Rais Samia aibeba Tanzania COP28

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
20231203_171516.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya kuungana na viongozi zaidi ya 160 duniani katika mji wa Dubai kwenye mkutano wa kujadili jinsi ya kukumbana na mabadiliko ya tabia nchi(COP28).

Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan ameibeba kwa dhati ajenda ya matumizi ya nishati mbadala kutokana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi, ilioneshwa makala yenye maudhui juu ya madhara ya matumizi kuni kwa familia za kiafrika hususani Tanzania. Lengo lilikuwa ni kuonesha umuhimu wa matumizi wa nishati mbadala kama gesi na umeme.

Tunafahamu ajenda ya Mhe, Rais kuhusiana na umuhimu wa nishati mbadala, tunafahamu changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na changamoto za mazingira kwa ujumla. Hii ni ajenda ambayo Mhe, Rais ameibeba kwa dhati kabisa kuhakikisha tunaanza mchakato wa kuelimishana kuondokana na nishati ambazo sio rafiki kwa mazingira na kutumia zilizo rafiki kwa mazingira.

Mkutano huo umeonesha namna mama zetu wanavyoteswa na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa. Lakini ajenda hiyo ya nishati mbadala siyo kwa ajili ya akina mama tu, lakini wote tunafahamu nguvu na mchango wa vijana kwenye masuala ya mabadiliko chanya. Kwa hiyo ajenda hii ni lazima twende nayo pamoja wanawake, vijana, wazee na kila kundi kwenye jamii.

Ajenda ya matumizi ya nishati mbadala inabebwa na Serikali ya awamu ya sita na inatakiwa kuungwa mkono na wananchi wote ili kuweza kuboresha mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea hivi sasa duniani kote.

Mpango wa nishati safi ya kupikia, Mhe, Rais ameungwa mkono wa wajumbe wa mkutano baada ya kuguswa sana na madhara yatokanayo na matumizi ya kuni na mkaa na kuhaidi kuunga mkono juhudi za Mhe, Rais kwa kuweka ya mazingira ya matumizi ya nishati iliyo salama kwa mtumiaji na kwa mazingira, ubora, upatikanaji wake, gharama nafuu, rafiki kwa mazingira na iliyo endelevu.

Ukizingatia matumizi ya nishati za kupikia na kiwango cha matumizi yake kwa hapa nchini, kuni inaongoza kwa 63.5% ikifuatiwa na mkaa 26.2%, gesi oevu 5.1%, umeme 3% na 2.2% vyanzo vinginevyo.

Kutokana na matumizi makubwa ya mkaa na kuni, imechangia uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na ukataji miti. Pia, athari nyingine ni za kiafya kwa watumiaji wa nishati hizo ambapo vifo zaidi ya 33,000 hutokea kwa mwaka kutokana na kuvuta hewa ya ukaa.

Kutokana na juhudi hizo zinazofanywa na Mhe, Rais Dkt Samia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, pamoja na nishati isiyofaa kwa matumizi ya kupikia, tuungane kwa pamoja kuunga mkono juhudi zake ili kuipata Tanzania salama.

Tanzania ni moja, kwamwe haitogawanyika. Tuungane 2025 kusimama na Rais mwenye maono ya kulivusha Taifa letu. Dkt Samia anatosha.

 
Back
Top Bottom