Rais Samia anafanya kile ambacho wengi wenye akili tunataka afanye! Kwa hili anastahili pongezi

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,047
Kwa miaka mingi sana Tanzania tumekuwa tunalalamika jambo moja kuu, nalo ni kwamba, pamoja na kuwa na maliasili na utajiri mwingi ila nchi yetu hasa wananchi wamekuwa masikini sana!

Mjadala huu umezungumzwa na kipindi kirefu sana na moja ya sababu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa Tanzania kuendelea kuwa masikini pamoja na kuwa na utajiri na Maliasili nyingi ni kwa sababu tumekuwa hatutumii utajiri wetu vizuri ikiwemo kuutangaza kwa dunia ili utunufaishe kiuchumi! Siku zote biashara ni Matangazo!

Kwenye hili suala napenda leo nikiri kuwa Rais Samia ameanza kulipatia majibu suala hili!

Kwa Bara la Afrika, nchi zinazoongoza kwa kupokea watalii wengi ni Morocco, Algeria, Misri na South Africa. Nchi hizi zinapokea watalii zaidi ya Mil 5 hadi Mil 10 kwa mwaka. Na kusema kweli hizi nchi utalii unazinufaisha sana! Kiuhalisia hizi ndo nchi zenye Uchumi mkubwa Afrika na ndo zinaongoza kwa kuwa na chumi imara na maisha bora kwa sehemu kubwa ya wananchi wake!

Ila kwa uhalisia, Kama umetembelea nchi hizi zinazoongoza kwa utalii Africa utagundua kuwa hazina kitu kikubwa kuizidi Tanzania na ukweli ni kuwa Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kuzizidi nchi zote hizi.

Kwa South Africa tu! Watalii wengi hupenda kutembelea makumbusho ya Mandela, beach za Cape Town na Mbuga maarufu ya Kruger National Park.

Kiuhalisia Tanzania tuna makumbusho nzuri za freedom fighters wa kusini mwa Afrika zilizopo Bagamoyo, Morogoro na Mtwara na pia Makumbusho ya Mwalimu Nyerere ambae kwa sehemu kubwa anaheshimika sana duniani. Ukiuliza kwa nini hazifahamiki jibu ni moja tu! Hatujazitangaza vya kutosha duniani huko! Na huu ndo ukweli! Vitu vyetu vizuri hatuvitangazi !

Kwa Kruger National Park ya South Afrika Hii ni sawa na nusu au robo ya Mikumi National Park. Kwa idadi ya wanyama haifikii Serengeti au Selous hata kwa robo tu, Ila Leo hii duniani huko ni watu wachache sana wanaijua Selous. Pamoja na Serengeti na Ngorongoro kufahamika ila bado hatujazipa promo za kutosha duniani huko! Selous ambayo kiuhalisia ina wanyama wengi kuliko hata Serengeti haitembelewi hata na watalii 10000 tu kwa mwaka na sababu kuu ni kwamba hatujaitangaza na haijulikani! Kweli kwa muda mrefu tumekuwa kichwa cha mwenda Wazimu!

Kwa beach za Cape Town hizi kwa uzuri hazifikii hata robo kwa uzuri compared na beach za Zanzibar na Mafia! Ila still wao beach zao zinatwmbelewa na watalii wengi kuliko beach zetu za Zanzibar na Mafia. Shida ni moja tu! Tumekuwa hatujitangazi na kujiuza kwa dunia ipasavyo!

Kabla ya COVID , sekta ya utalii ndo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa zaidi katika kuingiza fedha za kigeni na kwenye pato la Taifa hapa Tanzania! Imekuwa ikifanya hivi huku Tanzania ikiwa haijawai kupokea Watalii Milioni 3 tu tangu kupata uhuru! Fedha hizi ndo zimekuwa zikiendesha nchi, kulipa mishahara na kununua madawa! Swali la kujiuliza ni Je hali ingekuwaje Tanzania ingekuwa inapokea watalii Milioni 5 au 7 au 8 au 10 kwa mwaka? Leo hii si tungekuwa na maendeleo makubwa sana?

Kusema kweli napenda kumpongeza sana Rais Samia kwa Hii Royal Tour, napenda sana tufanye season 2 ya Royal Tour ambapo tuionyeshe Dunia makubwa zaidi yaliyopo Tanzania.

