Rais Samia ni chaguo la Mungu na aliandaliwa na Mungu kuongoza Taifa letu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu watanzania,

Huo ndio ukweli, ndio uhalisia,ndio jibu kwa wale wote wanaojiuliza ujasiri mkubwa alio nao na alio uonyesha Rais samia katika kuongoza Taifa letu pamoja na mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya muda mfupi.

Ni dhahiri katika ulimwengu wa kiroho Mwenyezi Mungu alikuwa Amemuandaa Rais samia kuja kuongoza Taifa letu na kulivusha katika kila Hatua,ndio maana tunaona hakuna jambo lililomtetemesha Rais wetu na kumpoteza muelekeo na Dira,ndio maana tumeona namna alivyo endelea kuwa imara na kuyakabili matatizo yaliyojitokeza mbele yetu kama Taifa licha ya baadhi ya watu kutaka kuleta Ubaguzi kwa misingi ya Udini ,ukabila ,ukanda na hata jinsia ili kumhamisha kiajenda na kutaka kumdhoofisha kiutendaji.

Ikumbukwe ya kuwa Mungu hutenda miujiza yake kupitia watu,huwasaidia watu kupitia watu,humuinua mtu kupitia watu,huwakomboa watu kupitia watu,huwafuta machozi waja wake kupitia watu,huwapa watu uongozi wake kupitia watu wake aliowateua katika ulimwengu wa kiroho kabla hata ya kuzaliwa kwao na kuonekana machoni pa watu.

Rais Samia Ni mteule na Chaguo la Mungu katika ulimwengu wa kiroho katika kuliongoza Taifa letu Tangia hata kabla ya kuzaliwa kwake, maana yeye hutujuwa sisi tungali bado katika matumbo ya mama zetu.

Ukiwa mteule na uliyeteuliwa kutumika kama chombo cha Mungu kama ilivyokuwa kwa aliyejulikana awali kama Sauli au Musa au Joshua au Esther lazima mkono na uso wa Mungu uwe nawe popote uwapo,lazima Mungu apigane upande wako.

Hata ipite dhoruba za aina mbalimbali lakini mwisho wa siku lazima uibuke mshindi tu,ndio maana Rais samia amekuwa mshindi katika mambo yote,ndio maana hakuna alipokwama na tulipokwama kama Taifa,Hakuna tulipoyumba wala Taifa letu kupasuka ,kwa kuwa Mungu yupo mbele ya Rais Samia na Taifa letu.Mungu anamtumia Rais samia kama chombo chake katika kuwaongoza watanzania, kuwafuta machozi waliao, kuwapa faraja waliokata Tamaa,kuwainua wanyonge na kuwapa nguvu za kiuchumi, kuwashika mkono masikini na kuwapa matumaini yatima, wajane, wazee na watu wasio jiweza.

Hivyo hakuna mtu yeyote au kikundi au chama chochote kitakachofanikiwa kumdhoofisha Rais samia kiutendaji,kila baya litakalotaka kuinuka dhidi ya Rais samia litaishia kufa kibudu kwa kukataliwa na watanzania.

Rais samia ni mmoja lakini anazungumza kwa mamilioni kupitia midomo na vinywa vya wananchi wanaoendelea kumtetea na kumsemea, kwa kuwa ni mpango wa Mungu anayeendelea kumlinda Rais samia katika kutimiza Agano lake katika ulimwengu wa kiroho wa kumfanya Rais Samia Kuongoza Taifa hili na kulivusha Salama.

Atapitia dhoruba lakini atashinda,atakutana na magumu lakini atashinda,atakutana na vikwazo lakini ataibuka na kubakia katika njia sahihi na mshindi, hata yumba wala kuyumbishwa na mwanadamu yoyote,.Amepewa kibali na mwenyezi Mungu na hakuna wa kumzuia wala kumkwamisha. Hakuna kinywa kitakachoinuka wala kitakacho shinda mbele yake wala fimbo itakayo inuka mbele yake na kumfikia.Ni nyota ya matumaini na Taa ya Taifa na nuru ya wanyonge.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Mkuu?

Mungu wa Mh. Samia ni Nani?

Me nadhan anaitwa CCM.

Je, Mungu wa Lissu ni huyo huyo wa Samia?
Wa Mwabukusi je?
Na Mungu wa akina sisi ambao hatulambi asali?

Mkuu miungu ni mingi mno.
 
