Rais Samia anafanya kile ambacho wengi wenye akili tunataka afanye! Kwa hili anastahili pongezi

We kima, utalambaje asali wakati vitalu vyote ni mali ya msoga? Kwani shida ya Tanzania unaifahamu wewe?

Tatizo si kukosa watalii, bali mapato yake yanakwenda wapi?

Kama unasikiliza bunge mlilotaka liwe live, iko hivi MSD wanatumia sh 117m kununua dawa ambayo kwenye soko la dunia ni sh 32m tu.

Hata Tanzania tupate fedha kiasi, tutabaki maskini kwa kuwa matumizi hayana huruma na Watanzania.

Ndipo utaona Magufuli anathamani kubwa kiasi kwenye kupambana na hilo.
Tupe ushahidi wa umiliki wa hivyo vitalu kwa huyo msoga!

Tatizo unalolisema la Msd umeligundua baada ya huyo Samia kuweka mambo wazi na hadi aliposema wanatakiwa kufanya mabadiliko! Ndo mana akateua Mtendaji Mkuu mpya
 
Hapo wenye akili mnataka nini? Mfumo wetu wa maisha ndicho kikwazo kwa watalii.
Mfumo wa Maisha unahusianaje na kuwa kikwazo kwa watalii?

Kama highest no ya watalii tuliyowai kupata tangu Tanzania kuwai kuwapo ni 2.7 Milion inamaanisha tukifanya zaidi tunaweza fikisha hata 10 Mil. Kikubwa ni jitihada ikiwemo kujitangaza bila kuchoka
 
Yani wee jamaa bado mawazo yako ni ya kizamani mno.Rasilimali kubwa ambayo tunatakiwa kuiendeleza ni akili ya watu wetu (human resource).Hii ikiwa kubwa rasilimali nyingine zote zitakuwa na maana vinginevyo zitabakia kuwa takataka tu. DR Congo wana rasilimali nyingi mno kuliko hata zilizopo Tz lakini kwa sababu ya kukosa akili wamebaki kuuana wenyewe kwa wenyewe na kubakia masikini.Hivyo mimi ningekuelewa kama ungezungumzia kuwekeza vya kutosha ktk elimu.
 
We kima, utalambaje asali wakati vitalu vyote ni mali ya msoga? Kwani shida ya Tanzania unaifahamu wewe?

Tatizo si kukosa watalii, bali mapato yake yanakwenda wapi?

Kama unasikiliza bunge mlilotaka liwe live, iko hivi MSD wanatumia sh 117m kununua dawa ambayo kwenye soko la dunia ni sh 32m tu.

Hata Tanzania tupate fedha kiasi, tutabaki maskini kwa kuwa matumizi hayana huruma na Watanzania.

Ndipo utaona Magufuli anathamani kubwa kiasi kwenye kupambana na hilo.
Kuhusu wizi, ufisadi na ubadhirifu, umesema vema. Ni tatizo kubwa kwa nchi yetu.

Ulipoharibu ni pale uliposema eti Magufuli aliamua kupambana na hili. Ukweli ni kwamba Magufuli.aliwazuia au kuwaondoa wevi, mafisadi na wabadhirifu wa mwanzo, kisha akatengeneza wa kwake, huku yeye mwenyewe akishiriki kikamilifu katika uovu huo, wakati huo huo akiwapumbaza watu kuwa anapambana na uovu.

Report ya CAG, imeweka wazi ambayo wengi wa waliopumbazwa na uwongo wa marehemu Magufuli, ambapo watu wake wa karibu wakiwa ndiyo mirija ya kuibia pesa ya umma. Mayanga ni mfano wa awali.
 
Tupe ushahidi wa umiliki wa hivyo vitalu kwa huyo msoga!

Tatizo unalolisema la Msd umeligundua baada ya huyo Samia kuweka mambo wazi na hadi aliposema wanatakiwa kufanya mabadiliko! Ndo mana akateua Mtendaji Mkuu mpya
Nakubaliana nawe. Uchafu wa MSD umewekwa wazi na utawala wa Samia. Utawala wa Magufuli uliulinda wizi wa MSD kama ulivyoulinda uharamia wa akina Sabaya, Makonda, Mayanga, na wengine wengi watu wake wa karibu.
 
Hayo madudu ni bajeti ya 2021/2022 ambayo inaendelea kutekelezwa. Meanwhile mama kaanza nayo na anaitekeleza.

Wachota hela hiyo ni timu msoga kwa taarifa yako. Na mama hawezi wadhibiti hao kwa kuwa ndo wanamlinda na kuongoza nchi.

