Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,111
Mheshimiwa Rais.
Nakuandikia waraka maalum juu ya hali ya mfanyakazi, hususan anayestaafu.
Nataka nikueleze kuwa, hiki kikotowo ulichokiweka hakina masilahi kwa mfanyakazi anayestaafu. Kiufupi ni dhuluma ya wazi.
Hali ya maisha imekuwa ngumu, gharama za maisha zinazidi kupanda. Kiufupi , hii 33% lumpsum unayotoa kupitia kikotowo, haitoshi, haikidhi, na ni dhulma kubwa mno kwa mfanyakazi.
Ndugu Rais, Jasho la mtu halipaswi kupangiwa masharti magumu. Haiwezekani Mfanyakazi afanye kazi miaka 30 au 35 kisha aje akutane na vijisent vya milioni 50 kama mafao ya kustaafu. Hivi ni vihela vidogo sana na siku hizi havitoshi hata kununua kiwanja na hapohapo kujenga nyumba ya vyumba vitatu.
Ndugu Rais, Hicho chama unachokiongoza kina alama ya jembe na nyundo. Nyundo ikiwakilisha wafanyakazi. Haiwezekani serikali unayoiongoza ikawa ni ya kuwagandamiza wafanyakazi.
Juzi hapa mbunge Heche kaeleza jinsi Wabunge wanavyopata lumpsum ya milioni 272 kwa kazi ya miaka Mitano. Wewe Rais hukatwi kodi katika mshahara wako na Ukistaafu unaendelea kupata 80% ya mshahara wa rais aliyeko madarakani na bado unaenda kupata mabenefit kibao ikiwemo kujengewa nyumba na Pensheni.
Rais hebu Muogope Mungu. Wafikirie watu wa chini. Kikokowa cha 33% ni dhulma kubwa, iondoe mara moja.
Wako katika ujenzi wa Taifa