Kuacha kufanyika kwa sherehe za Uhuru ni sahihi?

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Rais Samia Suluhu amesema mwaka huu hakutakuwa na sherehe za uhuru na pesa zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya sherehe izo ziende kuimarisha sekta ya elimu wadau wengi wa maendeleo wameunga mkono maamuzi haya na kusema kuwa hili ni wazo zuri halijawai kutokea toka Tanzania ipate uhuru.

Leo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema "Rais Samia ameelekeza Sh. milioni 960 zilizopangwa kutumika kwenye maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru, zikajenge mabweni katika shule 8 za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum".

Shule hizo za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum zitakazojengewa mabweni ni Buhangija- Shinyanga, Goheko - Tabora, Darajani - Singida, Mtanga - Lindi, Songambele - Manyara, Msanzi - Rukwa.

Mungu aendelee kumuweka Rais Smaia Suluhu kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Uhuru wa Tanganyika unamhusu nini Bibi wa Kojani?.
Sahihi

Sherehe uhuru wa Zanzibar mgeni rasmi huwa raisi wa Zanzibar

Sherehe za uhuru wa Tanganyika mgeni rasmi haeleweki mtanganyika

Raisi wa Muungano sherehe inamhusu ni sherehe ya Muungano

Mama Samia yuko sahihi hadi hapo katiba itakaporekenishwa kwenye hili kuonyesha mhusika mkuu upande wa Tanganyika siku.yao ya uhuru ambaye ni mtanganyika ni nani kikatiba?

Vinginevyo pesa zote za sherehe za uhuru wa Tanganyika ziendelee kupelekwa kwenye miradi mingine iliyopo Tanganyika kama alivyofanya
 
Back
Top Bottom