Rais Samia: Hili nalo nendeni mkalitizame

Rais Samia: Hili nalo nendeni mkalitizame

"Hakuna cha Lokudown wala cha shangazi yake lokudown" by Jiwe baada ya hofu ya covid-19 kupanda juu nawatu kuanza kupiga ramli kuwa inakuja lockdown na biashara kufungwa.
... akapatiwa lockdown ya milele na kitu kilekile alichokidharau.
 
Mm nachkulia kauli izo km kauli za busara, manake haukurupuki kwa unachoamishwa mpaka baada ya upembuzi yakinifu. Na baada ya kubaini ndio mtu anakula ubalozi. Ila tunatofautiana makuzi tulopitia ktk femlia zetu.
So U r right by the way
 
Ni mara kadhaa sasa nimekuwa nikimfuatilia huyu samia, nikagundua lugha yake ni nyepesi sana haina mamlaka ya mtu mwenye hadhi ya Rais au mtu "anayedhaniwa" kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

Si zaidi ya mara moja nimemsikia akitoa lugha dhaifu kama vile "nadhani hili tutalifanyia kazi" , au "hili nalo nadhani tutaenda kulitizama".

Lugha za sampuli hii ni lugha zisizo na amri ya kuchagiza utekelezaji.

Ni aina ya lugha ambazo mara nyingi nimezisikia zikitumika kwenye 'Kitchen parties' na matamasha ya kina mama ya kuhamasishana.

Kwa mtu "anayejiita" au "anayedhaniwa" kuwa ni Amiri jeshi mkuu wa nchi, anatarajiwa kuwa na ulimi wenye mamlaka na unaotoa amri.

Vinginevyo tutaanza kusikia wale wapambe wanajiliza humu, oooh mama anahujumiwa, mara oohh mama karogwa!!!

Hakuna cha mama anahujumiwa, anajiroga mwenyewe kwa ulegevu wa lugha zake.

Yeye mwenyewe alisema hawezi kuongea, ati anatenda kwa kalamu!!
Hivi anasubiri nini KUWAFUTA KAZI Mwigulu na Makamba?

Kufanya KAZI na watu wa aina hii lazima wapigiwe kelele masikioni Ili masikio YAZIBUKE Si kuwaachia kutumia akili zao.

Kuendelea kuwaachia hapo ni KUTUDHIHAKI wananchi.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mbongo unamwambia kwa lugha ya kuombaaa utajua hujuii
Nakumbuka Advance mwalimu wa BAM alikuwa anatubembeleza kuandika na kufanya kazi zake mwisho wa siku karibia robo tatu ya darasa walikua hawana hata daftari la hilo somo wala kuandika chochote zaidi kua na daftari la kuzugia tu anapokua darasani.
 
Lazima awabembeleze watanganyika..akiwakalipia nchini mwao wamfurumushie visiwani kwani yeye hapendi kulamba asali.

Zenji kuna nuka umasikini na ujinga.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote hana sababu ya kumiogopa mtu yeyote awe wa bara au visiwani yeye ndiye Top Nchi nzima !!
 
Mtoa mada inaonyesha umelelewa kikatili sana,inawezekana umelelewa kwa kipigo na manyanyaso..

Watu walio lelewa kwa bakora, ukizungumza nao au kuwaamrisha kwa sauti ya upole wanakuwa hawakufahamu,..wanachofahamu wao lazima itumike nguvu ya ziada

Mtu kama Magufuli,kisaikologia inaonyesha kuwa alipata shida sana katika malezi yake,vipigo,matusi vilikuwa vya kawaida utotoni kwake..

Wanasaikologia wanasema ukimlea mtoto kikatili na yeye atakuwa katili,Waswahili wana sema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo..

Raisi wetu Samia inaonyesha alipata malezi mazuri,kwahiyo anatuongoza kama alivyo lelewa,anatuongoza vizuri bila vishindo,bila utekaji,bila mauaji,bila utumbuaji hazarani,bila usingenyaji,bila sifa..

Raisi Samia Suluhu Hassan ni Mzanzibari,katokea kusini mwa Zanzibar..Wazanzibari wanajulikana kwa ukarimu wao,busara zao,upole wao

familia nyingi za kizanzibati zinawalea watoto wao kwa halua na tende,na urojo sio kwa ngumi na bakora..

Acha raisi atuongoze kwa busara na amani,hatutaki kuona viroba coco beach,acha kazi iendelee,kama humfahamu hamia Burundi au Rwanda
Kwa watoto watukutu ni lazima mlezi wakuogope vinginevyo huwezi kuwalea!!
 
Ni mara kadhaa sasa nimekuwa nikimfuatilia huyu samia, nikagundua lugha yake ni nyepesi sana haina mamlaka ya mtu mwenye hadhi ya Rais au mtu "anayedhaniwa" kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

Si zaidi ya mara moja nimemsikia akitoa lugha dhaifu kama vile "nadhani hili tutalifanyia kazi" , au "hili nalo nadhani tutaenda kulitizama".

Lugha za sampuli hii ni lugha zisizo na amri ya kuchagiza utekelezaji.

Ni aina ya lugha ambazo mara nyingi nimezisikia zikitumika kwenye 'Kitchen parties' na matamasha ya kina mama ya kuhamasishana.

Kwa mtu "anayejiita" au "anayedhaniwa" kuwa ni Amiri jeshi mkuu wa nchi, anatarajiwa kuwa na ulimi wenye mamlaka na unaotoa amri.

Vinginevyo tutaanza kusikia wale wapambe wanajiliza humu, oooh mama anahujumiwa, mara oohh mama karogwa!!!

Hakuna cha mama anahujumiwa, anajiroga mwenyewe kwa ulegevu wa lugha zake.

Yeye mwenyewe alisema hawezi kuongea, ati anatenda kwa kalamu!!
Kila binadamu kaumbwa tofauti. Unataka a force nature kwa kufoka wakati hakuumbwa hivyo? Na alishasema, akikwambia naomba mkafanye hivi...haimaanishi ni udhalili# Tuheshimu kila kiongozi na tabia zake za uongozi. 🙏🙏🙏
 
Kwa watoto watukutu ni lazima mlezi wakuogope vinginevyo huwezi kuwalea!!
Hamna mtoto mtukutu,mtoto anakuwa mtukutu kwavile mzazi unakuwa unapingana na mawazo.ya mtoto..

Kuna mtoto kumuheshimu mzazi na kuna mtoto kumuogopa mzazi..

Mtoto kumfanya akuogope ni kumfanya awe mjinga,..
 
Eee? Kumbe?
FB_IMG_16599691178969588.jpg
 
Back
Top Bottom