Rais Samia, ni sawa kutaka tuanze upya lakini lazima tuwe na pa kuanzia

Kujua ni lipi la maana na lipi siyo la maana inahitaji angalao kiwango fulani cha chini cha ufahamu. Kama hujakifikia, unaweza kuona kila ambacho watu wanajadili hakina maana, ila wakiongelea ubwabwa, biriani, hapo utaona wameongea cha maana, kwa sababu hata aliyepungukiwa akili, angalao anajua lazima ale.
 
Rais Samia mara baada ya kuapishwa alisema, tuanze upya. Sentensi ile ilibeba maana nzito iliyofichika kwa wasiotaka kutafakari.

Unaanza upya pale ambapo unaamini ulikosea, na ili uanze upya ni lazima ufahamu ulipokuwa, ulipokosea na namna ulivyokosea, ili unapoanza upya usiingie kwenye makosa ya mwanzo. Lakini cha muhimu zaidi ni kwamba unajenga mifumo itakayozuia kabisa kuangukia kwenye makosa ya mwanzo.

Sote, tunafahamu utawala wa awamu ya 5 ulivyoleta madhira mengi kwa watu wengi. Na wengi wao hawatausahau utawala wa awamu ya 5 kwa mabaya. Na wengine hawana nafasi hata ya kuukumbuka maana hawapo katika Ulimwengu huu. Bila shaka hao wameyafikisha masikitiko yao kwa mkuu wa Mbingu/ahera na Ulimwengu.

Fikiria ndugu, wanafamilia, marafiki wa waliopotezwa au kuuawa:

Ben Saanane
Azory Gwanda
Kanguye
Yule diwani wa Dar
Yule diwani Kilosa
Akwilina

Wafikirie waliojeruhiwa na familia zao:

Tundu Lisu
Na wengine wengi ambao majina yao siyo makubwa

Wafikirie walioporwa pesa kupitia TRA na wasiojulikana.

Wafikirie waliowekwa ndani kwa kesi za kubambikiwa, n.k.

Wafikirie akina Mbowe, Halima Mdee, Msigwa, n.k. waliowekwa ndani kwa tuhuma za kutengenezwa za kumwua Akwilina, huku wote tukijua kuwa Akwilina aliuawa na Polisi.

Watu wamepoteza wapendwa wao, watu wamefanywa kuwa vilema, watu wamepoteza fedha zao walizozipata kwa taabu na mateso, watu wameteseka mahabusu kwa kesi za kutengenezwa, watu wamedhalilishwa kwa kuvuliwa nguo mpaka kupekuliwa kwenye njia za siri, watu wamewekwa mahabusu kwa kesi za kihayawani, watu wamepoteza ajira baada ya waajiri wengi kufunga makampuni yao kutokana na mazingira mabaya ya uwekezaji, n.k, hivi hawa unaweza tu kuwaambia kuwa TUANZE UPYA, na kweli tukaanza upya?

Yaani tuanze upya, tusahau yote, huku:
Waliomteka na kumpoteza Ben Saanane wakifahamika na kuranda mitaani,
Huku waliomchukua na kumpoteza Azory Gwanda mbele ya familia yake, wakiwa wanafahamika, na wanaranda mitaani,

Huku waliomwua Akwilina wakiwa wanafahamika wazi, na wanaendelea kukalia viti vya ofisi za umma,

Huku waliomfyatulia risasi Tundu Lisu wakiwa wanafahamika na wanarandarandaranda mitaani,

Huku waliowabambikizia watu kesi za uhujumu uchumi, wakibadilishiwa ofisi,

Huku waliowabambikizia watu kesi za madawa ya kulevya, wakiwa wanaranda mitaani,

Huku waliowadhulumu watu pesa zao halali kupitia madai ya uwongo ya uhujumu uchumi wakiwa wamejaa tele maofisini?

Wenzetu kule Afrika Kusini, walipoamua kuanza upya, waliunda Tume ya maridhiano iliyoongozwa na Askofu Desmond Tutu. Tume hii ilizungumza na waathirika wote, watenda maovu, watunga sheria na sera, na kisha kuweka kila kitu wazi ikiwa ni pamoja na watenda maovu waliokuwa hai, kuomba msamaha. Hiyo ilileta faraja ya moyo japo haikufuta machozi ya walioumizwa.

Kama hatutafanya hivyo, hakika hii kuamza upya itabakia kuwa midomoni lakini mioyo ya watu bado ni mizito dhidi ya watenda maovu wote, maana wengi wao wanafahamika.