Napenda kushauri kuwa sasa kuwe na Tangazo la kuitangaza Tanzania kwenye channel kubwa kama CNN, Al Jazeera na BBC, kuwe pia na Matangazo ya Tanzania kwenye klabu kubwa duniani kama Barcelona au Real Madrid au Liverpool au Chelsea

Tuvute mikataba nao na tuuze bidhaa zetu hata korosho na kahawa kwenye stadiums zao!

Hongera Rais Samia! Umeanza vizuri, Royal Tour iwe mwanzo tu na wala usiloose focus kwenye hili! Hayo ndo maono ya Rais!
 
Watu wanaumia na hela anayolipwa mcheza ngoma wa kwenye promo. Utalii unahitaji serious promotion na ni gharama.
Kuna nchi kama Rwanda jambo hilo linafanywa na Rais mwenyewe kwa ukamilifu. Watanzania tumelala na siasa nyingi mno, kila mtu utadhani amewahi kuwa Rais.
 
Watu wanaumia na hela anayolipwa mcheza ngoma wa kwenye promo. Utalii unahitaji serious promotion na ni gharama.
Kuna nchi kama Rwanda jambo hilo linafanywa na Rais mwenyewe kwa ukamilifu. Watanzania tumelala na siasa nyingi mno, kila mtu utadhani amewahi kuwa Rais.
Wanaoumia ni either washamba au hawana ufahamu na jinsi dunia inavyo operate tu!

Ni wa kuonewa huruma tu
 
Acheni kusifia upuuuzi. Tanzania imeanza harakati za kutangaza Utalii Duniani huyo Mtu wenu akiwa bado anasoma.
LIGI YA UINGEREZA EPL kwenye Uwanja wa timu ya SUNDERLAND nk

Matangazo ya Vivutio vya Tanzania yameanza kutangazwa miaka na miaka, halafu anakuja msugua gaga mmoja anataka kutuaminisha kwamba harakati zimeanza Awamu ya 6 kwamba Utalii ulikua hautangazwi.

Kwa taarifa yako Ulaya na Marekani Wameeeshaenda hadi Waziri na Wasanii wa Bongo Movie kutangaza Vivutio mkuu usitiletee matapishi humu.
 
Acheni kusifia upuuuzi. Tanzania imeanza harakati za kutangaza Utalii Duniani huyo Mtu wenu akiwa bado anasoma.
LIGI YA UINGEREZA EPL kwenye Uwanja wa timu ya SUNDERLAND nk matangazo ya Vivutio vya Tanzania yameanza kutangazwa miaka na miaka, halafu anakuja msugua gaga mmoja anataka kutuaminisha kwamba harakati zimeanza Awamu ya 6 kwamba Utalii ulikua hautangazwi. Kwa taarifa yako Ulaya na Marekani Wameeeshaenda hadi Waziri na Wasanii wa Bongo Movie kutangaza Vivutio mkuu usitiletee matapishi humu.
Hizo harakati unazosema zilikuwa na consistency? Uliona muendelezo wowote?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hakika! Kwa jitihada hizi, wengi tutalamba asali
We kima, utalambaje asali wakati vitalu vyote ni mali ya msoga? Kwani shida ya Tanzania unaifahamu wewe?

Tatizo si kukosa watalii, bali mapato yake yanakwenda wapi?

Kama unasikiliza bunge mlilotaka liwe live, iko hivi MSD wanatumia sh 117m kununua dawa ambayo kwenye soko la dunia ni sh 32m tu.

Hata Tanzania tupate fedha kiasi, tutabaki maskini kwa kuwa matumizi hayana huruma na Watanzania.

Ndipo utaona Magufuli anathamani kubwa kiasi kwenye kupambana na hilo.
 
Kwahiyo harakati na consistency ni kukaa Marekani Wiki 2.
Wewe hiyo Consistency ya huyo unayemsifu umeipata wapi wakati tangu apewe kijiti ana siku 300s subir muda uongeee ndipo ulete ngonjera na mapambio sio huo uharo uharo wako.
Kukaa Marekani unamaanisha nini? Rais yupo Marekani Kikazi na anafanya kazi za kuliletea maendeleo Taifa huko Marekani! Shida iko wapi?

Unataka akae Tanzania tu Tanzania wakati kuna kazi muhimu za kufanya Marekani? Utakuwa na mtindio wa ubongo
 
Back
Top Bottom