Dugange Amshukuru Rais Samia Kurudisha Tabasamu Masaulwa

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Naibu Waziri Ofisi wa Tamisemi, Dk Festo Dugange amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumaliza changamoto ya muda mrefu ya zahanati katika Kijiji cha Masaulwa Kata ya Imalinyi Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.

Dk Dugange ametoa shukrani hizo wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo ambayo tayari imeshaanza kutoa huduma kwa wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Masaulwa, amesema kijiji hicho kwa muda mrefu kulikuwa hakina zahanati jambo ambalo lilikuwa linawalazimu wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya lakini ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia changamoto hiyo imepata tiba.

"Tunamshukuru Rais ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake ameleta kiasi ch Sh. Milioni 93.6 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hii ya kisasa sambamba na watumishi wawili kwa ajili ya kuhudumia afya za wananchi wa Masaulwa."
 
Huu ugonjwa wa kijinga wa kusifia unaharibu sn nchi yetu, nadhani wiki ijayo atakuja mwingine amshukuru Rais kwa kuleta mvua.
 
Back
Top Bottom