Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Tanzania tuna hifadhi ya gesi iliyofikia ujazo wa Trilion 57 cubic f.
Kwa mujibu wa hotuba ya Rais wakati wa kusaini mkataba wa kwanza wa uwekezaji wa Gesi baina ya Serikali na wawekezaji kuna vitalu takribani 28 vya gesi bado havijafanyiwa utafiti jambo ambalo endapo litafanyika linaweza kuifanya Tanzania kuwa na Lita za ujazo zaidi ya Trilioni hata 200 huko mbeleni.
Kwa sasa kuna Gesi inatolewa Songosongo na inasemekana ipo nyingi sana na matumizi yake madogo sana. Hali halisi inaonesha gesi inayouzwa na TPDC inauzwa kwa gharama ndogo sana kulinganisha na mafuta
Mapendekezo yangu
1. Serikali ije na mpango wa kubadilisha matumizi ya vyombo vya moto kutoka kutumia Mafuta tu hadi Gesi na Mafuta. Hii itawapa ahueni wananchi kuchagua kutumia Gesi au mafuta
2. Vianzishwe vituo vya Gesi nchi nzima kwa ushirikiano wa Serikali na Sekta binafsi
Haina ubishi kuwa gharama kubwa za nishati duniani ikiwemo Tanzania zinachangia sana kupanda gharama za maisha na bidhaa nyingine . Ni vizuri tukaenda kweli kwenye uchumi wa Gesi kwa kubadili chanzo cheti cha Nishati. Hili litaenda vizuri sana
Tumeanza kwenye nishati ya kupikia. Nina uhakika litaokoa sana miti yetu na mazingira yetu miaka ijayo, sasa twende kwenye vyombo vya moto ili tuokoe kuongezeka kwa gharama za maisha