Ndugu zangu watanzania,

Huo ndio ukweli ,ndio uhalisia,ndio jibu kwa wale wote wanaojiuliza ujasiri mkubwa alio nao na alio uonyesha Rais samia
Nakuomba sana usimkufuru Mungu utaafhibika kwa njia ya G5 Acha upumbavu wako tafuta kazi ya kufanya na tumia akili yako visuri mungu amekujalia akili usimjaribu na kumkebehi
 
Acha kutukana matusi na badala yake jikite katika kujibu hoja kwa hoja na siyo viroja
 
Nilijua utasahau kuweka namba ya simu nikukumbushe

Hii Nchi ngumu sana kwa kweli
 
Ndugu zangu watanzania,

Huo ndio ukweli ,ndio uhalisia,ndio jibu kwa wale wote wanaojiuliza ujasiri mkubwa alio nao na alio uonyesha Rais samia katika kuongoza Taifa letu pamoja na mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya muda mfupi.

Ni dhahiri katika ulimwengu wa kiroho Mwenyezi Mungu alikuwa Amemuandaa Rais samia kuja kuongoza Taifa letu na kulivusha katika kila Hatua,ndio maana tunaona hakuna jambo lililomtetemesha Rais wetu na kumpoteza muelekeo na Dira,ndio maana tumeona namna alivyo endelea kuwa imara na kuyakabili matatizo yaliyojitokeza mbele yetu kama Taifa licha ya baadhi ya watu kutaka kuleta Ubaguzi kwa misingi ya Udini ,ukabila ,ukanda na hata jinsia ili kumhamisha kiajenda na kutaka kumdhoofisha kiutendaji.

Ikumbukwe ya kuwa Mungu hutenda miujiza yake kupitia watu,huwasaidia watu kupitia watu,humuinua mtu kupitia watu,huwakomboa watu kupitia watu,huwafuta machozi waja wake kupitia watu,huwapa watu uongozi wake kupitia watu wake aliowateua katika ulimwengu wa kiroho kabla hata ya kuzaliwa kwao na kuonekana machoni pa watu.

Rais Samia Ni mteule na Chaguo la Mungu katika ulimwengu wa kiroho katika kuliongoza Taifa letu Tangia hata kabla ya kuzaliwa kwake, maana yeye hutujuwa sisi tungali bado katika matumbo ya mama zetu.

Ukiwa mteule na uliyeteuliwa kutumika kama chombo cha Mungu kama ilivyokuwa kwa aliyejulikana awali kama Sauli au Musa au Joshua au Esther lazima mkono na uso wa Mungu uwe nawe popote uwapo,lazima Mungu apigane upande wako.

Hata ipite dhoruba za aina mbalimbali lakini mwisho wa siku lazima uibuke mshindi tu,ndio maana Rais samia amekuwa mshindi katika mambo yote,ndio maana hakuna alipokwama na tulipokwama kama Taifa,Hakuna tulipoyumba wala Taifa letu kupasuka ,kwa kuwa Mungu yupo mbele ya Rais Samia na Taifa letu.Mungu anamtumia Rais samia kama chombo chake katika kuwaongoza watanzania, kuwafuta machozi waliao, kuwapa faraja waliokata Tamaa,kuwainua wanyonge na kuwapa nguvu za kiuchumi, kuwashika mkono masikini na kuwapa matumaini yatima, wajane, wazee na watu wasio jiweza.

Hivyo hakuna mtu yeyote au kikundi au chama chochote kitakachofanikiwa kumdhoofisha Rais samia kiutendaji,kila baya litakalotaka kuinuka dhidi ya Rais samia litaishia kufa kibudu kwa kukataliwa na watanzania.

Rais samia ni mmoja lakini anazungumza kwa mamilioni kupitia midomo na vinywa vya wananchi wanaoendelea kumtetea na kumsemea, kwa kuwa ni mpango wa Mungu anayeendelea kumlinda Rais samia katika kutimiza Agano lake katika ulimwengu wa kiroho wa kumfanya Rais Samia Kuongoza Taifa hili na kulivusha Salama.

Atapitia dhoruba lakini atashinda,atakutana na magumu lakini atashinda,atakutana na vikwazo lakini ataibuka na kubakia katika njia sahihi na mshindi, hata yumba wala kuyumbishwa na mwanadamu yoyote,.Amepewa kibali na mwenyezi Mungu na hakuna wa kumzuia wala kumkwamisha. Hakuna kinywa kitakachoinuka wala kitakacho shinda mbele yake wala fimbo itakayo inuka mbele yake na kumfikia.Ni nyota ya matumaini na Taa ya Taifa na nuru ya wanyonge.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Kwa bandiko hili na kwakuwa umeweka na contact yako,ikitokea hujapigiwa simu wala kutumiwa sms ya kukupongeza kutoka kwa Mamlaka za teuzi,basi itabidi urudi na kujipanga upya tena.Hii mbinu itakuwa haijakusaidia kuyafikia malengo yako.
 
Hapana mimi sitafuti uteuzi hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom