BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,413
- 8,199
Rais Samia amesema Serikali inashughulikia namna itakavyotoa tena Mikopo ya 10% ya Halmashauri kwaajili ya Vikundi ambayo ilisitishwa baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2022/23 kuonesha kulikuwa na ubadhirifu mkubwa
Akizungumza wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu Dar es Salaam, Rais Samia amesema kuna baadhi ya Watu hawadaiwi Fedha hizo kwasababu ni Watumishi wakiwemo Madiwani na Wenyeviti wa Halmashauri na Wanaounda Vikundi Bandia wanapewa Pesa wakati Vikundi havipo
Rais amesema Fedha hizo zilitengwa kwaajili ya Wananchi lakini zikaanza kutolewa kinyume na taratibu kutokana na baadhi ya Wasimamizi kukosa Uadilifu kwenye majukumu yao