Rais Samia: Hili nalo nendeni mkalitizame

Rais Samia: Hili nalo nendeni mkalitizame

Mtoa mada inaonyesha umelelewa kikatili sana,inawezekana umelelewa kwa kipigo na manyanyaso..

Watu walio lelewa kwa bakora, ukizungumza nao au kuwaamrisha kwa sauti ya upole wanakuwa hawakufahamu,..wanachofahamu wao lazima itumike nguvu ya ziada

Mtu kama Magufuli,kisaikologia inaonyesha kuwa alipata shida sana katika malezi yake,vipigo,matusi vilikuwa vya kawaida utotoni kwake..

Wanasaikologia wanasema ukimlea mtoto kikatili na yeye atakuwa katili,Waswahili wana sema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo..

Raisi wetu Samia inaonyesha alipata malezi mazuri,kwahiyo anatuongoza kama alivyo lelewa,anatuongoza vizuri bila vishindo,bila utekaji,bila mauaji,bila utumbuaji hazarani,bila usingenyaji,bila sifa..

Raisi Samia Suluhu Hassan ni Mzanzibari,katokea kusini mwa Zanzibar..Wazanzibari wanajulikana kwa ukarimu wao,busara zao,upole wao

familia nyingi za kizanzibati zinawalea watoto wao kwa halua na tende,na urojo sio kwa ngumi na bakora..

Acha raisi atuongoze kwa busara na amani,hatutaki kuona viroba coco beach,acha kazi iendelee,kama humfahamu hamia Burundi au Rwanda
Rais anatakiwa atoe maelekezo ya kiutendaji yanayohitaji utekelezaji , wala sio kuombana na kubembelezana!.

NB: nikukumbushe kuwa ni "Rais" na sio "Raisi"
 
Unamdanganya Rais wako!
If you like her, tell her the truth! Vinginevyo hatutakuelewa
Mimi swishing maisha ya ku pretend, refer comments zangu humu, mimi SIO ccm team and will never join them, President Samia nime m judge as she is,kwangu yupo Safi so far,nchi hii ni ngumu maana mazuzu ni wengi sana na wasaidizi wengi wake ni wanafiki, ni wachumia tumbo
 
Kashfa zako hazipunguzi chochote ktk mamlaka yake.
Kwa Samia unajizeesha bure mana huna cha kubadili.
Majeshi yote yanampigia salute, hana nenda kazuie ss
Wewe bado ni kinda.

Una mengi ya kujifunza.
 
"Hakuna cha Lokudown wala cha shangazi yake lokudown" by Jiwe baada ya hofu ya covid-19 kupanda juu nawatu kuanza kupiga ramli kuwa inakuja lockdown na biashara kufungwa.
Mimi ndiye Rais wa Tanzania, nawaagiza ma Rc wote,ma Dc wote ,wakurugenzi wote ifikapo kesho saa mbili malipo yote yamemalizwa!!!
Sikia huko nje watakavyotetemeka kuanzia ikulu mpk vitongojini!!
 
Naam, hii ndio lugha ya Amiri Jeshi Mkuu.

Angekuwa samia hapo angeanza kujing'ata ng'ata na kujiliza liza mbele ya mabeberu.

Lugha za kiume hizi. Mpaka mawakala wa ibilisi wanatetemeka.
Mi naikumbuka ile kauli ua Jiwe akimuuliza IGP Sirro "...eti Polisi mnamwita mtu kituoni nae anakuja eti na waumini wake wanaimba siku nzima hapo kituoni. Eti CDF, inaweza kutokea kambini kwenu...?"

Kesho yake Manji aliipata freshi!
 
Nakumbuka Advance mwalimu wa BAM alikuwa anatubembeleza kuandika na kufanya kazi zake mwisho wa siku karibia robo tatu ya darasa walikua hawana hata daftari la hilo somo wala kuandika chochote zaidi kua na daftari la kuzugia tu anapokua darasani.
Mrejesho sas, matokeo ya BAM yakawaje??
 
Maendeleo yanakuja vipi kama huwezi kutoa amri zinazotekelezwa?

Kama Rais wa nchi, kuna wakati lazima ukitoa AMRI, mamlaka zote za chini zinakutii.

It is called, "the hierarchy of power". You don't have power if you can't command anything.

