Ujumbe kwa Rais Samia na CCM

joseph2

Senior Member
May 31, 2015
126
251
Habari za Leo wanajami forum wezangu. Ni matumaini yangu kuwa wote mnaendelea na mapambano yakujitafutia ugali wa kila siku

Kwenye nchi iliyo fanywa kuwa kisiwa cha wavumilivu. Leo naomba ni ongee na mwenyekiti wa ccm na wanachoma wake, kupitia kwenye hili jukwaa letu.

Bila kuwapotezea mda acha kwanza nianze na kuwaelezea hisia zangu juu ya kilicho tokea Jana, katika jiji letu la Dar es salaam.

Kusema kweli chadema wmeandika historia na wamepanda mbegu ya mbuyu ambao utastawi kwa Hali yoyote ile.

Wale watanzania waliozaniwa kwa mda mlefu kuwa ni waoga na wasio kuwa na uwezo wa kuchuja propaganda na ukweli, Jana wamejieleza kwa ufasaha zaidi, na bila shaka wemeeleweka kwa wote wenye akili timam.

Ila Kuna uwezekano kwa wale ambao walio kwisha kabidhi akili zao kwa wenye mamraka na pesa: hao hawawezi kuwaelewa kiulahisi.

Watu kama kina makonda hawawezi kuelewa kilicho tokea 24/1/2024.

Najuwa raisi amezungukwa na watu kama kina makonda ambao Hawana uwezo wa kufikiri bila kuweka masilahi binafusi mbele.

Mheshimiwa raisi Samia nakusihi Sana utafute siku ukae peke yako ujiulize swali hili moja tu: je ukiondoka Leo Duniani unataka ukumbukwe na watanzania kwa lipi?

Kumbuka wewe ni mwanamke wa kwanza katika historia ya Tanzania kukaria hicho kiti.

Kwa maana hiyo unawajibu mkubwa sio tu kwa wanawake wa taifa hili Bali pia KWA wanawake wote Duniani.
Pia unawajibu mkubwa zaidi kwa watanzania wote na Dunia nzima kwa ujumla.

Kwani wanawake wenye nafasi kama yako katika Dunia hii, hawazidi kumi.

Unaweza ukawa una unafurahia Sana kuwa mkuu wa nchi kwa Sasa, na ukasahau kabisa kuwa wewe pamoja na nguvu ulizo nazo za uraisi, lakini bado wewe ni binadam wa kawaida kabisa.

Na kama unakumbuka Hilo, basi na uhakika hautaziba masikio na macho yako na kupuuzia watu wote wale walio tembea kwa miguu kwa zaidi ya kilometers 30.

Hivyo nakuomba utafakari Sana kwa kina bila kuhusisha hao wanao kuzunguka.

Maana hao hawawezi kukwambia UKWELI.
Ila watakwambia kile unacho taka kusikia na ambacho hakiwezi kuhatarisha nafasi zao kwenye utawala wako.

Hivyo ni vizuri kusikiliza watu wa kawaida kama MIMI, ambao Hawana masirahi yoyote na utawala wako au Chama chochote cha siasa.

Ukisha maliza kutafakari kwa kuweka masirahi ya taifa mbele, na kuyakana ya kwako na wanao kuzunguka.

Hakika utafanya maamuzi ambayo yatakufanya uishi miaka mia, baada wewe kutoweka Duniani.

Mhesbimiwa Samia kama huwezi kukaa peke yako kwa siku moja na kutafakari mambo ya taifa. Basi panga na usalama wa taifa, siku moja ujifanye raia wa kawaida uingie mitaani uongee na watu wa kawaida USIKILIZE Hali zao, za maisha.

Na waulize wanaona je Chama chako na utawala wako? Ila ukifanya hivyo usiruhusu mtu yoyote akuchagulie sehemu ya kujichanganya au watu wa kuongea nao. Maana ukiruhusu hivyo hao wa usalama wata kupangia watu wao watakao kueleza Yale Yale watu wa Chama chako wamekuwa wakikueleza.

Mhesbimiwa raisi Samia, la mwisho ambalo nataka nikudokeze, na ambalo watu wanao kuzunguka hawawezi kukwambia.

Ni kwamba, watanzania waleo sio wale wa miaka ya 70s kuja mpaka miaka ya mwanzoni mwa 1990s. Watanzania wa Leo wanajuwa kutafuta Habari nje ya Habari.

Kwa maneno mengine propaganda na maigizo yanayo fanya na viogozi wa Chama chako ccm kupindisha ukweli, Hayafanyi kazi tena.

Kwani siku hizi Kuna wasomi wengi mitaani kuliko maofisini. Mimi nakushauri wewe na chama chako kama mnataka kuendelea kuwepo kwenye mchezo wa siasa kwa miaka mingine zaidi ya kumi.

Badilisha mbinu za utawala na mbinu za kushawishi wananchi.

Haya mambo ya kutisha watu, na kutengeneza matukio, kutumia wasanii, na vyombo vya Habari kulisha watu Habari za kupika.

Sio tu yatakuja kuangamiza Chama chako Bali pia yatakuja kuuwa sekita zote zinazo tumika kuficha ukweli, wa Hali halisi ya maisha ya watanzania.

Mwisho na maliza kwa kusema : nafasi uliyo nayo usipo itumia kubadilisha mifumo mbovu ya utawala. Basi jiandae kuingia kwenye vitabu vya historia ya walevi wa madaraka kama kina mbutu, Charles Taylor, omari Bashir wa Sudan na wengine wengi kama hao.

Kumbuka uraisi unapita hata ukitumia nguvu kuendelea kuwa raisi kwa miaka mingine kumi zaidi. Haita kuwa na faida yoyote kwako maana mda wako wa kuwepo Duniani hauwezi kuongezeka hata siku MOJA.

NA KILA SIKU IPITAYO NDIO MDA WAKO WA KUWEPO DUNIANI UNAPUNGUWA. La mwisho jifuze kupitia kwa mtangulizi wako Magufuli.

Maana wewe unajuwa ukweli kuhusu mtangulizi wako kuliko watu wengi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom