Ni mara kadhaa sasa nimekuwa nikimfuatilia huyu samia, nikagundua lugha yake ni nyepesi sana haina mamlaka ya mtu mwenye hadhi ya Rais au mtu "anayedhaniwa" kuwa Amiri Jeshi Mkuu.
Si zaidi ya mara moja nimemsikia akitoa lugha dhaifu kama vile "nadhani hili tutalifanyia kazi" , au "hili nalo nadhani tutaenda kulitizama".
Lugha za sampuli hii ni lugha zisizo na amri ya kuchagiza utekelezaji.
Ni aina ya lugha ambazo mara nyingi nimezisikia zikitumika kwenye 'Kitchen parties' na matamasha ya kina mama ya kuhamasishana.
Kwa mtu "anayejiita" au "anayedhaniwa" kuwa ni Amiri jeshi mkuu wa nchi, anatarajiwa kuwa na ulimi wenye mamlaka na unaotoa amri.
Vinginevyo tutaanza kusikia wale wapambe wanajiliza humu, oooh mama anahujumiwa, mara oohh mama karogwa!!!
Hakuna cha mama anahujumiwa, anajiroga mwenyewe kwa ulegevu wa lugha zake.
Yeye mwenyewe alisema hawezi kuongea, ati anatenda kwa kalamu!!