Kuhamishwa kwa Wamisai Ngorongoro, tumechelewa lakini tumpongeze Rais Samia. Tujifunze Canada na tusahihishe

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Ni muda muafaka wa kumpongeza Rais Samia kwa kuwahamisha Wamasai na wakazi wengine ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kulingana na maamuzi kama hayo yaliyowahi kufanyika Canada na Marekani.

Tarehe 20 ya mwezi wa 7 kila mwaka nchini Canada wanasherehea ' National Park Day" sherehe ambayo Wacanada wanapewa ruhusa ya kutembelea hifadhi za Taifa bure.

Inasemwa kwamba furaha ya uwepo wa siku hii unachagizwa na maamuzi magumu na mazito yaliyochukuliwa miaka ya 1880 na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Taifa hilo la kuwahamisha wazawa na wakazi kwenye hifadhi za Taifa.

Mwaka 1887 hifadhi ya kwanza Canada na ya Tatu duniani inayoitwa "Banff National Park" ilianzishwa Kwa wazawa kuhamishwa tena kwa kutumia nguvu kubwa. Maamuzi hayo leo ndio yamesadia kukuza utalii ndani ya Canada na utalii unachangia pakubwa sana katika Pato la Taifa la pili kwa ukubwa Marekani ya Kaskazini.

Mchakato wa kuwahamisha wazawa kwenye hifadhi haukuishia hapo bali uliendelea kwenye hifadhi nyingine ndani ya Canada na Marekani.

Faida zilizopatikana/zinazopatika a maeneo husika Kwa kuwahamisha wakazi kwenye hifadhi:
Kwanza, kukuza utalii wa ndani na wa nje. Utalii kama chanzo kikubwa Cha mapato na fedha za kigeni kwa mataifa mengi, mataifa mengi yameangalia suala la kukuza utalii Kwa namna hii. Kama ilivyokuwa kwa hifadhi ya 'Banff' nchini Canada na hapa Tanzania utalii Ngorongoro utakua sana.

Pili, kulingana na mtazamo wa wahifadhi, Moja ya njia ya uhifadhi ni kuwatenganisha binadamu na viumbe wengine. Kwenye hifadhi Kuna viumbe vingi ambavyo ni urithi wa dunia, viumbe hivyo kuwa karibu na binadamu ni kuhatarisha uwepo wao. Ndio maana yanafanyika maamuzi ya kuwahamisha.

Hasara za kuwahamisha wazawa kwenye maeneo ya hifadhi:
Kwanza, kupotea kwa utamaduni wa wazawa na asili yao.

Pili, kama itatumika nguvu inawezekana wakapanga kurudi tena baadae Kwa hoja za kurejesha utamaduni na asili yao.

The way forward: Wazawa kama wahifadhi:
Ili kuepukana hasara za hapo juu nchini Canada walifanya makubaliano mbalimbali na wazawa na wazawa wakawa ni wahifadhi namba moja na haya ni baadhi ya makubaliano hayo:

Mwaka 1984 kulifanyika "Inuvialuit Final Agreement" ya kuruhusu wazawa kuwepo hifadhini Kwa kutengenewa eneo dogo ndani ya hifadhi ili waweze kudumisha mila, desturi na tamaduni zao.

Vivyo hivyo mwaka 1993 kulifanyika "Gwaii Haanas Agreement" kati ya Haida Nation na nchi ya Canada juu ya uhifadhi wa maliasili na utamaduni katika " Gwaii National Park Reserve"

Makubaliano kama hayo yanaendelea kwenye nchi nyingine nyingi mpaka Leo katika hoja kwamba WAZAWA NI WAHIFADHI.

The way forward: Hoja ya wazawa ni wahifadhi na suala la Ngorongoro:
Nadhani nasi pia tunaweza kwenda na hoja hiyo ya wazawa ni wahifadhi kwenye suala la Ngorongoro na Wamasai lakini iendane na mazingira ya kwetu.