Kwani January amewekwa pale na nani kukatakata umeme.

Kwani kodi utitiri za miamala kila nahali zimewekwa na nani. Na je fedha lukuki za miamala zinaketa madiliko gani ya maendeleo tangu zianze mwaka jana.

Ester Bulaya alisema hakuna barabara mpya zinazojengwa tangu mrithi wa marehem ashike kijiti. Ulimwelewa?

Kwa ujumla spidi ya maendeleo imerudi nyuma. Mama anabadilshia baibui kwenye ndege. Ana safari nyingi za nje kuliko za kutembelea wananchi.
 
Kwa miaka mingi sana Tanzania tumekuwa tunalalamika jambo moja kuu, nalo ni kwamba, pamoja na kuwa na maliasili na utajiri mwingi ila nchi yetu hasa wananchi wamekuwa masikini sana!

Mjadala huu umezungumzwa na kipindi kirefu sana na moja ya sababu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa Tanzania kuendelea kuwa masikini pamoja na kuwa na utajiri na Maliasili nyingi ni kwa sababu tumekuwa hatutumii utajiri wetu vizuri ikiwemo kuutangaza kwa dunia ili utunufaishe kiuchumi! Siku zote biashara ni Matangazo!

Kwenye hili suala napenda leo nikiri kuwa Rais Samia ameanza kulipatia majibu suala hili!

Kwa Bara la Afrika, nchi zinazoongoza kwa kupokea watalii wengi ni Morocco, Algeria, Misri na South Africa. Nchi hizi zinapokea watalii zaidi ya Mil 5 hadi Mil 10 kwa mwaka. Na kusema kweli hizi nchi utalii unazinufaisha sana! Kiuhalisia hizi ndo nchi zenye Uchumi mkubwa Afrika na ndo zinaongoza kwa kuwa na chumi imara na maisha bora kwa sehemu kubwa ya wananchi wake!

Ila kwa uhalisia, Kama umetembelea nchi hizi zinazoongoza kwa utalii Africa utagundua kuwa hazina kitu kikubwa kuizidi Tanzania na ukweli ni kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kuzizidi nchi zote hizi.

Kwa South Africa tu! Watalii wengi hupenda kutembelea makumbusho ya Mandela, beach za Cape Town na Mbuga maarufu ya Kruger National Park.

Kiuhalisia Tanzania tuna makumbusho nzuri za freedom fighters wa kusini mwa Afrika zilizopo Bagamoyo, Morogoro na Mtwara na pia Makumbusho ya Mwalimu Nyerere ambae kwa sehemu kubwa anaheshimika sana duniani. Ukiuliza kwa nini hazifahamiki jibu ni moja tu! Hatujazitangaza vya kutosha duniani huko! Na huu ndo ukweli! Vitu vyetu vizuri hatuvitangazi !

Kwa Kruger National Park ya South Afrika Hii ni sawa na nusu au robo ya Mikumi National Park. Kwa idadi ya wanyama haifikii Serengeti au Selous hata kwa robo tu, Ila Leo hii duniani huko ni watu wachache sana wanaijua Selous. Pamoja na Serengeti na Ngorongoro kufahamika ila bado hatujazipa promo za kutosha duniani huko! Selous ambayo kiuhalisia ina wanyama wengi kuliko hata Serengeti haitembelewi hata na watalii 10000 tu kwa mwaka na sababu kuu ni kwamba hatujaitangaza na haijulikani! Kweli kwa muda mrefu tumekuwa kichwa cha mwenda Wazimu!

Kwa beach za Cape Town hizi kwa uzuri hazifikii hata robo kwa uzuri compared na beach za Zanzibar na Mafia! Ila still wao beach zao zinatwmbelewa na watalii wengi kuliko beach zetu za Zanzibar na Mafia. Shida ni moja tu! Tumekuwa hatujitangazi na kujiuza kwa dunia ipasavyo!

Kabla ya COVID , sekta ya utalii ndo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa zaidi katika kuingiza fedha za kigeni na kwenye pato la Taifa! Imekuwa ikifanya hivi huku Tanzania ikiwa haijawai kupokea Watalii Milioni 3 tu tangu kupata uhuru! Fedha hizi ndo zimekuwa zikiendesha nchi, kulipa mishahara na kununua madawa! Swali la kujiuliza ni Je hali ingekuwaje Tanzania ingekuwa inapokea watalii Milioni 5 au 7 au 8 au 10 kwa mwaka? Leo hii si tungekuwa na maendeleo makubwa sana?

