Mbunge Mwantum Zodo Aibana Serikali Kuvisaidia Vikundi vya Uzalishaji Mali vya Ufugaji Vinavyosimamiwa na Wanawake

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

Mbunge Mwantum Zodo Aibana Serikali Kuvisaidia Vikundi vya Uzalishaji Mali vya Ufugaji Vinavyosimamiwa na Wanawake

VIKUNDI 102 VYA WAFUGAJI VYANUFAIKA NA MIKOPO

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi amesema vikundi 102 vya Wanawake vyenye wanufaika 875 vinavyojishughulisha na kazi za ufugaji vimekopeshwa kiasi cha Sh Milioni 575.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Mwantum Zodo aliyehoji Serikali ina mpango gani wa kuvisaidia vikundi vya uzalishaji mali vikiwemo vya ufugaji ambavyo wanawake wamehamasika ili waweze kufanya ufugaji wenye tija.

Amesema Halmashauri za Mkoa wa Tanga na maeneo mengine nchini zimekua zikitoa mikopo ya uwezeshaji kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani. Mikopo hiyo imekua ikitumika kwenye shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo ufugaji.

“Kwa mwaka wa fedha 2021/22 na 2022/23, Halmashauri yenye thamani ya Sh Bilioni 4.5 ambapo kati ya fedha hizo Sh Bilioni 1.8 zilikopeshwa kwenye vikundi vya Wanawake,” Amesema Mhe Ndejembi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-03 at 14.39.08.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-03 at 14.39.08.jpeg
    45.3 KB · Views: 1
  • aishauripiiic.jpg
    aishauripiiic.jpg
    76.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom