Rais Samia kuwa mgeni rasmi miaka 69 ya Uhuru Zambia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,070
49,752
Yule Rais Hichilema ambae Chadema Huwa Wanajidai ni role model wao anamkubali sana Rais Samia kiasi Cha kumpa heshima ya kuwa mgeni Rasmi.

--

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Zambia kuanzia Oktoba 23 hadi Oktoba 25, mwaka huu ikiwa na lengo la kujenga ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Katika ziara yake nchini humo, Rais Samia amekubali pia mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia, yatakayofanyika Oktoba 24, 2023, jijini Lusaka.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, amesema maeneo ya kipaumbele katika ziara hiyo ni pamoja na namna bora ya kuboresha miundombinu inayounganisha Tanzania na Zambia ili kufikia faida za kiuchumi.

Aidha, ziara hiyo pia itaangazia namna ya kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia pamoja na kuibua fursa mpya za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ameeleza kuwa Rais atahudhuria kongamano la biashara kati ya Tanzania na Zambia, ambapo wafanyabiashara wakubwa 100 kutoka Tanzania watashiriki.

“Hii inaonyesha nia ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo na kuendeleza ushirikiano wa kikanda,” ameeleza Makamba.

My Take
Samia ni role model wa Africa, tafuteni kazi ya kufanya 2025.

View: https://twitter.com/eastafricatv/status/1715722032707416259?t=YphSKc7rVk65BSGFXJnvmg&s=19
 
Attachments

  • IMG-20231019-WA0005.jpg
    IMG-20231019-WA0005.jpg
    26.6 KB · Views: 1
Huu ndio ujinga hata kuusoma ni basi, kwani unadhani ni mwaliko wa Mama Abdul au kwa Rais wa Tanzania?
 
Hichilema ni kioo cha upinzani, although wa Zambia na kiherehere Chao wanalia kweli kweli hali ni mbaya mno wanajutia kweli na ndicho kioo cha kwa wale watakaochagua upinzani, iwe fundisho, SOME CHANGE ARE MORE DANGEROUS AND POISONOUS THAN BLACK MAMBA. 😈😈😈
 
Yule Rais Hichilema ambae Chadema Huwa Wanajidai ni role model wao anamkubali sana Rais Samia kiasi Cha kumpa heshima ya kuwa mgeni Rasmi.

Chedema mnazidi kupuuzwa ndani na Nje ya Nchi 🤣🤣🤣🤣

View: https://www.instagram.com/p/CyqGx_jq16z/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

My Take
Samia ni role model wa Africa, tafuteni kazi ya kufanya 2025.

Wewe ni mpumbavu tu hakuna kingine chochote unachojua,kwani kualikwa ndiyo role model au ni ushirikiano uliasisiwa na Julius Nyerere na Kenneth Kaunda na ndiyo maana hizi nchi zote zina Reli inayoziunganisha na inajulikana kwa jina la RELI YA UHURU(TAZARA)
 
Mwaka huu CHADEMA watapasukaa kwa hasira maana Rais wetu Anaendelea kuchanja mbuga tu katika mioyo ya wana Afrika. Rais samia ni kioo kwa Bara la Afrika. Kila mtu na kila kiongozi anatamani kujifunza kutoka kwake. Mungu amjalie maisha marefu yenye heri na Baraka mh Rais wetu Dr Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, jasiri muongoza njia,chuma cha Reli,shujaa wa Afrika na Nuru ya wanyonge.
 
Mtatukana sana mwaka huu na kuzirai chini maana Rais samia anaendelea kusonga mbele kwa kishindo kinachoitetemesha Afrika nzima
 
Mwaka huu CHADEMA watapasukaa kwa hasira maana Rais wetu Anaendelea kuchanja mbuga tu katika mioyo ya wana Afrika. Rais samia ni kioo kwa Bara la Afrika. Kila mtu na kila kiongozi anatamani kujifunza kutoka kwake. Mungu amjalie maisha marefu yenye heri na Baraka mh Rais wetu Dr Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, jasiri muongoza njia,chuma cha Reli,shujaa wa Afrika na Nuru ya wanyonge.
ONA HATA BARAKA NDANI YA TIMU ZETU ONA WAGENI WANAVYOMIMINIKA, HUKO KENYA NI GUMZO HIVI LEO!, KWA UTENDAJI SAFI HASA KATIKA TASNIA ZOTE, ELIMU,
TIBA, KILIMO, MICHEZO, VIWANDA, UWEKEZAJI, UTALII, YAANI ANAPIGA KOTE KOTE, HATARI SANA 😁😁😁
 
Mwaka huu CHADEMA watapasukaa kwa hasira maana Rais wetu Anaendelea kuchanja mbuga tu katika mioyo ya wana Afrika. Rais samia ni kioo kwa Bara la Afrika. Kila mtu na kila kiongozi anatamani kujifunza kutoka kwake. Mungu amjalie maisha marefu yenye heri na Baraka mh Rais wetu Dr Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, jasiri muongoza njia,chuma cha Reli,shujaa wa Afrika na Nuru ya wanyonge.
Umesahau kuweka number yako ya simu.
 
Back
Top Bottom