Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
18,126
12,341
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa mujibu wa waziri wa mifugo na uvuvi Mheshimiwa Abdallal Ulega Amesema ya kuwa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan atakuwa mgeni Rasmi wa mkutano wa uvuvi Barani Afrika.

Ameyasema hayo na kutoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam siku ya jana ya Tarehe 23 Mei. Ambapo amesema kuwa mkutano huo utafanyika Tarehe 5-7 Mwezi Julai, katika ukumbi wa Mlimani city unaopatikana Jijini Dar es salaam.

Naweka kalamu yangu chini na sina Maneno mengi na wala sitaki kuwachosheni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ziara, mikutano, makongamano, vigodoro nk haviwezi kumkomboa Mtanzania na kuleta mapinduzi ya kiuchumi.

Mwambieni shillingi inaporomoka thamani, Dola haionekani mitaani, exportation yetu kiduchu, tunakopa kila siku, wizi,, Rushwa vimetamalaki.

UDART imeshajifia, Air Tanzania inachechemea, SGR inasuasua, Stieggler zimepaki sinema tu, Hali ya maisha mitaani inatisha.

Mwambieni uchumi unajengwa kwa watu kufanya kazi kwa bidii, kulinda rasirimali na usimamizi mzuri wa rasirimali watu na sio KUOMBAOMBA na kukopakopa.
 
Huku wavuvi wetu bado wanavua na ngalawa za kusukuma na mwiko, hamasisha wapatiwe mikopo nafuu, Elimu ya uvuvi wa kisasa, technology na masoko badala ya kuhangaika na hii mikutano ya ovyo ovyo isiyo na faida yeyote
 
Kwani umeambiwa mkutano huo ni kwa ajili ya kuomba pesa? Suala la kukopa pesa nalo siyo dhambi wala baya.maana kinachotakiwa kuzingatiwa ni aina ya mkopo, masharti ya mkopo mfano riba yake,muda wa kuanza kurejesha mkopo na muda wa kumaliza mkopo. Mahali unapokwenda kuwekeza mkopo au kazi itakayofanywa na pesa za mkopo. Sera yetu chini ya uongozi shupavu, imara na madhubuti wa Rais Samia imekiwa ikizingatia hayo kwa kuchukua mikopo ya riba nafuu na kuwekeza katika shughuli zenye matokeo chanya kwa uchumi wetu .
 
Huku wavuvi wetu bado wanavua na ngalawa za kusukuma na mwiko, hamasisha wapatiwe mikopo nafuu, Elimu ya uvuvi wa kisasa, technology na masoko badala ya kuhangaika na hii mikutano ya ovyo ovyo isiyo na faida yeyote
Hayo yote serikali yetu inafanya kwa kuwawezesha wavuvi wetu kuwa na zana za kisasa za uvuvi,kusindika au kuhifadhi samaki kwa teknolojia ya kisasa,kuwapatia mitaji kwa mikopo ya masharti nafuu kupitia vikundi vyao pamoja na kuwaunganisha na mabenki mbalimbali hapa nchini.
 
Umepewa shs ngapi kuandika huu urojo? Wewe mwenyewe njaa ndio zinakufanya unaandika huu ujinga. Watoto wako nawaonea huruma kwa hii hasara
 
Back
Top Bottom