RAIS SAMIA KUHUTUBIA ULIMWENGU KUPITIA BARANa Bwanku M Bwanku.
Mabibi na Mabwana, kesho Alhamisi Septemba 23, 2021 Mwanamke wa shoka Rais Samia Suluhu Hassan atahutubia ulimwengu kupitia Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) Jijini New York, Marekani. Rais Samia atahutubia Baraza hilo lenye Wakuu wa nchi, Serikali na Wakubwa wote wa dunia baada ya kupita miaka 6 bila Mkuu wa nchi ya Tanzania kuhudhuria Baraza hilo muhimu sana kwa uchumi, uwekezaji, biashara na maendeleo ya Taifa letu.
Kitendo tu cha Rais Samia ambaye ametajwa na Jarida la Avance Media la nchini Ghana kuwa moja ya Wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika na dunia kwa ujumla kushiriki Mkutano huo kunamuwezesha kukutana na Wawekezaji na Wafanyabiashara wakubwa wa dunia, Wakuu wa taasisi kubwa za kifedha ulimwenguni kama Benki ya Dunia (WB), Shirika la Biashara duniani (WTO) na wengine wengi na moja kwa moja kuwezesha kushusha uwekezaji mkubwa wa biashara na utalii nchini ambao utatoa ajira kwa Watanzania na kuimarisha uchumi wetu maradufu. Nani Kama Mama Samia?
0657475347