Rais Samia katuthibitishia matumizi ya Kiswahili hayakuwa kukikuza bali kuna mtu lugha ya Kimataifa hakuiweza

Huyu mama mambo ya kiprotokali hayajui vizuri vinginevyo atakua na jambo lake. Waziri wake kaanza na kingereza kisha kaomba radhi aendelee kwa lugha rasmi ya kwao. Rais wake kuja anapwaga tu kizungu. Hakika ni pigo kwa juhudi ya kukipa hadhi yake kiswahili.
Tatizo ni kuwa tunafanya Kiswahili kama mali binafsi ya Tanzania.
 
Jinsi tunavyoendelea kupambana na marehemu ndio jinsi tunavyolijenga jina lake lizidi kuwa kubwa. Tukumbuke, hii ni free airtime. Alipokuwa hai aliongea mwenyewe. sasa hivi tunabeba vipaza sauti kumpigia debe.
JPM kweli alikuwa mwamba. So far tunamkuza kwa kufikiri ndio tunamzamisha
Marehemu hawezi kuzamishwa na maneno, atafutika kwa ukweli kujulikana kama ilivyotokea kwa watu kama Hitler, Bokassa nk
 
Huwezi kusoma kwa mtiririko mzuri lugha usiyo ielewa vizuri. Huoni jamaa hata alipokuwa anaandikiwa akisoma ni vichekesho?
We expect much and credible things from her. Hivi vya kusoma ulichoandikiwa any office sssistant is capable of doing that.
 
Hadi leo kuna wajinga wanajua kuongea kiingereza kizuri ndio usomi!Ni ujuha. Kiingereza ni lugha kama kiswahili tu.acha ujuha na mawazo mgando.
Hata wewe hukijui, ririkuwa harijui kidhungu usitutishe!
 
Usichokijua ni kuwa kiingereza ni lugha ya kimataifa na kiswahili ni lugha ya kitaifa
kusema ati english ni lugha tu kama kiswahili ni kujiongopea
Sio kujiongopea tu bali ni uzwazwa pia
 
Mkutano wake wa kwanza nje ya nchi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katumia Kiingereza lugha ambayo inaeleweka vizuri kwa wenzetu Waganda na hao Wawekezaji badala ya kiswahili ambacho kilikuwa kinalazimishwa na JPM eti kulienzi wakati ukweli ni kuwa lugha hiyo nyingine ilikuwa inampiga chenga hivyo hakuielewa kiufasaha.
Naamini hatukua tunaambiwa ukweli lakini njia iliyokuwa inatumika hangeweza kuwa sahihi kukuza kiswahili nje ya Tanzania bali njia sahihi ni kuifundisha katika mashule na vyuo huko nje.

Hongera kwa rais wetu,ila neno Invitation linatamkwa /in·vuh·tei·shn/ na sio in.vuh.itei.shn/

Hongera sana,kazi iendelee mama
 
Sasa wewe Tz na njaa zako unajifananisha na hayo mataifa? Ni Sawa na jirani maskini kumuiga jirani tajiri kutokuhudhuria misiba na shughuli zingine za kijamii mtaani, subiri mfiwe kwa pamoja then utajua kwa nini yule tajiri alikuwa hahudhurii
Jikite kwenye hoja acha mipasho na kukata viuno usije ukakata shanga bure.
 
Mbona nyie mnamuongelea kumsifu na mapambio?
Ulitaka yale aliyoharibu atajwe nani kuwa kaharibu? Nenda DRC, Mobutu anatajwa kwa mabaya yake hadi leo iwe huyu wa juzi ambaye aliowaumiza hata vidonda havijapona!

Siwaongelei wafu nawaacha wapumzike kwa amani.

Mlisema vyuma vimekaza enzi zake, sasa wote mtakua matajiri mbaya wenu kafariki.

Kuhusu Mobutu, hujui unachoongelea, wacongo wanatamani Mobutu angekuwa Rais wao milele kuliko vibaraka walioingia baada yake. Congo ya Mobutu ilikua na maendeleo kuliko hii ya sasa. Sisemi aliyofanya Mobutu ni mazuri ila he's a lesser evil than his successors. And JPM wasn't anywhere near Mobutu.

Jionee mwenyewe hapa maoni ya wacongo:

Mkutano wake wa kwanza nje ya nchi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katumia Kiingereza lugha ambayo inaeleweka vizuri kwa wenzetu Waganda na hao Wawekezaji badala ya kiswahili ambacho kilikuwa kinalazimishwa na JPM eti kulienzi wakati ukweli ni kuwa lugha hiyo nyingine ilikuwa inampiga chenga hivyo hakuielewa kiufasaha.
Naamini hatukua tunaambiwa ukweli lakini njia iliyokuwa inatumika hangeweza kuwa sahihi kukuza kiswahili nje ya Tanzania bali njia sahihi ni kuifundisha katika mashule na vyuo huko nje.

Lugha ilikuwa inampa shida sn anajificha kwenye uzalendo
 
Hadi leo kuna wajinga wanajua kuongea kiingereza kizuri ndio usomi!Ni ujuha. Kiingereza ni lugha kama kiswahili tu.acha ujuha na mawazo mgando.
Lugha yoyote ambayo sio lugha yako ya kwanza wala ya pili kwa tulio wengi na ukaijua vizuri inaonyesha una uwezo mkubwa wa kuelewa vitu haraka hivyo pia akili yako iko vzr
 
Marais wa France,China German,Russia na kwingineko wote hua wanatumia lugha zao,acha kua na mawazo ya kitumwa.
Simu unayotumia apa imetengenezwa kwa lugha ya kitumwa pia na watoto wako uko shuleni wanafundishwa lugha ya kitumwa pia. Anzisha maandamano sasa
 
Back
Top Bottom