Hata sisimizi watakucheka.
Una mentality ya punda..huendi bila mboko
 
Mrejesho sas, matokeo ya BAM yakawaje??
Tuliwahi kufanya Joint na shule fulani mimi nilipata moja na nusu nilidhani nitakuwa wa mwisho kumbe kuna kiazi mwenzangu aliscore moja ikawa kasoro watu 3 class ambao hawakupata F. Baada ya hapo wanaanza kutoa makucha kukagua notes na hata watu kupigwa mikwaju inapobidi baadae mabadiliko yakaonekana.
 
Tuliwahi kufanya Joint na shule fulani mimi nilipata moka na nusu nilidhani nitakuwa wa mwisho kumbe kuna kiazi mwenzangu aliscore moja ikawa kasoro watu 3 class ambao hawakupata F. Baada ya hapo wanaanza kutoa makucha kukagua notes na hata watu kupigwa mikwaju inapobidi baadae mabadiliko yakaonekana.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe bado ni kinda.

Una mengi ya kujifunza.
Nyoo!
Nijifunze kwa washamba nyie wa usukumani!!
Kuna mnachokijua zaidi ya kuishi porini na mifugo.
Mnakuja mjini hamjui ht kuvaa suruali.
Mkituona na kanzu zetu nyie si mlikuwa mnakimbia eti mmeona jini!
Hata kupika bado, hamjui ht kula chapati kwa mchuzi.
 
Mkuu, tafadhali naomba umuheshimu Mama. Mkosoe kwa staha siyo kwa dhiaka tafadhali. Yule kwa Sasa ndiye "nembo" ya Taifa Letu ujue. Kumdhiaki ni kutudhiaki watanzania. Hii wengi wetu hatuwezi kukubali.
Hivi unadhani anajua hata alichokiandika huyo.
Ndo kwanza anajifunza lugha.
Ushamba umemuathiri sana. Kwake yeye kila akimuona mtu mwenye furaha roho yamuuma
 
"Hakuna cha Lokudown wala cha shangazi yake lokudown" by Jiwe baada ya hofu ya covid-19 kupanda juu nawatu kuanza kupiga ramli kuwa inakuja lockdown na biashara kufungwa.
Mkuu kwa ridhaa yako naomba hiyo nukuu yako niitumie kwenye ka mkweche kangu ka kusafirisha abiria huko mjini!
 
Mimi ndiye Rais wa Tanzania, nawaagiza ma Rc wote,ma Dc wote ,wakurugenzi wote ifikapo kesho saa mbili malipo yote yamemalizwa!!!
Sikia huko nje watakavyotetemeka kuanzia ikulu mpk vitongojini!!
Samia hawezi kuwa na haya mamlaka. Amekaa kiudhaifu dhaifu sana.

Nafikiri kuwa na mamlaka ni KIPAWA pia.

Unaweza ukatunukiwa mamlaka ya urais na ya kijeshi lakini bado ukawa dhaifu sana.

You are vested with powers but you are powerless from within.

Vested powers are an illusion if you don't have powers in you.

Unakuwa kama chui wa makaratasi.
 
Ni mara kadhaa sasa nimekuwa nikimfuatilia huyu samia, nikagundua lugha yake ni nyepesi sana haina mamlaka ya mtu mwenye hadhi ya Rais au mtu "anayedhaniwa" kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

Si zaidi ya mara moja nimemsikia akitoa lugha dhaifu kama vile "nadhani hili tutalifanyia kazi" , au "hili nalo nadhani tutaenda kulitizama".

Lugha za sampuli hii ni lugha zisizo na amri ya kuchagiza utekelezaji.

Ni aina ya lugha ambazo mara nyingi nimezisikia zikitumika kwenye 'Kitchen parties' na matamasha ya kina mama ya kuhamasishana.

Kwa mtu "anayejiita" au "anayedhaniwa" kuwa ni Amiri jeshi mkuu wa nchi, anatarajiwa kuwa na ulimi wenye mamlaka na unaotoa amri.

Vinginevyo tutaanza kusikia wale wapambe wanajiliza humu, oooh mama anahujumiwa, mara oohh mama karogwa!!!

Hakuna cha mama anahujumiwa, anajiroga mwenyewe kwa ulegevu wa lugha zake.

Yeye mwenyewe alisema hawezi kuongea, ati anatenda kwa kalamu!!

Tumepigwa; hakuna Rais hapo. Wewe mtu anawaambia wateule wake “…jipimieni, kuleni kwa urefu wa kamba zenu…” bado kweli unaona kuna Rais hapo?
 
Piga kazi mama tumecheleweshwa mnooo kama taifa. Kanyaga twende
 
Back
Top Bottom