Rais Samia ashiriki maadhimisho ya miaka 60 ya Mkoa wa Singida, leo Oktoba 16, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki maadhimisho ya miaka 60 ya mkoa wa Singida na kuhutubia mkutano wa hadhara uwanja wa Bombadia mkoani Singida leo tarehe 16 Oktoba, 2023.

View: https://www.youtube.com/live/K8j7hmFrrgQ?si=gNNG4Lv6ssAf5wxO

26e8ca69-c921-4d47-9dbe-571f97a25949.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watoto wa Kijiji cha Msingi mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Mkalama Mkoani Singida.
7a8f6a78-b4b9-414e-9bfd-508e01c5f0cd.jpeg

b7ac75f1-8dcb-4e52-9547-405840741ba8.jpeg

Viongozi mbalimbali pamoja na Wageni waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023.

a9f5ece6-8f41-43f3-a28c-0ef372d6a789.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba mara baada ya kufungua Rasmi Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023.

016c8214-72c9-44b9-bb82-a193a13c70bf.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Mkalama mara baada ya kufungua Rasmi Daraja la Msingi Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023.​
 
Singida kumbe ni mkoa tangu 1963 lakini bado hauna maendeleo? hatari sn
Kwani nchi yenyewe ya Tanzania ina maendeleo gani?? toka uhuru??, umeme na maji safi ya bomba ni shida mpaka leo. Elimu imedumaa, vilaza kibao wanahitimu UDSM siku hizi. Kiufupi tu nchi imeoza hii, inapitwa hadi na Rwanda ambao 1994 walikua na vita ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Mkuu ufukara wa Singida huwezi kulinganisha na Arusha, Mbeya, Dar, Mwanza, Kagera, KIlimanjaro n.k
 
Matumizi mabaya ya pesa za umma
Lissu anawaogopesha
Hivi mafaili huwa yanasomwa kweli? au kazi ni ziara ziara uteuzi utenguzi vichambo na kuuza……
 
kwa mara ya kwanza nasikia birthday ya mikoa, kwamba kila mkoa utafanya maadhimisho? na vipi ukawa utaratibu kila mwaka watu wanapiga party ya mkoa, au ni fursa ya kutafuna mapato ya halmashauri
 
Tunaongelea unafuu wa maisha asee, Singida hapana imezidi mkuu, nyumba za tembe
Nyumba za tembe hata hapo hapo makao makuu yenu ya nchi Dodoma zipo tele, tena sio mbali Ihumwa tu hapo au Bahi. Mikoa karibu yote ukiondoa Kilimanjaro zina nyumba za udongo manyasi na matembe. Hadi hapo Dar toka kidogo uelekee huko pugu, bagamoyo hadi chalinze kuna nyumba za udongo na miti. Hamna unafuu wowote nchi yote ni masikini tu. Umeme na maji shidaa.
 
Siyo kweli, nyumba za udongo kweli zipo lakini siyo nyumba za tembe, nimezunguka mikoa mingi sn lakini ufakara wa Singida ni aibu, Dodoma ni wapuuzi fulani hawana tofauti na Singida, siyo rahisi kukuta mgogo ni tajiri
 
Back
Top Bottom