hadi finishing kukamilika ni miaka 10........hawana hata uwezo wa kukopesheka kununua nyumba ya kawaida ya mil. 150, hao ndo unaambiwa waandamizi, sasa wale kima cha chini hali inakuwaje?​
 
Mheshimiwa Rais.

Nakuandikia waraka maalum juu ya hali ya mfanyakazi, hususan anayestaafu.

Nataka nikueleze kuwa, hiki kikotowo ulichokiweka hakina masilahi kwa mfanyakazi anayestaafu. Kiufupi ni dhuluma ya wazi.

Hali ya maisha imekuwa ngumu, gharama za maisha zinazidi kupanda. Kiufupi , hii 33% lumpsum unayotoa kupitia kikotowo, haitoshi, haikidhi, na ni dhulma kubwa mno kwa mfanyakazi.

Ndugu Rais, Jasho la mtu halipaswi kupangiwa masharti magumu. Haiwezekani Mfanyakazi afanye kazi miaka 30 au 35 kisha aje akutane na vijisent vya milioni 50 kama mafao ya kustaafu. Hivi ni vihela vidogo sana na siku hizi havitoshi hata kununua kiwanja na hapohapo kujenga nyumba ya vyumba vitatu.

Ndugu Rais, Hicho chama unachokiongoza kina alama ya jembe na nyundo. Nyundo ikiwakilisha wafanyakazi. Haiwezekani serikali unayoiongoza ikawa ni ya kuwagandamiza wafanyakazi.

Juzi hapa mbunge Heche kaeleza jinsi Wabunge wanavyopata lumpsum ya milioni 272 kwa kazi ya miaka Mitano. Wewe Rais hukatwi kodi katika mshahara wako na Ukistaafu unaendelea kupata 80% ya mshahara wa rais aliyeko madarakani na bado unaenda kupata mabenefit kibao ikiwemo kujengewa nyumba na Pensheni.

Rais hebu Muogope Mungu. Wafikirie watu wa chini. Kikokowa cha 33% ni dhulma kubwa, iondoe mara moja.

Wako katika ujenzi wa Taifa

Missile of the Nation
Wewe ni mjinga na haupo informed. Serikali ina lengo zuri sana la kuhakikisha wastaafu wanakuwa anagalu na kitu fulani cha kupokea kila mwezi. Hiyo 33% inatosha kabisa kikubwa ni kuwa na plan nzuri. Hivyo msimsubue Rais Samia na uzushi wenu.
 
Wewe ni mjinga na haupo informed. Serikali ina lengo zuri sana la kuhakikisha wastaafu wanakuwa anagalu na kitu fulani cha kupokea kila mwezi. Hiyo 33% inatosha kabisa kikubwa ni kuwa na plan nzuri. Hivyo msimsubue Rais Samia na uzushi wenu.
Watu wazima hawapangiwi pesa yao waitumieje.
Wape watu pesa yao, kuhusu wataitumiaje waachie wenyewe!
 
Na Sasa Benki, hasa TCB, hazifanyi Top up ya Mikopo ya Wastaafu mpaka umalize Deni walisema NSSF wametoa katazo Hilo!!!

Riba kwa Mikopo ni kubwa.

Mnatuua mapema.

Serikali tunaomba mrekebishe hili.
Bima inakatwa kwenye Mkopo, Riba ya tarakimu mbili, kwa nini mnatunyima Top up!!??
 
Hivi kimeanza kutumika? Wastaafu wa nchi hii wanachukuliwa kama zero brain.

Wale wanapata pensheni zao kupitia NMB hawaruhusiwi kutuma na kuchukua zaidi ya 1M kwa siku kupitia NMB Mobile au kwa wakala.

Hiki kituko kimeanza juzi kati.
 
Unadhani watu wote wanaweza kufanya biashara?hivi watu wangapi wanapoteza mafao yao sasa assume wapewe asilimia 100 halafu wapoteze ni bora hata kuwapa 50%, 50% itoke kama pensheni.
kwani mmeshawahi pokea malalamiko ya watu kumaliza hela zao mapema au mnawakadiria tu?
 
Nimeshituka kuona kuwa TUCTA imeridhia na kuwaambia wafanyakazi eti mjadala umefungwa! Pamoja na kuwa TUCTA ni tawi la CCM lakini wafanyakazi wanayo haki kujadili maslahi yao hata kama TUCTA na CCM hawatawasikiliza.
Naungana na tucta kikokotoo hakina shida , tatizo ni elimu tuu haijatolewa vizuri hivyo watu hawajui lolote
 
Naungana na tucta kikokotoo hakina shida , tatizo ni elimu tuu haijatolewa vizuri hivyo watu hawajui lolote
Hivyo Tucta haioni umuhimu wa wahusika kujua! Mfanyakazi anapofanya kazi kwa miaka 20 kisha unasema alipwe miaka 14 tu huo ni unyang'anyi, hata unielimishe vipi sitaelewa.
 
Back
Top Bottom