Utawala wa Mama Samia una nafuu kubwa lakini hauwezi kuwa na utakatifu kwa sababu ndani yake wale wauaji wamo, wale watesaji wamo, waliokuwa wanabambikizia watu kesi bado wamo, waliokuwa wanawaweka mahabusu wanasiasa wa upinzani kwa uonevu bado wamo.

Hawa wasipoondolewa, wasipotubu, utawala wa Mama Samia bado utaendelea kutembea na laana ya utawala wa awamu ya 5.

Mama Samia tunakuomba uliunganishe Taifa. Kwanza tupate taarifa kamili za walioiawa na kupotezwa, tuomboleze na waliowapoteza wanafamilia wao, tuwaombe msamaha maana kama jamii tulishindwa kutetea uhai wa hawa Watanzania wenzetu. Lililo kubwa zaidi, kama Taifa turudi kwenye kutengeneza Katiba mpya na kubadilisha baadhi ya sheria, ili mfumo wetu usiruhusu kuwapata viongozi/watawala dhulumati katika ngazi yoyote ile kama ilivyotokea wakati wa awamu ya 5. Leo, kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa letu, DC anashtakiwa kwa kosa la kuwa kiongozi wa genge la majambazi! Laana kubwa hii.

Unapenda sana kudhani choo chako Ni tofauti. Kinanukia cake. Moja. Hao Akina Azory unajua kwa dhati kabisa pasipo Shaka wamepoteaje na nani kawapoteza na kwa sababu gani. Wamelifanyia Nini Taifa na mtu wa kawaida ili uzi wako Uwe na maana.

Mbili: je wewe Ni mmoja ya Wale waliokua wanashangilia vifo vya watanzania kule KiBITI tena kwa maneno ya kisiasa. Umetubu? Kwa nani. Je Mfano mtu kama wewe, ndo naye Azory alikuwa mitaaa hiyo Tutajuaje uhusika wenu katika mahuaji Yale ya kutisha. Au Wale wasomalia. Au nyani. Au kuku?

Tatu. Asilimia ngapi ya watu kama wewe wanaona JPM alikuwa unavyohisi. Wewe. Mana naowafahamu wengi na hawa wakati wa kifo chake wanaonyesha walimwelewa na kumpenda. Hata mimi nilimpenda Rais wetu. Na nampenda Pia Mama Samia. Sijui wewe unamwakilisha Nani. Watu kama nyie hamjui chochote ila mnaropoka kwa kuwa mna bundle.

Nne. Mama hana Pa kutubu wala haja hiyo. Kazi na iendelee. Wewe kaaa nusa tu kama cake kula. Nachojua. Yakifunuka tunayoyatenda. Sote tuna cha kujibu. Lakini kwa Sasa. Endelea kujifurahisha.

You are stupid. Grow up. Move forward. Jenga. Onyesha njia. Ziba ufa.
 
Hakuna asiyejua kuwa kifo kipo na ndiyo mwisho wa maisha ya kila mwanadamu aishiye hapa Duniani. Suala siyo kuishi au kufa, cha muhimu uliishi vipi ukiwa hai, uliwasaidiaje Dunia na Taifa lako kuwa mahali pema pa kuishi wanadamu wa leo na kesho? Ulikuja kuitengeneza au kuiharibu Dunia? Kama huwezi kuiboresha Dunia, kama huwezi kuchangia ustawi wa wanadamu na Dunia kwa ujumla, ni aheri usingelizaliwa.

Mwanadamu mwenye hekima, kwa muda mfupi aliopewa kuishi Duniani, hujenga kumbukumbu yake ya kukumbukwa kwa mema, na siyo kwa kuteka, kuua na kutesa wanadamu wenzake.

Pole km wewe utamkumbuka kwa mabaya sie tunamkumbuka kwa mazuri....na hayo mabaya unayosema sisi tunaona alikuwa analinda nyumba yake ambayo ni Tanzania..km baba sensitive anavyolinda familia..km walitokea watoto watukutu wakufikia ama mahalf cast waliochanganya damu, hawamsikii wanabishana nae tufanyeje sisi...they learned the hard way...

Ni busara kwa kweli hawa watoto watukutu ama wawakilishi wao wangejipanga kwenda Chato kwenye nyumba yake ya milele na maua kumuomba msamaha kwa kumkwaza mzee wetu alietupambania usiku na mchana..

Rest easy JPM we miss you!
 
Mada hii ni kubwa na ya kufikirisha kuliko huu utoto ulioandika hapa. Ni vyema shule zifunguliwe mapema urudi shule kuliko kuingiza utoto kwenye mada za wakubwa.
Kama mada hii ni kubwa basi dunia ina vioja!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom