Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa. Natamani kukutana na Wapinzani

Huyu Mama sikutegemea atakuwa mwongo kiasi hiki.

Mbowe amekamatwa wamesema amekamatwa kwa sababu za tuhuma za ugaidi na siyo kwa sababu ya mkutano wa katiba. Hivi Mbowe alikamatwa pekee yake? Na akina Mwamakula walikamatwa kwa sababu ya tuhuma za ugaidi? Na waliokamatwa juzi ni kwa sababu ya ugaidi? Hao watu zaidi ya150, wote walikamatwa kwa sababu ya ugaidi?

Huyu Mama, basi tu, ngoja nimheshimu kwa sababu tu ya ubinadamu na nafasi yake. Lakini anajidhalilisha na kudhalilisha kiti cha Urais.
 
Urais ni taasisi ndugu yangu mambo mengine yanafanyika hata yeye "NADHANI" huwa hajui. Rais hasilaumiwe sanaa
"The buck stops here"- President Harry S Truman

Kajifunze maana ya huo msemo kisha uje kufuta hiyo posti yako.
 
Wasiomuelewa Rais wetu watapata taabu sana
Binafsi namwelewa sana mama anavyojibu au anavyomaza kwa mambo yasiyokua na tija

Acha kazi iendelee
Nendeni na Gwajima mkachomwe Chanjo ya Corona sasa.
 
Leo katika mahojiano yake na Shirika la Utangazaji BBC yaliyorushwa katika kipindi maalum cha Dira ya Dunia, Mhe. Rais SSH amezungumzia umuhimu wa kukutana na wapinzania.

Hata hivyo kipekee Rais ameeleza kuwa kwa muda amekuwa akisita kukutana na vyama hivyo kutokana na kuwa viko vipande vipande, na amekuwa akisubiri vije pamoja kupitia TCD. Rais ametuambia uchaguzi wa TCD umekwishafanyika na kutoa nafasi ya yeye kuweza kupanga kukutana na vyama hivyo.

Mhe. Rais ameeleza pia kwamba hivi vyama vidogo vidogo vimekuwa na agenda isiyokuwa na mashiko.

Hivyo ni dhahiri kwamba Rais amekitafsiri chama cha CHADEMA kama miongoni mwa vyama vidogo vidogo nchini vilivyo vipande vipande na visivyo na mwelekeo. Kwahivyo CDM isitarajie special treatment waliyokuwa wanadhani wataipata katika utawala huu. Kwa tafsiri ya mama hiki ni chama kidogo.

Kusuka au kunyoa, Chadema ikubali kuingia kwenye hilo kalai la TCD au kuendelea kujimwambafai bila hadhi stahiki.
 
Kwamba siyo Siasa?

1. Kwa nini wanazuwia watu kwenda mahakamani?
2. Kwanini alikamatwa usiku usiku pamoja na waliokuwa wamepanga kwenda kwenye kongamano la kisiasa?...
Uta"Brand" kitu gani katika hali kama hii iliyopo nchini sasa!
 
Yaani unazidi kuonyesha ubovu wa katiba ya sasa! Yaani DPP afute kesi na sababu anayotoa ni kutoona haja ya kuendelea na kesi. Hii ni hatari, maana anaweza kutumika kuvuta muda wa jambo fulani lipite!
Lete katiba ya nchi yoyote duniani ambayo DPP hana mamlaka ya kushtaki na kuondoa kesi mahakamani
 
Leo katika mahojiano yake na Shirika la Utangazaji BBC yaliyorushwa katika kipindi maalum cha Dira ya Dunia, Mhe. Rais SSH amezungumzia umuhimu wa kukutana na wapinzania...
Na kweli kwa sasa Chadema ni chama kidogo. Kigezo kikatiba ni idadi ya wabunge.
 
Baada ya kusikiliza kwa makini majibu ya maswali juu ya Mbowe na nikiunganisha dots na matamshi ya aijipii, sina shaka yoyote kwamba wafuasi wa Mbowe wajindae tu kisaikolojia.

The guy is going down!!! unless litokee shinikizo toka nje na jumuiya zake
 
Back
Top Bottom