Rais Samia: Hili nalo nendeni mkalitizame

Rais Samia: Hili nalo nendeni mkalitizame

Dokta Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2022
Posts
1,370
Reaction score
3,165
Ni mara kadhaa sasa nimekuwa nikimfuatilia huyu samia, nikagundua lugha yake ni nyepesi sana haina mamlaka ya mtu mwenye hadhi ya Rais au mtu "anayedhaniwa" kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

Si zaidi ya mara moja nimemsikia akitoa lugha dhaifu kama vile "nadhani hili tutalifanyia kazi" , au "hili nalo nadhani tutaenda kulitizama".

Lugha za sampuli hii ni lugha zisizo na amri ya kuchagiza utekelezaji.

Ni aina ya lugha ambazo mara nyingi nimezisikia zikitumika kwenye 'Kitchen parties' na matamasha ya kina mama ya kuhamasishana.

Kwa mtu "anayejiita" au "anayedhaniwa" kuwa ni Amiri jeshi mkuu wa nchi, anatarajiwa kuwa na ulimi wenye mamlaka na unaotoa amri.

Vinginevyo tutaanza kusikia wale wapambe wanajiliza humu, oooh mama anahujumiwa, mara oohh mama karogwa!!!

Hakuna cha mama anahujumiwa, anajiroga mwenyewe kwa ulegevu wa lugha zake.

Yeye mwenyewe alisema hawezi kuongea, ati anatenda kwa kalamu!!
 
Unataka aseme hao watu wasaliti wa vita vya kiuchumi halafu watandikwe kama ilivyotokea kule kwa mtu fulani.
 
Du kwa hiyo tumeshazoea lugha za ukali ndio maana tunatengeneza familia zilizojaa ukatili, PM wa NZ wadau tafuteni speech zake, hana tofauti kabisa with our president, nchi inahitaji maendeleo yanayoletwa na ari ya kujituma sio vitisho, binafsi my president so far so good, thanks
 
nchi inahitaji maendeleo yanayoletwa na ari ya kujituma sio vitisho

Maendeleo yanakuja vipi kama huwezi kutoa amri zinazotekelezwa?

Kama Rais wa nchi, kuna wakati lazima ukitoa AMRI, mamlaka zote za chini zinakutii.

It is called, "the hierarchy of power". You don't have power if you can't command anything.

Hata sisimizi watakucheka.
 
Ni mara kadhaa sasa nimekuwa nikimfuatilia huyu samia, nikagundua lugha yake ni nyepesi sana haina mamlaka ya mtu mwenye hadhi ya Rais au mtu "anayedhaniwa" kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

Si zaidi ya mara moja nimemsikia akitoa lugha dhaifu kama vile "nadhani hili tutalifanyia kazi" , au "hili nalo nadhani tutaenda kulitizama".

Lugha za sampuli hii ni lugha zisizo na amri ya kuchagiza utekelezaji.

Ni aina ya lugha ambazo mara nyingi nimezisikia zikitumika kwenye 'Kitchen parties' za matamasha ya kina mama ya kuhamasishana.

Kwa mtu "anayejiita" au "anayedhaniwa" kuwa ni Amiri jeshi mkuu wa nchi, anapaswa kuwa na ulimi wenye mamlaka na unaotoa amri.

Vinginevyo tutaanza kusikia wale wapambe wanajiliza humu, oooh mama anahujumiwa, mara oohh mama karogwa!!!

Hakuna cha mama anahujumiwa, anajiroga mwenyewe kwa ulegevu wa lugha zake.

Yeye mwenyewe alisema hawezi kuongea, ati anatenda kwa kalamu!!
 
Uongozi sahihi so kuamlishana Bali kueleweshana mkuu
Rais sio karani wa vikoba..

Rais ni kiongozi wa nchi mwenye mamlaka ya KUAGIZA na KUAMRISHA. (at some point in time).

Amiri jeshi mkuu unabembelezana? nadhani hii, nadhani tuta... nadhani... nadhani!!!!!!!!!!!!! ???

Hata sekretari wa mahakama aliyeishia fom foo hawezi kuwa na lugha ya aina hii!
 
Back
Top Bottom