Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,675
- 40,928
Rais Samia wakati akirejea toka France na Belgium wakati akitoa salamu zake na asante kwa mapokezi pale uwanja wa Mwalimu Nyerere alisema kwamba wakati wa awamu ya tano mahusiano yetu na nchi za Ulaya yalilega sana ila kwa sasa amejitahidi kuyarejesha.
Observation yangu ndogo ya matendo yatokanayo na jitihada hizo za kurejesha mahusiano na nchi za ulaya yanaonesha kwamba kasi ya ukopaji na misaada toka nchi za Ulaya na taasisi za kifedha imeongezeka.
Rais mwenyewe anakiri kwamba kuna fedha zilikuwa withheld ila kuna possibility kubwa sasa zikaachiwa.
Kauli ya Rais Magufuli mara kwa mara ilikua kukataa mikopo na misaada yenye masharti magumu kwa Taifa.
Ushahidi wa kauli za Magufuli za kukataa kwa mikopo awamu ya tano ni kwa kauli ya Rais hivi majuzi kuwa kuna fedha zilizuiwa.
Kwakua sasa misaada na mikopo imeanza kumiminika kwa wingi ni wazi kwamba uongozi wa awamu hii unakubaliana na masharti ya mikopo hiyo.
Swala hapa la kujiuliza ni je masharti hayo yana madhara gani kwa Taifa letu.
Na kama yana faida basi tuambiwe faida hizo ni zipi?
Ninachoomba tu kwa Serikali ni kuwa makini wakati inapokubaliana na masharti hayo ya mikopo na misaada isiwe tunafanya tu kwa lengo la kuwafurahisha nchi za ulaya wakati kwa uhalisia tunaoumia ni sisi na vizazi vyetu huku wao na vizazi vyao wakinufaika.
Pia ningependa kujua, je ni lazima tukope na kupokea misaada toka nchi za Ulaya ili mahusiano yetu na wao yawe mazuri.
Kwani hatuwezi kuwa na mahusiano nao mazuri bila kukopa na kupewa misaada.
Nasema hivi kwani inaonekana kwamba kukopa na kuomba misaada ndio njia pekee ya kuwa na mahusiano mazuri na nchi za Ulaya.
Nachelea kusema kwamba Nchi za Ulaya zinanufaika mno na mikopo na misaada wanayotupa maana wasingepata hasira kwa sisi kukataa mikopo na misaada yao.
Tuwe makini.