Pawepo na makubaliano maalumu na wazee wa kabila la kimasai na Serikali, watengewe eneo kidogo ndani ya hifadhi ambalo watakuwa wanaishi humo. Hoja ya msingi ya kutengewa eneo hilo ni kuendeleza na kudumisha utamaduni wao na sio vinginevyo

Hitimisho,
Kama kichwa Cha mada kinavyosema uamuzi wa kuwahamisha Wamasai Ngorongoro ni sahihi na Rais Samia apongezwe Kwa hilo.

Kwa uelewa Zaidi, pitia mada hii website ya straight: Charlotte Dawe: Canadian parks-a dark history and a way forward
 
images - 2023-09-12T190146.837.jpeg
 
Wakati Nchi zilizofanya maangamizi dhidi ya Watu bara la Marekani kaskazini na Canada wakitafuta suluhu na Kuanza kutubu na kuomba misamaha ya kufanya Uangamizaji huko kwa karne na karne, leo hii anatokea mtu Kumpongeza Raisi wa Tanzania kufanya Uangamizaji wa watu wa Maasai.

Sijawahi kusema haya,..
Raisi Samia hastahili pongezi lelote lile likija suala la Wamasai.

Wanaangamia.

This is Pure Terrorism
 
WAZAWA KAMA WAHIFADHI

Kwetu haiwezekani kwani wafugaji wa kimasai wamekuwa wakitumiwa na matajiri wakubwa walioko ndani ya nchi na nchini Kenya kufugiwa mifugo yao humo Ngorongoro...

Hiki ni kitisho cha usalama wa wanyamapori......

Huko nyuma makubaliano yangewezekana lakini si sasa ambako SOKO HURIA na NGUVU YA PESA inatetemesha maadili na makubaliano .....

Naiunga mkono serikali yetu adhimu kuwahimishia wafugaji wa Ngorongoro huko Msomera Handeni

#SiempreJMT

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wazungu wenyewe wa Canada walipora hiyo nchi/ardhi yote na rasilimali zake zote kwa mabavu na udhalimu mkubwa sana kutoka kwa Wahindi wekundu, mfano wako hauna mashiko.
 
Kama uko katika zile NGO's zinazopokea mamia ya mamilioni kufuatilia maisha ya wamasai basi ni LAZIMA uumie kihisia na uishambulie serikali kwa kutumia WMD's za maneno

Nina jamaa zangu walio katika NGO's za ELIMU na AFYA....mapovu yanawatoka tu....

Daah nimekumbuka yale ya "wako wasiotaka HIV/AIDS ipate tiba

#Kongole Serikali Yetu Adhimu Kwa Uamuzi Wa Kulinda Hifadhi Zetu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Dunia itambue kwamba, Ndugu zetu Wamasai Wanateseka.

Wamasai ni wahanga wa Serikali ambayo imeshindwa kuwapa haki ya kumiliki na kuishi katika ardhi yao. Ni muhimu kuwawajibisha wale walio madarakani kwa matendo yao na kutetea haki za Jamii zilizotengwa.
 
Wazungu wenyewe wa Canada walipora hiyo nchi/ardhi yote na rasilimali zake zote kwa mabavu na udhalimu mkubwa sana kutoka kwa Wahindi wekundu, mfano wako hauna mashiko.
Lini ardhi kubwa zenye rutuba na raslimali zikapatikana kwa kugawana kwa nderemo ,vifijo na tafrija?!!!

Huku mitaani kuna kesi kibao za majirani kulumbana kisa mipaka ya "viwanja" na kufikia kutosalimiana ,kupelekana kwa wajumbe ,polisi na hata kutumiana nguvu za "giza"....

Mkuu naongelea UHALISIA kinyume na HISIA

#YerzerHatov
#DoNotDoHarm

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Dunia itambue kwamba, Ndugu zetu Wamasai Wanateseka.

Wamasai ni wahanga wa Serikali ambayo imeshindwa kuwapa haki ya kumiliki na kuishi katika ardhi yao. Ni muhimu kuwawajibisha wale walio madarakani kwa matendo yao na kutetea haki za Jamii zilizotengwa.
Kakupiga katika "mshono"?!!!

Watu wa NGO's za hifadhini mule sasa mapovu yamekuwa yakiwatoka mno....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wakati Nchi zilizofanya maangamizi dhidi ya Watu bara la Marekani kaskazini na Canada wakitafuta suluhu na Kuanza kutubu na kuomba misamaha ya kufanya Uangamizaji huko kwa karne na karne, leo hii anatokea mtu Kumpongeza Raisi wa Tanzania kufanya Uangamizaji wa watu wa Maasa...
Maamuzi ya kuwepo "National Park Day" yamekuja miaka 100 baada ya mpango wa kuhamisha watu hifadhini kutekelezwa. Mpango umetimia na Sasa Canada ni nchi yenye vivutio Bora vya utalii.

Wanachofanya Sasa ni kutoa elimu ya kutosha Kwa hao wazawa ili wasiharibu hifadhi halafu wanaruhsiwa kurudi.

Acha mama naye afanye miaka 100 ijayo watafuruhia maamuzi yake
 
Kama uko katika zile NGO's zinazopokea mamia ya mamilioni kufuatilia maisha ya wamasai basi ni LAZIMA uumie kihisia na uishambulie serikali kwa kutumia WMD's za maneno

Nina jamaa zangu walio katika NGO's za ELIMU na AFYA....mapovu yanawatoka tu....

Daah nimekumbuka yale ya "wako wasiotaka HIV/AIDS ipate tiba

#Kongole Serikali Yetu Adhimu Kwa Uamuzi Wa Kulinda Hifadhi Zetu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Huna hoja.
 
Maamuzi ya kuwepo "National Park Day" yamekuja miaka 100 baada ya mpango wa kuhamisha watu hifadhini kutekelezwa. Mpango umetimia na Sasa Canada ni nchi yenye vivutio Bora vya utalii.

Wanachofanya Sasa ni kutoa elimu ya kutosha Kwa hao wazawa ili wasiharibu hifadhi halafu wanaruhsiwa kurudi.

Acha mama naye afanye miaka 100 ijayo watafuruhia maamuzi yake
Hakika

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkimaliza kuuza Ngorongoro na Loliondo uzeni na mlima Kilimanjaro msisahau na Saanane Island hata ikulu ya Magogoni nayo msiache kuipiga bei,, siku umbumbumbu ukituisha tukute kila kitu ni cha wazungu na waarabu,,
 
Kakupiga katika "mshono"?!!!

Watu wa NGO's za hifadhini mule sasa mapovu yamekuwa yakiwatoka mno....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ndio nimesema wewe mleta mada ni Magaidi. Itoshe, badala ya kutetea hoja yenu mnaanza kunishambulia. Mtashindwa na mtalegea.

Narudia, Nyie ni magaidi, hamna tofauti na Magaidi na madhalimu wengine hapa Duniani.

Roho zenu zinaungua na mtaendelea kuungua mbeleni. Mlegee.
 
Mzungu hapendi ujue kuvua samaki anataka akuvulie akupatie. Kitendo Cha kuhamisha wazawa ni siri ya utalii endelevu. Binadamu anahatarisha maisha ya viumbe hai hifadhini ambavyo kimsingi vikitoweka hakuna utalii. Sasa unataka Siri hiyo upewe na wazungu?

Waliwafukuza kwanza waliopona hifadhi zimejaa viumbe wanavyotaka wakawarejesha lakini wamepewa elimu za uhifadhi na zaidi hawafanyi shughuli zozote za uzalishaji kama kilimo au ufugaji ndani ya hifadhi zaidi ya kuendeleza tamaduni zao.
 
Maamuzi ya kuwepo "National Park Day" yamekuja miaka 100 baada ya mpango wa kuhamisha watu hifadhini kutekelezwa. Mpango umetimia na Sasa Canada ni nchi yenye vivutio Bora vya utalii.

Wanachofanya Sasa ni kutoa elimu ya kutosha Kwa hao wazawa ili wasiharibu hifadhi halafu wanaruhsiwa kurudi.

Acha mama naye afanye miaka 100 ijayo watafuruhia maamuzi yake
Raisi Samia ashutumiwe na Kulaaniwa kwa Nguvu zote na Watanzania wote wapenda haki.

Back
Top Bottom