Rais Samia: Milioni 960 za sherehe ya Uhuru zikajenge mabweni shule nane za wanafunzi wenye mahitaji maalum

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
msemajimkuuwaserikali_20221205_p_2986475527007134560_1_2986475518836668125.jpg


NB: Ya Magufuli ni yake Samia.
====


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza TZS milioni 960 ambazo zilitengwa katika bajeti kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru inayoadhimishwa kila Desemba 9, zipelekwe Ofisi ya Rais TAMISEMI na zitumike kujenga mabweni katika shule nane za msingi zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 5, 2022 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, George Simbachawene amezitaja shule hizo kuwa ni Buhangija (Shinyanga), Goeko (Tabora), Darajani (Singida), Mtanga (Lindi), Songambele (Manyara), Msanzi (Rukwa), Idofi (Njombe), na Longido (Arusha).

Amesema shule hizo zimekwisha ratibiwa na TAMISEMI na tayari zimekwisha gawiwa fedha hizo kwa ajili ya kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

“Ikiwa ni dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwajali na kuwajengea mazingira rafiki watu wenye mahitaji maalum hapa nchini, hili ni jambo kubwa na la kishujaa na la kupongezwa sana,” amesema.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika midahalo na makongamano katika wilaya zote na kujadili kwa kina kuhusu maendeleo endelevu katika siku ya maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania.

 
Mheshimiwa Rais Dr. Samia S.Hassan zile milioni 500 ulizotoa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD) Hospitali ya wilaya ya Nyamagana zimepigwa zote, jengo halijaisha watumishi wapo wanarushiana mpira! Mh. Rais pengine una nia nzuri ila tunajua huku chini wanasubiria huo mgao wa madaraja wazitafune kama mchwa!
 
Mheshimiwa Rais Dr. Samia S.Hassan zile milioni 500 ulizotoa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD) Hospitali ya wilaya ya Nyamagana zimepigwa zote, jengo halijaisha watumishi wapo wanarushiana mpira! Mh. Rais pengine una nia nzuri ila tunajua huku chini wanasubiria huo mgao wa madaraja wazitafune kama mchwa!
Pesa zinapigwa sana sana mkuu.
Sio huko tu . Huku niliko ni kiama , kila mtu anaondoka na chake,.
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
ameelekeza fedha zote Tsh. Milioni 960 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe za Uhuru inayoadhimishwa kila mwaka December 9, zipelekwe Ofisi ya Rais TAMISEMI na zitumike kujenga mabweni katika Shule nane za msingi za Wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, George Simbachawene ametoa taarifa hiyo leo ambapo amezitaja Shule hizo kuwa ni Buhangija (Shinyanga), Goeko (Tabora), Darajani (Singida), Mtanga (Lindi), Songambele
(Manyara), Msanzi (Rukwa), Idofi (Njombe), na Longido (Arusha).


Amesema Shule hizo zimekwisha ratibiwa na TAMISEMI na tayari zimekwisha gawiwa fedha hizo kwa ajili ya kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

“Hii ni dhamira ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwajali na kuwajengea mazingira rafiki Watu wenye mahitaji maalum hapa nchini, hili ni jambo kubwa na la kishujaa na la kupongezwa sana na Wananchi wote wa
Tanzania.

Milliard ayo
 
View attachment 2436580

NB: Ya Magufuli ni yake Samia.
Uhuru wa taifa letu ndiyo msingi wa taifa husika. Kama tunaweza kufanya sherehe za kuzindua matundu ya vyoo, miradi ya maji nk kwa gharama kubwa tunashindwaje kuona umuhimu wa sherehe ya kumbukumbu ya siku ya uhuru ambayo inabeba alama na historia ya taifa letu?. Kwa viongozi mliopo madarakani kunahaja ya kuweka vipaumbele vya taifa hili vizuri kwani vinginevyo taifa litaangamia.

Labda kama kuna nadharia nyingine kwamba uhuru waliopigania wakati huo umeshaporwa hivyo hakuna haja ya kufanya sherehe hizi kwa maana kwamba walichopigania kutoka kwa utawala wa mkoloni hakipo tena.
 
Wangepika tu pilau tule tujue na sisi kwenye historia ya maisha yetu tumekula pilau ya Taifa.

Hayo makeki ya Taifa acha wao wale...
 
Back
Top Bottom