DALLAI LAMA
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 8,651
- 2,627
Rais Samia
Pole na Majukumu ya Kuliongoza taifa.
Kwa niaba ya madereva Guide wa Utalii nipende kuelezea kero juu ya kona kali ya perving ya kupandia kutoka ndani ya Crater.
Mh Rais ni kwamba Mamlaka ya Ngorongoro imeshindwa kuchonga Mwamba hata mita mbili ili kuondoa wimbi la ajali inayotokea mara kwa mara.
Eneo hilo ni hatari na magari mengi hushindwa kuimaliza kona hiyo kwa kuwa ni Landcruiser warbus na pale unaporudi nyuma kuna hatari kubwa kwa kuwa ni shimo na hata wameshindwa kuweka vyuma pembezoni ili kuzuia ajali.
Wakati mwingine wageni huangua kilio pindi gari inaposhindwa kumaliza na kurudi nyuma
Rais Samia ikiwezekani turuhusiwe sisi tunaopita katika eneo hilo tuchonge kwa shoka kwani Adha imekuwa kubwa na wageni wanalalamika.
Rais Samia kero hii mara kadhaa tumekuwa tukiielezea NCAA ila hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na hivi karibuni kuna ajali kadhaa zimetokea katika eneo hilo la mlima mkali na kona kali.
Natanguliza Shukrani za dhati
N.B
Niipongeze mamlaka kwa ufuatiliaji wa mara kwa mara wa Barabara zake ambazo ni bora..ila tatizo letu ni Kona ya kubusu wakati unapanda toka Crater