Rais Samia katuthibitishia matumizi ya Kiswahili hayakuwa kukikuza bali kuna mtu lugha ya Kimataifa hakuiweza

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,215
Mkutano wake wa kwanza nje ya nchi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katumia Kiingereza lugha ambayo inaeleweka vizuri kwa wenzetu Waganda na hao Wawekezaji badala ya kiswahili ambacho kilikuwa kinalazimishwa na JPM eti kulienzi wakati ukweli ni kuwa lugha hiyo nyingine ilikuwa inampiga chenga hivyo hakuielewa kiufasaha.

Naamini hatukua tunaambiwa ukweli lakini njia iliyokuwa inatumika hangeweza kuwa sahihi kukuza kiswahili nje ya Tanzania bali njia sahihi ni kuifundisha katika mashule na vyuo huko nje.

Nakwambia nyeti zote za mauwongo na utapeli wa awamu ya 5 zitaanikwa mchana kweupe sasa. MATAGA watajificha wapi masikini!
 
... delegation za Her Excellency abroad zitakuwa miongoni mwa delegation zenye furaha na amani mama atakapokuwa anasimama ku-deliver speeches zake. Ule ujinga wa "kuokoa jahazi" sijui upumbavu gani umekwisha rasmi! Inapofika hatua hadi host wako "anaokoa jahazi" ni fedheha kwa taifa!
 
Kumkosoa mtu kuwa hafahamu kiingereza hata wazungu wenyewe watakuona una upumbavu au kichwani haupo vizuri. Kiingereza si lugha ya mtu husika akijua au asipojua siyo issue. Kikwete hakuwa akifahamu kiingereza vizuri. Mwinyi hakuwa akifahamu kiingereza vizuri ila alizunguza kiswahili kizuri cha kuvutia.

Marais waliokuwa wakifahamu kiingereza vizuri ni Nyerere na Mkapa. Kiingereza cha Mama Samia cha kawaida. But pia sawa. Anafahamu kiingereza. So what? Mumlaumu mtu ambaye hafahamu kiswahili na ni mtanzania. Mengine ni kuendeleza utumwa karne ya 21.
 
Inatosha sasa tumuache mzee apumzike tuige yale mema mabaya tuyaepuke yaani nyuzi zimekuwa nyingi sana tuache izo
Kwa mateso aliyowaachia watu, sio rahisi kumuacha , tatizo lake hayo mabaya aliyowafanyia watu, si kutokana na sheria bali zilikuwa chuki zake binafsi tu kwa wahusika!!kila kiongozi kuna mabaya lazima utawafanyia watu kutokana na kusimamia sheria, lakini huyu hakuwa hivyo, chuki binafsi ndio zimewaumiza wengi!!acha watu wamalize hasira zao.
 
Back
Top Bottom