Kusema kweli napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa Hii Royal Tour, napenda sana tufanye season 2 ya Royal Tour ambapo tuionyeshe Dunia makubwa zaidi yaliyopo Tanzania.

Napenda kushauri kuwa sasa kuwe na Tangazo la kuitangaza Tanzania kwenye channel kubwa kama CNN, Al Jazeera na BBC, kuwe pia na Matangazo ya Tanzania kwenye klabu kubwa duniani kama Barcelona au Real Madrid au Liverpool au Chelsea

Tuvute mikataba nao na tuuze bidhaa zetu hata korosho na kahawa kwenye stadiums zao!

Hongera Rais Samia! Umeanza vizuri, Royal Tour iwe mwanzo tu na wala usiloose focus kwenye hili! Hayo ndo maono ya Rais!
Dogo wacha kulamba mavi ya watu....hii kazi afanyayo rais ni kazi wanaifanya mabalozi wetu na maofisa wao. Mama anapoteza muda tu na pesa za wananchi kuzunguka maduniani kuitangaza Tanzania.
 
Mfumo wa Maisha unahusianaje na kuwa kikwazo kwa watalii?

Kama highest no ya watalii tuliyowai kupata tangu Tanzania kuwai kuwapo ni 2.7 Milion inamaanisha tukifanya zaidi tunaweza fikisha hata 10 Mil. Kikubwa ni jitihada ikiwemo kujitangaza bila kuchoka
Lazima uwe na sehemu za kufikia watalii zenye kuwavutia, mfano hoteli zilizo rafiki na kambi zilizo rafiki, pia uwe na waongoza watalii wanaojua lugha kulingana na mtalii na wasiwe wababaishaji. Ubabaishaji na ukwapuaji ndio mtindo wetu wa maisha, ukweli kwetu ni tatizo.
 
Wanaoumia ni either washamba au hawana ufahamu na jinsi dunia inavyo operate tu!

Ni wa kuonewa huruma tu
ukisema tutumie gharama kubwa kuutngaza utalii na wakati huku ndani ya nchi miundo mbinu ya kufika kwenye hizo sehemu ili watalii wapelekwe haipo sawa. utakuwa tabularasa. miundo mbinu ya hotels barabara bado sio rafiki. taasisi zinazosimamia utalii zenyewe ni mkanganyiko haileweki nani ni nani ukienda huku unakutana na TAWA huku TANAPA kule wengine vurugu tupu.
 
Acheni kusifia upuuuzi. Tanzania imeanza harakati za kutangaza Utalii Duniani huyo Mtu wenu akiwa bado anasoma.
LIGI YA UINGEREZA EPL kwenye Uwanja wa timu ya SUNDERLAND nk matangazo ya Vivutio vya Tanzania yameanza kutangazwa miaka na miaka, halafu anakuja msugua gaga mmoja anataka kutuaminisha kwamba harakati zimeanza Awamu ya 6 kwamba Utalii ulikua hautangazwi. Kwa taarifa yako Ulaya na Marekani Wameeeshaenda hadi Waziri na Wasanii wa Bongo Movie kutangaza Vivutio mkuu usitiletee matapishi humu.
Kwanza inabidi wewe ndio uache matamko ya kuwapangia watu nini cha kuongea maana hizo zama hazipo tena.
Hamna mtu aliyesema kuwa matangazo ya utalii yameanza awamu hii. Hata hivyo kinachofanyika sasa ni revolutionary na kuendana na wenzetu hasa wenye uchumi unaotegemea Utalii. Ndivyo wanavyofanya.
Zile akili mgando za kuona kujifungia ndani tu ni ujasiri na kusafiri nje ni dhambi, dead and buried bandugu.
 
Kwa miaka mingi sana Tanzania tumekuwa tunalalamika jambo moja kuu, nalo ni kwamba, pamoja na kuwa na maliasili na utajiri mwingi ila nchi yetu hasa wananchi wamekuwa masikini sana!

Mjadala huu umezungumzwa na kipindi kirefu sana na moja ya sababu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa Tanzania kuendelea kuwa masikini pamoja na kuwa na utajiri na Maliasili nyingi ni kwa sababu tumekuwa hatutumii utajiri wetu vizuri ikiwemo kuutangaza kwa dunia ili utunufaishe kiuchumi! Siku zote biashara ni Matangazo!

Kwenye hili suala napenda leo nikiri kuwa Rais Samia ameanza kulipatia majibu suala hili!

