Rais Samia amepoteza ushawishi kwa wananchi

Watu wa namna hii hata mkija kuongozwa na Malaika mtalalamika tu. Nahisi hata kujiongiza wenyewe ni ngumu. Na kwa namna hiyo basi kwa kuwa mmezoea kulalamika hata siku mkipewa nchi mtaanza kugombania vyeo na kuleta mgawanyiko mkubwa wa kikanda au ukabila katika nchi.
Pro-Chadema wengi wao ni watu wa kishikiwa akili wanakubalina kila pumba alimuladi ziwafurahishe tu eti wanakubalia mtaani kuna wafuasi wengi wa Chadema🤣🤣
 
Huu ndiyo ukweli, bila kumung'unya maneno rais Samia hana ushawishi mkubwa kwa wananchi.
Nimezunguuka mitaani na kutaka kujua maoni ya wananchi juu ya Rais Samia, wengi ninaozungumza nao ni kama wamepoteza hope kwa rais Samia.

Lakini kitu kingine nilichonotice ni kuwa wananchi wako aware sana na yanayoendelea nchini ila wengi wana fatigue (uchovu wa kisiasa) baada ya system systematically kutumia nguvu kubwa kuvunja taasisi huru za kisiasa nchini.

Hii systematic approach ya dola kusilence wananchi na Taasisi zao za kisiasa imeanza kupelekea imani kwa wananchi kuwa siasa pengine siyo njia itakayopelekea mabadiliko ya msingi katika nchi yao.

Kuna watu wanawaombea mabaya viongozi wao, wanatamani mabaya yawafike n. k

Pia hali ngumu ya maisha, bei za mafuta ya kula, sukari, tozo, miamala, kodi za Luku na huduma mbalimbali kuwa juu kumeleta kinyongo kikubwa sana kwa wananchi dhidi ya serikali ya Samia.
Pia na kauli zake tata kama vile wananchi wamekubali tozo etc

Pia Chadema ina wafuasi wengi nchini, wananchi wengi wenye kufuata siasa za mrengo wa upinzani wana chuki na Rais Samia, wanamuona kama muonevu, mtu anayeendesha nchi kwa kufuata siasa za kibabe, hii ni kutokana na kuamua kutumia ubabe kuvunja katiba na sheria hasa inapokuja suala la vysma vya siasa kufanya siasa

Huku mtaani, wananchi hawamuelewi kabisa Samia, tofauti na zile siku zake 100.

Kama hawaamini basi wafanye tafiti watajionea wenyewe namna Samia alivyopoteza Support mtaani
Nahisi kuna ukweli kwenye hoja hii, kingine ni Rais kupoteza nguvu kwa vyombo vya dola hasa Police na wizara ya fedha. Hii ni hatari sana, je nani atakaetupa hali ya uchumi wetu ipoje kwani hizi tozo ni nyingi ni dalili ya kukosa uwezo wa kukusanya kodi kwenye vianzio vya kawaida kama biashara, exports, kilimo, nk. kwani vyanzo hivi vya tozo vinaonekana kama ni vya mpito tu kwani nchi haendeshwi kwa ukandamizaji w wananchi wake.
 
Back
Top Bottom