Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa. Natamani kukutana na Wapinzani

Nahudhunika sana na suala la binadamu mwenye akili timamu kujitoa ufahamu wake waziwazi kulihusisha suala la mashtaka ya mbowe na masuala ya katiba mpya,maana yake kwa hapa watu wanashindwa kutofautisha jambo gani lilifanyika wakati gani, na jambo lipi lilifanyika wakati upi?so ningeliomba chadema na wapambe wao wao waache upotoshaji wa suala hili na tuzisubiri mahakama zetu tukufu zituonyeshe mlango sahihi maana ndivyo vyombo pekee vya umma vyenye kazi rasmi ya kuuthibitishia umma baada ya malumbano ya mawakili wa pande zote mbili kuumana vilivyo na kuja na jawabu moja yenye vithibitisho mahsusi.
 
Hii ni maana yako wewe. Siyo ya kisheria kwa mujibu wa Katiba na mamlaka ya DPP. Jitahidi kusoma Katiba
Wewe akili nyembamba umeona sasa unavyojitia ujuaji? Haya wame-edit vizuri heading umeelewa sasa maana ya maneno yako ya NADHANI na SIDHANI? next time usijifanye mjuaji
 
Kwahiyo mikutano ya hadhara aliyopiga marufuku ni fujo za kisiasa?!

Hili taifa lina watawala wa hovyo sana...

Yaani Dikteta Uchwara la Kiume linatoka, linaingia Dikteta Uchwara la Kike
Na bado mtanena sana kwa lugha!

Si mlikuwa mnademka humu eti hoo sasa tunapumua, tuko huru, tulibanwa sana!

Wenye akili tuliwambia huo ni mfumo na si matakwa ya mtu binafsi, na bado

Anyway.. Mama anafungua nchi,

Mama anawakomesha mataga na sukuma gang

Mama anarudisha hela mtaani ili sisi mibavicha tuwe tunaziokota

Uchumi uko juu, mafuta bei chini, bidhaa muhimu bei sawa na bure.

Bashiru na Polepole wanakiona cha moto

 
Kama kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe alikuwepo mahakamani tangu mwaka Jana kabla ya uchaguzi, Umoja wa Mataifa na watetezi wa haki za binadamu wanasubiri nini kuitangaza Tanzania kuwa nchi inayoongoza duniani kwa "Ustaarabu wa Kijinai?"
Maana hakuna nchi duniani ambayo ingeweza kumwacha anatamba mitaani mtuhumiwa mkuu wa votendo vya ugaidi na kuua viongozi. Yaani tuseme viongozi wa Tanzania walikuwa tayari wauawe na GAIDI huku wakichekelea lakini hawako tayari kuona Mtanzania akienda mahakamani kusikiliza kesi dhidi ya GAIDI huyo? Inachukua mwaka mzima kumkamata GAIDI lakini haiishi hata sekunde kumkamata mwananchi aliyekwenda Kisutu kusikiliza kesi dhidi ya GAIDI huyo?
UN, Amnesty nk mnaionea gere Tanzania, itangazeni mara moja kuwa nchi bora katika Ustaarabu wa kijinai.
 
Hizi ndio nyuzi za kufutwa daima
 
Rais amezungumza vizuri kweli tena kwa uwazi ulio uwazi kwamba shauri hili sio la leo lilikuwepo na bw yule yule alikuwa analifahamu fika na baadhi ya wahusika wa jambo hili walikuwepo rumamnde kwa muda mrefu tu kabla bwana yule hajakamatwa isipokuwa bw yule ni intelegent wa kutisha sana ana akili nyingi sana akaona atafanyaje suala hile alipe mlango au mwonekano mwingine wa ki umma zaidi akaingilia kwa kasi ya katiba mpya bahati mbaya kondoo wake hawajui haya au intelegency aliyonayo kiongozi wao katika kuwatumia vyema koondoo wake, ''Rais amesaema mahakama itatupa majawabu sahihi baada ya mahakimu na wanasheria wa pande zote mbili kukabiliana kwa kina na kuja na jawabu moja tuvute subraaaaa
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Muda utasema
Hata hizi tozo zimetuchosha sana
Ukweli tunatumia gharama kubwa sana kuhudumia Rulling Class
Natamani ifike 2025 nione mtifuano ndani ya chama tawala
 
Narudia...

Wakati Jiwe anaingia madarakani, nilimuunga mkono lakini alipolikoroga nikaanza kumpa vitasa hadi mkawa na kazi moja tu... kumwaga matusi!!!

Alipoingia Samia, sikum-support kama nilivyokuwa nimefanya kwa Jiwe lakini vilevile sikufanya shangwe yoyote kama unavyodai, lakini pia SIKUMPINGA kwa sababu sikuwa na sababu za kumpinga!!

Hivi sasa nina kila sababu ya kumpinga kwa sababu ninazo sababu za kumpinga ambazo sikuwa nazo hapo awali!! Mimi sina siasa za "Oyaa! Oyaa!" za kupinga kila kitu na kushangilia kitu kama mnavyofanya wafuasi wa vyama!!!
 
Duh! Unamtuhumu mtu kwa ugaidi tokea mwaka jana na unamuachia achanje mbuga!!!!!
 
Labda kwa vile yeye yupo huru anaona kila mtu yupo huru

Ukifuata mipaka yako ya kujidai na kujimwayamwaya siku zote utakuwa huru.
Ngoja nikupe mfano, hata kwako huwezi kuwa huru kama umeamua ucheze na mkeo ndombolo huku mmevaa kaunda suti zasiku ya kuzaliwa sebuleni. Hata kama ni baba house, lazima uhuru hautakuwa nao. Uhuru bila mipaka ni fujo. Au wazia kila mtu barabarani anajihisi huru na kuamua kuendesha upande au site yoyote, je barabarani kutakuwa na USALAMA??
 
Mpuuzi wewe unaongea nini! kaa kwa shemeji yako huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…