Kwa Bara la Afrika, nchi zinazoongoza kwa kupokea watalii wengi ni Morocco, Algeria, Misri na South Africa. Nchi hizi zinapokea watalii zaidi ya Mil 5 hadi Mil 10 kwa mwaka. Na kusema kweli hizi nchi utalii unazinufaisha sana! Kiuhalisia hizi ndo nchi zenye Uchumi mkubwa Afrika na ndo zinaongoza kwa kuwa na chumi imara na maisha bora kwa sehemu kubwa ya wananchi wake!

Ila kwa uhalisia, Kama umetembelea nchi hizi zinazoongoza kwa utalii Africa utagundua kuwa hazina kitu kikubwa kuizidi Tanzania na ukweli ni kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kuzizidi nchi zote hizi.

Kwa South Africa tu! Watalii wengi hupenda kutembelea makumbusho ya Mandela, beach za Cape Town na Mbuga maarufu ya Kruger National Park.

Kiuhalisia Tanzania tuna makumbusho nzuri za freedom fighters wa kusini mwa Afrika zilizopo Bagamoyo, Morogoro na Mtwara na pia Makumbusho ya Mwalimu Nyerere ambae kwa sehemu kubwa anaheshimika sana duniani. Ukiuliza kwa nini hazifahamiki jibu ni moja tu! Hatujazitangaza vya kutosha duniani huko! Na huu ndo ukweli! Vitu vyetu vizuri hatuvitangazi !

Kwa Kruger National Park ya South Afrika Hii ni sawa na nusu au robo ya Mikumi National Park. Kwa idadi ya wanyama haifikii Serengeti au Selous hata kwa robo tu, Ila Leo hii duniani huko ni watu wachache sana wanaijua Selous. Pamoja na Serengeti na Ngorongoro kufahamika ila bado hatujazipa promo za kutosha duniani huko! Selous ambayo kiuhalisia ina wanyama wengi kuliko hata Serengeti haitembelewi hata na watalii 10000 tu kwa mwaka na sababu kuu ni kwamba hatujaitangaza na haijulikani! Kweli kwa muda mrefu tumekuwa kichwa cha mwenda Wazimu!

Kwa beach za Cape Town hizi kwa uzuri hazifikii hata robo kwa uzuri compared na beach za Zanzibar na Mafia! Ila still wao beach zao zinatwmbelewa na watalii wengi kuliko beach zetu za Zanzibar na Mafia. Shida ni moja tu! Tumekuwa hatujitangazi na kujiuza kwa dunia ipasavyo!

Kabla ya COVID , sekta ya utalii ndo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa zaidi katika kuingiza fedha za kigeni na kwenye pato la Taifa! Imekuwa ikifanya hivi huku Tanzania ikiwa haijawai kupokea Watalii Milioni 3 tu tangu kupata uhuru! Fedha hizi ndo zimekuwa zikiendesha nchi, kulipa mishahara na kununua madawa! Swali la kujiuliza ni Je hali ingekuwaje Tanzania ingekuwa inapokea watalii Milioni 5 au 7 au 8 au 10 kwa mwaka? Leo hii si tungekuwa na maendeleo makubwa sana?

Kusema kweli napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa Hii Royal Tour, napenda sana tufanye season 2 ya Royal Tour ambapo tuionyeshe Dunia makubwa zaidi yaliyopo Tanzania.

Napenda kushauri kuwa sasa kuwe na Tangazo la kuitangaza Tanzania kwenye channel kubwa kama CNN, Al Jazeera na BBC, kuwe pia na Matangazo ya Tanzania kwenye klabu kubwa duniani kama Barcelona au Real Madrid au Liverpool au Chelsea

Tuvute mikataba nao na tuuze bidhaa zetu hata korosho na kahawa kwenye stadiums zao!

Hongera Rais Samia! Umeanza vizuri, Royal Tour iwe mwanzo tu na wala usiloose focus kwenye hili! Hayo ndo maono ya Rais!
Hongereni nyie wenye akili mbaya
 
Uchafu wa MSD umewekwa wazi na utawala wa Samia
Kuweka wazi ni jambo moja na kuchukua hatua ni jambo lingine.

Wananchi wanataka kuona hiyo ripoti ya CAG ikifanyiwa kazi. (Jambo ambalo nina hakika halitafanyika kwenye huu utawala) CCM ni mafia.
Sasa hivi wananchi wengi(hata upinzani) wanacheza ngoma ya hiki chama bila kujitambua.
 
Back
Top Bottom